njumu za kosovo
JF-Expert Member
- Mar 9, 2017
- 3,820
- 9,625
Haya tumuone huko kigali na kitambi chake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mayahudi wabaguzi sana. Mbona hua wanakimbia wake na watoto ikibidi kurudi kwao. Wanaoa waafrika kupata maslahi tu. Wakifanikiwa au kufeli wanakitoa wanaacha familia. Nawajua machotara fulani baba myahufi aliwakimbia zamani tu.Baba yake Moise Katumbi ni Myahudi!!!
Na Afrika ya Kusini, wamekuwa wakijitahidi sana kuweka mazingira ya uwazi na kuaminiana kwenye michakato yao ya uchaguzi. Kura zimekuwa zikipigwa na kuhesabiwa ktk mazingira ya uwazi kabisa, wakati mwingine hata Waandishi wa Habari wakiwa wanarekodi matukio yote mubashara kwenye vituo vya kupigia Kura. Hali hii kwa kiasi kikubwa imesaidia kuondoa hofu ya kuwepo kwa vitendo vya udanganyifu kwenye uchaguzi na kujenga hali ya watu kuaminiana pamoja na hali ya watu kukubali matokeo ya kura hata kama matokeo husika yameenda kinyume na matarajio yao.Africa uchaguzi wa kweli huwa unafanyika nchi ya Ghana tu.huku kwingine ni mwendo wa isidingo
actually alikusudia kuchakaza wenye mioyo fyatu na halafu wakajaa vizuri sana kwenye 18 zake dah!!Yale matokeo yaliyoletwa humu JF na Chakaza
Wakongo Demokrasia yao bado ni changa sana baada ya Nchi yao kuharibiwa na Autocratic rule ya Mobutu na vita vya wenyewe kwa wenyewe.actually alikusudia kuchakaza wenye mioyo fyatu na halafu wakajaa vizuri sana kwenye 18 zake dah!!
Ofcoz licha ya changamoto nyingi za hapa napale, uchaguzi wa DRC umekwenda vizuri labda zaidi ya chaguzi zilizoopita...
Tuvute subra,
tuwaombee Amani wakati matokeo yakiendelea kutangazwa pole pole...
Mungu ni Mwema, awavushe vyema bana ba Congo katika yote..Wakongo Demokrasia yao bado ni changa sana baada ya Nchi yao kuharibiwa na Autocratic rule ya Mobutu na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Lakini nawatakia kila kheri wapate kiongozi ambaye hataendekeza endless wars.
Kiongozi ambaye hata maji yakikatika Kinshasa hata walaumu majirani zake waliomo ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki.
Vp kwa wasiokuwa na mikono.Mimi Huwa nashauri kwamba namna nzuri ya kupiga kura ni kwa njia ya kielektroniki Yani wapiga kura wasajiliwe kwa alama za vidole na watapiga kura kwa kutumia vidole kwa kugusa kifaa maalumu Cha kielektroniki ambapo mfumo utamruhusu kila mtu kupiga kura mwenyewe na mara Moja tu kwa mgombea wa nafasi Fulani. Hii njia haita ruhusu mtu kumpigia mtu mwingine kama ilivyo kwa njia ya makaratasi lakini pia idadi ya wapiga kura watakao jisajili kupiga kura haitaongezeka labda kupungua endapo baadhi ya wapiga kura waliojisajiri watashindwa kufika wakati wa uchaguzi.
Hii njia pia inaweza kuwa nzuri kwasababu kifaa chenyewe kitakuwa kinahesabu kura automatically kwa kila mgombea na muda wa upigaji kura utakapofika mwisho tayari idadi ya kura za ndio kwa kila mgombea zitakuwa zinajulikana.
Mpiga kura atagusa picha au Jina la mgombea Fulani kwa nafasi husika mara Moja tu na kura itahesabika na huyo mpiga kura hatoruhusiwa Tena na mfumo kuludia kupiga kura kwa nafasi Ile Ile ambayo amekwisha kuipigia kura.
Hii njia inaweza kupunguza ujinga kwa karibu 98% hivyo uchaguzi utakuwa wa haki.
Idadi ya wasiokuwa na mikono itajulikana na unaweza kuandaliwa utaratibu maalumu kwa ajili YaoVp kwa wasiokuwa na mikono.
Imemkata huyo baada ya kuangukia pua.View attachment 2849698Wapinzani watano, ikiwa ni pamoja na aliyekuwa Gavana wa Mkoa Moise Katumbi, walisema Jumamosi kwamba kura hiyo haipaswi kuthibitishwa kwani ilikuwa imeharibiwa na "udanganyifu mkubwa."
