Yanayojiri Uchaguzi Mkuu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 2023: Felix Tshisekedi atangazwa Mshindi wa Urais

Baba yake Moise Katumbi ni Myahudi!!!
Mayahudi wabaguzi sana. Mbona hua wanakimbia wake na watoto ikibidi kurudi kwao. Wanaoa waafrika kupata maslahi tu. Wakifanikiwa au kufeli wanakitoa wanaacha familia. Nawajua machotara fulani baba myahufi aliwakimbia zamani tu.
 
Africa uchaguzi wa kweli huwa unafanyika nchi ya Ghana tu.huku kwingine ni mwendo wa isidingo
Na Afrika ya Kusini, wamekuwa wakijitahidi sana kuweka mazingira ya uwazi na kuaminiana kwenye michakato yao ya uchaguzi. Kura zimekuwa zikipigwa na kuhesabiwa ktk mazingira ya uwazi kabisa, wakati mwingine hata Waandishi wa Habari wakiwa wanarekodi matukio yote mubashara kwenye vituo vya kupigia Kura. Hali hii kwa kiasi kikubwa imesaidia kuondoa hofu ya kuwepo kwa vitendo vya udanganyifu kwenye uchaguzi na kujenga hali ya watu kuaminiana pamoja na hali ya watu kukubali matokeo ya kura hata kama matokeo husika yameenda kinyume na matarajio yao.
 
Yale matokeo yaliyoletwa humu JF na Chakaza
actually alikusudia kuchakaza wenye mioyo fyatu na halafu wakajaa vizuri sana kwenye 18 zake dah!!

Ofcoz licha ya changamoto nyingi za hapa napale, uchaguzi wa DRC umekwenda vizuri labda zaidi ya chaguzi zilizoopita...

Tuvute subra,
tuwaombee Amani wakati matokeo yakiendelea kutangazwa pole pole...
 
Wakongo Demokrasia yao bado ni changa sana baada ya Nchi yao kuharibiwa na Autocratic rule ya Mobutu na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Lakini nawatakia kila kheri wapate kiongozi ambaye hataendekeza endless wars.

Kiongozi ambaye hata maji yakikatika Kinshasa hata walaumu majirani zake waliomo ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki.
 
Mungu ni Mwema, awavushe vyema bana ba Congo katika yote..
Aimen..
 
Mimi Huwa nashauri kwamba namna nzuri ya kupiga kura ni kwa njia ya kielektroniki Yani wapiga kura wasajiliwe kwa alama za vidole na watapiga kura kwa kutumia vidole kwa kugusa kifaa maalumu Cha kielektroniki ambapo mfumo utamruhusu kila mtu kupiga kura mwenyewe na mara Moja tu kwa mgombea wa nafasi Fulani. Hii njia haita ruhusu mtu kumpigia mtu mwingine kama ilivyo kwa njia ya makaratasi lakini pia idadi ya wapiga kura watakao jisajili kupiga kura haitaongezeka labda kupungua endapo baadhi ya wapiga kura waliojisajiri watashindwa kufika wakati wa uchaguzi.

Hii njia pia inaweza kuwa nzuri kwasababu kifaa chenyewe kitakuwa kinahesabu kura automatically kwa kila mgombea na muda wa upigaji kura utakapofika mwisho tayari idadi ya kura za ndio kwa kila mgombea zitakuwa zinajulikana.

Mpiga kura atagusa picha au Jina la mgombea Fulani kwa nafasi husika mara Moja tu na kura itahesabika na huyo mpiga kura hatoruhusiwa Tena na mfumo kuludia kupiga kura kwa nafasi Ile Ile ambayo amekwisha kuipigia kura.

Hii njia inaweza kupunguza ujinga kwa karibu 98% hivyo uchaguzi utakuwa wa haki.
 
Vp kwa wasiokuwa na mikono.
 
Imemkata huyo baada ya kuangukia pua.

Ni kawaida ya Wapinzani kulalamika baada ya kuangukia pua 🤪🤪
 
Hello familia ya JF.
Heri na Baraka za krismass.

Mwenye kufuatilia uchaguzi muhimu wa kidemokrasia kwa majirani zetu muhimu sana DRC, tafadhali atujaalie matokeo yanaendaje?

Na vip hali ya utulivu na amani ya bana ba Congo...

Tunawatakia subra, ustahimilivu na moyo wa kujizuia wakati matokeo ya mwisho yatakapo tangazwa.
 

Attachments

  • IMG_20231226_171452.jpg
    234.3 KB · Views: 2
Upo sahihi kwenye uwazi ila electric systems zinaweza kudukuliwa.
 
Angalau katiba inaweza kuwa jambo muhimu ambapo kila raia atakuwa chini ya katiba. Lakini kuhusu tume huru Bado haiwezi kuwa mchango mkubwa kwa nchi zetu kwasababu unaweza kujiuliza kwamba hiyo tume itaundwaje, na ikishaundwa itatimiza mamlaka yake Ikiwa ndani ya nchi au nje ya nchi? Watakaounda tume huru watatokana na vyanzo gani? Haya ndo maswali yanayonipa kichwa kuuma kuhusu tume huru.
 
Upo sahihi kwenye uwazi ila electric systems zinaweza kudukuliwa.
Ni kweli lakini inaweza kuwa sio rahisi kwasababu huo mfumo utakuwa unahesabu kura na kurekodi Moja kwa Moja na Hadi muda wa kupiga kura ukifika mwisho kila taarifa itakuwa inajulikana na endapo kutakuwa na mazingira ya ujinga ni rahisi kugundulika kuliko kwa kutumia makaratasi. Tuna watalamu wengi Sana nchini na duniani wenye uwezo wa kulinda taarifa za kielektroniki.
 
Historia? Ipi hiyo? Hivi ni Nji kama Kenya kila kukicha vinajimwambafy kumbe hamna kitu. Kwani DRC wana uzoefu gani wa Katiba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…