Wakuu,
Kwa niaba ya JF, nitahakikisha mnafahamu kinachojiri toka hapa Kenya ambapo uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika hapo kesho.
Tayari Raila Odinga ametangaza kuwa Muungano wa NASA utakuwa “National Resistance Movement” na kuwataka wakenya kutoshiriki uchaguzi huu ambao amesisitiza ni batili.
Kwa kuanzia, hali ya usalama imeimarishwa kila kona:
========
Oktoba 26, 2017
08:00am
> Vituo vingi vina wapiga kura wachache sana! Hadi muda huu dalili si nzuri kama wananchi watajitokeza kwa wingi
14:00
Mtu mmoja ameuawa huko Kisumu na wengine 8 kujeruhiwa baada ya polisi kukabiliana na wafuasi wa upinzani waliotaka kuvuruga uchaguzi.
Marehemu alikuwa ni kijana mwenye umri wa miaka 19 na alifariki baada ya kupigwa risasi ya paja na kuvuja damu nyingi
View attachment 617579
==========================================
16:30
IEBC yaahirisha uchaguzi Kaunti za Kisumu, Migori, Homa Bay na Siaya mpaka Jumamosi. Kaunti hizo ni ngome ya upinzani.
Hii ni kutokana na hali ya mshike mshike kati ya Polisi na Wapiga kura asubuhi ya leo
> Kisumu, mtu mmoja ameripotiwa kufa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya wafuasi wa upinzani kupigana na Polisi
> Migori, mtu mmoja amepigwa risasi na kujeruhiwa baada ya watu waliokuwa wakijaribu kuzuia vituo vya kupigia kura kupambana na Polisi. Mtu huyo alipelekwa hospitali ya Migori kwa matibabu
>Homa Bay, kulikuwa hakuna matukio mengi zaidi ya vijana wakijaribu kuzuia watu kupiga kura na viongozi wa IEBC kushindwa kutokea kwenye vituo vya kupigia kura
>Siaya wasiamamizi wavituo vya kupiga kura hawakutokea kabia
17:00
Kura zimeanza kuhesabiwa sehemu ambazo hakuna utata