Pre GE2025 Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Pre GE2025 Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ni Mbowe au Lissu

  • Mbowe

    Votes: 179 14.7%
  • Lissu

    Votes: 1,038 85.3%

  • Total voters
    1,217
  • Poll closed .
Kuna kitu kinaitwa executive summary!! Mambo ya msingi yote unayaongea kwa majumuisho sio unasoma neno kwa neno.
Pengine hayo yanafanywa kwenye mikutano midogo na sio kwenye huu mkutano mkuu.
 
Kwani kabla ya zoezi muhimu kama hili, huwa hawafanyi vikao vya maandalizi? Maana kuna mambo ukiyatazama, hadi mwenyewe unashikwa hasira.

Kuna watu wanaweza kuona zoezi linavyoenda, wakaishia tu kusonya na kusema hao bado wachanga, hawawezi kitu.

Idadi ya wajumbe wasiofika 1000, zoezi lote lilitakiwa liwe limekamilika ndani ya saa 2 au 3 tu!
Bado niwachanga, (better to name them as figureheads), yaani mtu unamuona ana wadhifa Fulani mtanashati na amenona lakini gorofani hakuna kitu
 
Wekeni matokeo hapa
Tumesema matokeo muda bado ndio kwanza upigaji kura ndio umeanza.

Au unataka matokeo haya?
Screenshot_20250122-030154.png
 
Kama wako serious kweli kushika hatamu ya uongozi, lazima wabadilike. Kama mwendo ndio huu, wasahau kabisa habari za kuwa mbadala wa chama tawala.
They have a long way to go, of recent I suggest they are running a pressure group not a political party

Tuseme ni kundi la kushinikiza jambo fulani
 
Unabadilika, mbona lowassa hakusoma ilani akasema ipo mtandaoni! Kuna muda unatakiwa uwe mbunifu.

Hata ripoti ya CAG ina kurasa zaidi ya 300 ila huwa inasomwa tu executive summary.
Na hata kama ulimfuatilia Katibu Mkuu wakati anasoma hiyo hotuba kuna sehemu nyingi aliziruka akidai hizo tayari zishawahi kutolewa ufafanuzi.

Maana yake amefanya briefing ile ile ambayo wewe umei-recommend.
 
Back
Top Bottom