MOISE KATUMBI ATAKA UCHAGUZI UFUTWE. VIONGOZI WA UPINZANI WAPANGA KUFANYA MAANDAMANO
Viongozi wengine watano wa upinzani, ikiwa ni pamoja na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Denis Mukwege na aliyekuwa mtendaji wa mafuta Martin Fayulu, wametoa wito wa maandamano dhidi ya matokeo Jumatano ijayo.
"Tutapinga dhidi ya irregula zilizobainika wakati wa shughuli za kupiga kura," walisema katika barua kwa gavana wa Kinshasa, ambapo wanapanga kukusanyika.
MATOKEO YA AWALI YAANZA KUTANGAZWA
Matokeo ya awali ya kura ya urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yalianza kuingia taratibu siku ya Ijumaa baada ya uchaguzi uliogubikwa na misukosuko kwenye baadhi ya maeneo nchini humo ambapo mamlaka zilitangaza kuwa uchaguzi huo umemalizika vizuri
Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ceni, ilitangaza matokeo kwa wapiga kura wa Kongo wanaoishi Afrika Kusini, Ubelgiji, Ufaransa, Canada, na Marekani.
Matokeo haya yanawakilisha sehemu ndogo sana ya kura zote zilizopigwa, lakini yalionyesha Felix Tshisekedi, anawania kuongoza kwa muhula wa pili anaongoza kwenye matokeo hayo.
Ucheleweshwaji mkubwa na urasimu ilisababisha baadhi ya vituo kuchelewa kufunguliwa huku vingine kutofunguliwa kabisa, ambapo Ceni iliongeza muda wa kupiga kura kwenye baadhi ya maeno mpaka Alhamisi
Tume ya uchaguzi ilitoa taarifa kuwa hakuna kituo cha kupigia kura kilichoruhusiwa kufunguliwa siku ya Ijumaa.
Kucheleweshwa kwa kiasi kikubwa na machafuko ya utaratibu yaliharibu uchaguzi na baadhi ya vituo vya kupigia kura vilishindwa kufunguliwa kabisa.
Ceni iliongeza muda wa kupiga kura katika baadhi ya maeneo hadi Alhamisi.
Kupitia taarifa, tume ya uchaguzi ilisema hakuna kituo cha kupigia kura kilichoruhusiwa kufunguliwa siku ya Ijumaa.
Hata hivyo, kwa mujibu wa maafisa, upigaji kura uliendelea kwenye maeneo ambayo hasa yako mbali na mji siku ya Ijumaa
Mfano wananchi wa Kilembwe, katika eneo la Fizi jimbo la South Kivu, mashariki mwa nchi hiyo, walipiga kura kwa kuchelewa sana baada ya vifaa kuwasili kuchelewa siku ya Alhamisi.
Ceni inatarajiwa kuanza kutangaza matokeo ya awali kwenye majimbo 26 ya DRC leo Jumamosi 23/12/2023
22/12/2023 - MATOKEO YA UCHAGUZI KUTANGAZWA HATUA KWA HATUATume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo - CENI imesema itaanza kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano, hatua kwa hatua.
Tangazuo hilo linatolewa licha ya malalamiko makubwa kutoka wagombea wa upinzani, na wadau wengine waliochunguza mwenendo wa uchaguzi huo, ambao wanasema umekuwa na hitilafu chungu nzima.
Mmoja wa maafisa wakuu wa CENI Didi Manara amesema matokeo ya awali yataanza kuchapishwa leo Ijumaa. Huku matokeo rasmi yakitarajiwa kutangazwa mapema na Mahakama ya Kikatiba mapema Januari 2024.
21/12/2023 MABOXI YALIYOKWISHAPIGIWA KURA WAKATI ZOEZI LA KUPIGA KURA LIKIENDELEA YAKAMATWA
View attachment 2849752
View attachment 2849755
View attachment 2849759
View attachment 2849770
Mjini Mbujimayi, karatasi ya matokeo iliyoonyeshwa katika Kituo cha Kupigia Kura 8011051-C inaonyesha wapiga kura 742, wote wakimuunga mkono mgombea Félix Tshisekedi, kati ya wapiga kura 704 waliojipanga kwenye orodha. Kiwango cha ushiriki kinaonyesha 105.40%
20/12/2023 - WAGOMBE WA UPINZANI KONGO WALALAMIKIA DOSARI ZA UCHAGUZI
Wagombea wakuu wa upinzani katika uchaguzi wa rais unaofanyika leo nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamesema raia wengi wameshuhudia mparaganyiko na dosari nyingi vituoni walipokwenda kupiga kura.
Akizungumza baada ya kupiga kura mjini, Kinshasa, mwanasiasa wa upinzani Martin Fayulu amelalamika dhidi ya kile alichokieleza kuwa ni kukosekana "utaratibu mzuri" vituoni na kuutuhumu upande wa chama tawala kula njama za kuiba kura.
