Pre GE2025 Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ni Mbowe au Lissu

  • Mbowe

    Votes: 179 14.7%
  • Lissu

    Votes: 1,038 85.3%

  • Total voters
    1,217
  • Poll closed .
Ukiskia neno "mnyukano" kwenye uchaguzi basi shurti uende hadi asubuhi. Sio zile chaguzi za mshindi 99.9% matokeo saa kumi jioni
 
Ni halali wajumbe wapokee rushwa hili zoezi sio dogo ukileta uyesu ukajifanya mzalendo sana nayo jau unaweza kujikuta umesanda.

Sema wafanye nao u-turn kama ile ya Wenje wamgeuke aliyewapa rushwa kura ziende kwa Lissu.
 
Sema ile Hotuba ya Katibu Mkuu imechangia sana kupoteza muda.
Mambo mengi sana. Mkutano muhimu kama huu ulipaswa ujielekeze kwenye mambo ya msingi tu.

Halafu muda wa kuanza shughuli yote ulikuwa umeenda sana. Walipaswa kuanza saa tatu asubuhi. Kama wajumbe walifika tangu juzi (tarehe 20), kulikuwa na sababu gani kuchelewa kuanza mkutano?

Ulitakiwa uwepo mfumo mzuri wa kuwahakiki wajumbe kabla na baada ya leo. Kuitana majina haikuwa na sababu.

Kwenye kujieleza, hakukuwa na sababu yoyote ya kuwauliza maswali wagombea. Walipaswa tu kupewa dakika 5 kila mmoja - wajieleze na kuomba kura.

Taarifa za chama zilipaswa ziwe zimetolewa mapema kwa wajumbe wote kabla ya mkutano. Katibu alipaswa kufanya majumuisho ya mambo makuu tu.

Nidhamu na utulivu hakuna. Hii pia imechangia kupoteza muda mwingi mno. Hadi wajumbe watulie, tayari mnajikuta mmekula dakika 5 au zaidi.
 
Hakuna uchaguzi wa hivi ni uhuni uchaguzi hauishi
 
Wanajifunza pia kwa zama hizi za kidigitali tuseme katibu ni mzembe
 
Walikuwa na muda wa kutosha kabisa kufanya maandalizi ya huo uchaguzi.

Walishindwa nini kupanga kufanya Mapema huo uchaguzi wao?

Yaani uchaguzi mdogo namna hiyo wa watu wasiozidi hata 5,000 unachukua muda wote huo?!!

Bad organization skills.

Au kuna figisu?
 
Ukiskia neno "mnyukano" kwenye uchaguzi basi shurti uende hadi asubuhi. Sio zile chaguzi za mshindi 99.9% matokeo saa kumi jioni
Kawaida kwa uzoefu weru ukiona kuna uchelewwshaji wa mambo ujue aliyeahikikia kiti huwa amekula za uso so inaangakiwa namna ya kufanya
 
Lakini kwa namna nyingine naweza kusema wapo sahihi.

Kumbuka huu ni mkutano Mkuu.

Kwenye mkutano mkuu kunakuwa na mambo mengi zaidi ambayo yanachukua muda.

Lakini idadi ya wajumbe nayo imechangia kula muda. Kwenye mabaraza wajumbe walikuwa 300 lakini zoezi lilikamilika kwa saa zaidi ya 24.

Hata hivyo kulikuwa na mambo mengi ambayo hayakuwa ya umuhimu yaliyofanyika ikiwemo kugawa pesa manually kwa wajumbe jambo ambalo lilichangia kupoteza muda.

Jambo hilo limekuja kurekebishwa kwenye uchaguzi mkuu unao endelea sasa.

Na mpaka sasa walau imeonekana kuna time management yakuridhisha ukizingatia idadi ya wajumbe kuwa mara 3 ya wajumbe wa mabaraza.
 
Katibu mkuu mimi sikumwelewa, hivi hawakuwa na vijitabu vya hotuba wakangawiwa watu badala ya kutumia muda mrefu?
Uko wapi u Smart wa Chandema
Je kila mwanachama angepata hivyo vijitabu? Au wajumbe tu ndio wangepata?

Ripoti ya utekelezaji haiwahusu tu wajumbe waliohudhuria bali pia wanachama wote nchi nzima kwahiyo ilikuwa sahihi.

Fidel Castro aliwahi kutoa speech ya masaa 4 na dakika 29 UN. Kwani walishindwa kumuambia awagawie transcripts wasome ili waokoe muda?
 
Weka makadirio yako ulipenda kuona unachukua muda gani?
 
Lakini pia kuna namna huu mkutano unafuatiliwa na watu wengi sana kutoka nje ya nchi hususan Diaspora ambao ni muhimili mkubwa wa Chama.

Nadhani Chama kilipanga ratiba ambayo itakuwa ni rafiki kwa watu wa nje kuweza kufatilia kinacho jiri.
 
Wanajifunza pia kwa zama hizi za kidigitali tuseme katibu ni mzembe
Kwani kabla ya zoezi muhimu kama hili, huwa hawafanyi vikao vya maandalizi? Maana kuna mambo ukiyatazama, hadi mwenyewe unashikwa hasira.

Kuna watu wanaweza kuona zoezi linavyoenda, wakaishia tu kusonya na kusema hao bado wachanga, hawawezi kitu.

Idadi ya wajumbe wasiofika 1000, zoezi lote lilitakiwa liwe limekamilika ndani ya saa 2 au 3 tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…