Pre GE2025 Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Pre GE2025 Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ni Mbowe au Lissu

  • Mbowe

    Votes: 179 14.7%
  • Lissu

    Votes: 1,038 85.3%

  • Total voters
    1,217
  • Poll closed .
Wakuu,

Leo mbali na kuwa ni Uchaguzi Mkuu wa CHADEMA pia wanasherekea Miaka 32 ya CHADEMA kupata Usajili wa Kudumu, ambapo ulipatikana Januari 21, 1993.


Mbivu na mbichi kujulikana leo, tumeona mengi na kusikia mengi kila upande ukitetea kwake. Je, nani ataibuka kidedea? Nani atatolewa kimasomaso na wajumbe?

Katika uchaguzi huu wajumbe watachagua Mwenyekiti Taifa pamoja na Makamu Mwenyekiti kwa Bara na Zanzibar, ambako ushindani mkubwa upo kati ya Mbowe na Lissu kwa nafasi ya Uenyekiti, na Wenje na Heche kwa nafasi ya Umakamu Uenyekiti.


Je, ni Mbowe au Lissu? Ni Heche au Wenje?

Orodha ya Wagombea wote ni;

Mwenyekiti Taifa
  • Freeman Mbowe
  • Odero Odero
  • Tundu Lissu
Makamu Mwenyekiti Bara
  • Ezekia Wenye
  • John Heche
  • Mathayo Gekul
Makamu Mwenyekiti Zanzibar
  • Hafidh Saleh
  • Said Issa Mohammed
  • Said Mzee Said
  • Suleiman Makame Issa


Wagombea Wanatoa Salamu kwa Wageni Waalikwa na Wapiga Kura

Tundu Lissu


Lissu amshukuru Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe kwa kufanya nae kazi kwa kipindi cha miaka 20, licha ya kutofautiana kimitazamo lakini amekiri hawajawahi kugombana.

"Nimekaa pembeni ya Mwenyekiti wetu wa Chama mfululizo kwa miaka zaidi ya 20 na katika kipindi chote hicho hatajawahi kugombana, hatujawahi kupigana mimi na yeye binafsi. Ndio tumetofautiana kimsimamo lakini hatujawahi kugombani"

"Vyovyote itakavyokuwa leo, tutakuwa pamoja katika kukijenga chama chetu (Chadema)"

Freeman Mbowe

"Hiki chama tunawajibu wote wa kibinadamu na Wakimungu wakukilinda kwa gharama yoyote ile, na chama hiki hatutakiruhusu kwa gharama yoyote eti kwasababu pengine kura za mbowe hazikutosha au kura za Mhe. Lissu hazikutosha ama za Mhe. Odero yule mzee wetu wa kesho kuna mwanga kwamba kura hazijatosha".

"Uchaguzi huu usiwe vita unapashwa kuwa furaha ya ujenzi wa demokrasia"

"Wako watabiri wengi sana wamesema kuhusu uchaguzi wa CHADEMA, Mhe. Mbowe unaenda kukipasua chama, Mhe. Mbowe inakuaje, hawa ni wanademokrasia, wote kama mnavyowaona. Tofauti zetu kwenye mitazamo hii naamini tunakwenda kuizika mwisho wa kikao hiki tunanelea mbele stronger together"

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, ametoa taarifa kwa ufupi kuhusiana na hali halisi ya Uchaguzi Mkuu wa Wabunge na Urais wa mwaka 2020.

Mnyika asoma maazimio ya kamati kuu kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa (2024), ambapo yatapelekwa Mkutano Mkuu kwaajili ya kupendekezwa kupitishwa kama maadhimio ya mkutano mkuu wa chama.

Mnyika amehitimisha kwa kuwasilisha mapendekezo ya maazimio ya Mkutano Mkuu

Updates za Matukio

Waambieni kabisa team FAM hakutakuwa na dakika za nyongeza. Tunamaliza hii ngwe ndani ya dakika 90 maana naona team FAM wanapoteza sana muda kwa kusoma hotuba ndefu kama safari ya kwenda mwezini
 
kwani ratiba yao inaonyesha zoezi la upigaji kura litaanza muda gani hasa na litamalizika muda gani?
tundu lisu tayari ameshapigwa bao la kisigino!
uchaguzi kufanyika usiku!!??tundu lisu tayari Hana chake
Anapita kweupee
 
Taarifa ndio kama unavyoisoma, hii ndio maana halisi ya Stronger Together.

Pamoja na mashambulizi yote ya mitandaoni lakini hali ndio kama mnavyoona.

Screenshot_2025-01-21-16-17-47-1.png
 
Katika uchaguzi huu wajumbe watachagua Mwenyekiti Taifa pamoja na Makamu Mwenyekiti kwa Bara na Zanzibar, ambako ushindani mkubwa upo kati ya Mbowe na Lissu kwa nafasi ya Uenyekiti, na Wenje na Heche kwa nafasi ya Umakamu Uenyekiti.
 
Back
Top Bottom