"Hivi sasa (kambi ya rais) imejiandaa kufanya udanganyifu. Nimewaambia watu wa Kongo, hakuna uchakachuaji safari hii, na kama mtu atajaribu kupora ushindi wetu, ibara ya 64 ya katiba ipo, na tutateremka mitaani kudai ushindi wa umma," alisema Fayulu.
Madai ya dosari vituoni yametolewa pia na wagombea wengine ikiwemo Denis Mukwege na mwanasiasa kigogo Moise Katumbi anayetazamiwa kutoa upinzani mkali kwa Rais Felix Tshisekedi anayewania muhula wa pili.
Zaidi ya wapiga kura milioni 44 wamesajiliwa kushiriki zoezi hilo la kidemokrasia la kumchagua rais, bunge la taifa, mabunge ya mikoa na madiwani.
========
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) imelazimika kuongeza muda zaidi wa kupiga Kura baada ya Malalamiko mengi kuonesha kulikuwa na ucheleweshaji katika zoezi la kufungua Vituo vya Kupigia Kura katika maeneo mengi.
Hali hiyo imedaiwa kuanza kuibua hisia za Vurugu kwa baadhi ya Wananchi huku Wagombea wa Upinzani wakidai ni njama za Chama Tawala kutaka kushinda Uchaguzi kwa mbinu za wizi wa Matokeo au kuvuruga uwazi katika zoezi hilo.
Takriban Watu Milioni 44 wanatarajiwa kupiga Kura katika Uchaguzi huo ingawa takwimu zinaonesha idadi kubwa ya Watu katika baadhi ya maeneo imeyakimbia Makazi yao kutokana na Mapigano ambayo yalisababisha Watu Milioni 1.5 kushidnwa Kujiandikisha.
AL Jazeera
===============
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inatarajia kufanya Uchaguzi wa Mkuu hapo Desemba 20, huku Rais Félix Tshisekedi akitafuta nafasi ya kuongoza kwa muhula wa pili, na wa mwisho, wa miaka 5 madarakani
Takriban Watu Milioni 40 kati ya Raia zaidi ya Milioni 102 wanatarajiwa kupiga Kura kutoka Taifa hilo kubwa zaidi katika eneo la Jangwa la Sahara lenye utajiri wa Madini yenye Thamani Kubwa
KWANINI UCHAGUZI HUU NI MUHIMU?
DRC ndio makazi ya 70% ya Madini ya Coltan yanayotumiwa katika uundaji wa Simu za Mkononi, 30% ya Almasi inayouzwa duniani kote na madini mengine mengi
Licha ya Utajiri huo mkubwa wa Maliasili, Congo inatajwa kuwa kati ya Nchi zilizoshindwa kutumia rasilimali zake katika kuboresha Maisha ya Wananchi. Sababu kuu ni Machafuko ya Kivita, Rushwa pamoja na Utawala Unaoyumba kila wakati
Inakadiriwa kuwa tangu mwaka 2008, takriban watu Milioni 5.4 wamepoteza maisha kutokana na Mapigano, Njaa na Magonjwa ya Mripuko. Hata hivyo, idadi hiyo inaweza kuwa chini au zaidi
NANI WANAGOMBEA URAIS?
Hadi sasa Wagombea waliobaki ni 20 huku 6 wakijiondoa akiwemo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Augustin Matata Ponyo
WANAOTAJWA KUWA NA USHAWISHI ZAIDI
Mbali na Rais Felix mwenyewe, wagombea wengine wenye nguvu zaidi ni:
1. Martin Fayulu ambaye alitajwa kuwa mshindi wa Urais katika Uchaguzi wa mwaka 2018, ingawa alitajwa kuwa wa pili katika Matokeo, anapewa nafasi zaidi katika Uchaguzi huo
2. Anayefuatia ni Moïse Katumbi, Mfanyabiashara na Gavana wa zamani wa Jimbo la Katanga na Mmiliki wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya TP Mazembe
3. Mwingine ni Dkt. Denis Mukwege, Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka 2018 kutokana na Kazi za kutetea haki za Waathirika wa Vitendo vya Ubakaji
Wagombea 4 kati ya 6 waliojiondoa, wameonesha kumuunga mkono Mfanyabiashara Katumbi. Wengine wawili wanamuunga mkono Rais Felix
GHARAMA ZA UCHAGUZI
Wagombea wote walilazimika kulipa faranga za Kongo Milioni 160 (Takriban Tsh. Milioni 151,112,340) ili kulipia ada ya Fomu ya maombi. Kumbuka pesa hii hairejeshwi hata ikitokea umejiondoa au umekatwa na Wajumbe
UTARATIBU WA UCHAGUZI
Mgombea yeyote atakayepata idadi kubwa ya Kura kuzidi wengine, atakuwa Mshindi wa Urais hata kama asipofika 50% ya Kura.
