Wakuu,
Kwa niaba ya JF, nitahakikisha mnafahamu kinachojiri toka hapa Kenya ambapo uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika hapo kesho.
Tayari Raila Odinga ametangaza kuwa Muungano wa NASA utakuwa “National Resistance Movement” na kuwataka wakenya kutoshiriki uchaguzi huu ambao amesisitiza ni batili.
Kwa kuanzia, hali ya usalama imeimarishwa kila kona:
========
Oktoba 26, 2017
08:00am
> Vituo vingi vina wapiga kura wachache sana! Hadi muda huu dalili si nzuri kama wananchi watajitokeza kwa wingi
14:00
Mtu mmoja ameuawa huko Kisumu na wengine 8 kujeruhiwa baada ya polisi kukabiliana na wafuasi wa upinzani waliotaka kuvuruga uchaguzi.
Marehemu alikuwa ni kijana mwenye umri wa miaka 19 na alifariki baada ya kupigwa risasi ya paja na kuvuja damu nyingi[/QUOT
Tuwaombee wakenya