Hakutakuwa na Uchaguzi wa Marudio
Uchaguzi unafanyika Siku 90 kabla ya muda wa Rais aliyeko madarakani kumalizika. Uchaguzi wa mwaka huu unajumuisha Wabunge, Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa
MASUALA GANI YANATAJWA KWENYE KAMPENI?
Congo inafanya Uchaguzi wakati Hali ya Uchumi ikitajwa kuzidi kuzorota, Sarafu yake imeporomoka kwa 15% hadi 20% dhidi ya Dola ya Marekani
Zaidi ya 65% ya Wananchi wanaishi katika mazingira ya Umasikini kipato chao kikiwa chini ya Dola 2.5 au chini
MATOKEO YATATANGAZWA LINI?
Kalenda ya Tume ya Uchaguzi inaonesha Matokeo yote yatakuwa hadharani kufikia Desemba 31, 2023.
Kama kila kitu kitaenda kama ilivyopangwa, Rais Mteule ataapishwa rasmi Januari 20, 2024
Upo sahihi kwenye uwazi ila electric systems zinaweza kudukuliwa.Mimi Huwa nashauri kwamba namna nzuri ya kupiga kura ni kwa njia ya kielektroniki Yani wapiga kura wasajiliwe kwa alama za vidole na watapiga kura kwa kutumia vidole kwa kugusa kifaa maalumu Cha kielektroniki ambapo mfumo utamruhusu kila mtu kupiga kura mwenyewe na mara Moja tu kwa mgombea wa nafasi Fulani. Hii njia haita ruhusu mtu kumpigia mtu mwingine kama ilivyo kwa njia ya makaratasi lakini pia idadi ya wapiga kura watakao jisajili kupiga kura haitaongezeka labda kupungua endapo baadhi ya wapiga kura waliojisajiri watashindwa kufika wakati wa uchaguzi.
Hii njia pia inaweza kuwa nzuri kwasababu kifaa chenyewe kitakuwa kinahesabu kura automatically kwa kila mgombea na muda wa upigaji kura utakapofika mwisho tayari idadi ya kura za ndio kwa kila mgombea zitakuwa zinajulikana.
Mpiga kura atagusa picha au Jina la mgombea Fulani kwa nafasi husika mara Moja tu na kura itahesabika na huyo mpiga kura hatoruhusiwa Tena na mfumo kuludia kupiga kura kwa nafasi Ile Ile ambayo amekwisha kuipigia kura.
Hii njia inaweza kupunguza ujinga kwa karibu 98% hivyo uchaguzi utakuwa wa haki.
Angalau katiba inaweza kuwa jambo muhimu ambapo kila raia atakuwa chini ya katiba. Lakini kuhusu tume huru Bado haiwezi kuwa mchango mkubwa kwa nchi zetu kwasababu unaweza kujiuliza kwamba hiyo tume itaundwaje, na ikishaundwa itatimiza mamlaka yake Ikiwa ndani ya nchi au nje ya nchi? Watakaounda tume huru watatokana na vyanzo gani? Haya ndo maswali yanayonipa kichwa kuuma kuhusu tume huru.Mbona walifanya hivyo kwa Edward Lowasa tena Lowasa alikuwa na nguvu nyingi sana wakati ule
Miye nafikiri kwanza tatizo ni katiba, tume huru na elimu ya urai kwa wananchi wetu uelewa wa wengi bado mdogo sana Kwenye mambo haya ya uchaguzi na demokrasia ya kweli
Ni kweli lakini inaweza kuwa sio rahisi kwasababu huo mfumo utakuwa unahesabu kura na kurekodi Moja kwa Moja na Hadi muda wa kupiga kura ukifika mwisho kila taarifa itakuwa inajulikana na endapo kutakuwa na mazingira ya ujinga ni rahisi kugundulika kuliko kwa kutumia makaratasi. Tuna watalamu wengi Sana nchini na duniani wenye uwezo wa kulinda taarifa za kielektroniki.Upo sahihi kwenye uwazi ila electric systems zinaweza kudukuliwa.
Historia? Ipi hiyo? Hivi ni Nji kama Kenya kila kukicha vinajimwambafy kumbe hamna kitu. Kwani DRC wana uzoefu gani wa Katiba!Hello familia ya JF.
Heri na Baraka za krismass.
Mwenye kufuatilia uchaguzi muhimu wa kidemokrasia kwa majirani zetu muhimu sana DRC, tafadhali atujaalie matokeo yanaendaje?
Na vip hali ya utulivu na amani ya bana ba Congo...
Tunawatakia subra, ustahimilivu na moyo wa kujizuia wakati matokeo ya mwisho yatakapo tangazwa.
Africa bara la kishenzi sana.....Historia? Ipi hiyo? Hivi ni Nji kama Kenya kila kukicha vinajimwambafy kumbe hamna kitu. Kwani DRC wana uzoefu gani wa Katiba!