LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Haya kazi indeleee
 
Unamaanisha HAMAS walitegeshewa na wakajaa wenyewe kwa 18 z. Mdogo wake Yoni anaenda kuwafunza adabu hawatokaa warudie tena
 
Ndg yangu kuna kauli inasema usimwamini mwanasiasa, akikwambia nje kuna mvua, usikae kama zoba toka nje ukahakikishe ni kweli!.

Nyamizi 👇🏾
Alichokifanya PM-N ni jambo baya sana kwa raia wa Israel.

kwanza alipewa taarifa za ambush na Cairo state jamaa akavunga, pentagon wakamwambia umeingiliwa mzee akavunga akijua ngoja awaonyeshe why Benjamin still 😄!.

So Mosad walijua ila tusiojua deeper na wale wengine kule mashariki ya kati wanajua Israel imedoda kumbe huyu mzee alitaka kufika hapa, kisiasa na kimkakati kwa Israel.
 
Una uhakika na hili?


Wewe je una uhakika mababu zako wametoka kwenye nchi uliyopo sasa na unayoitambua kama nyumbani?...

.je ukifukuzwa uambiwe ufuate chimbuko lao urudi huko, upo tayari kwa hilo?
Pale si Israel wala Palestina anayetakiwa kuondoka. Wote pale ni kwao kabisa pasipo na shaka.
Wapelestina hawakuwahi kufukuzwa pale. Miaka yote Wapalestina na Wayahudi wamekuwa pamoja kwenye ardhi ile pamoja na kuwa na tofauti zao.
Kulikua na Wapalestina Wakristo, wapagani pia wengi tu walioabudu katika Uyahudi, hata ulipokuja Uislam na wapalestina wakaamua kuupokea uislam, bado maisha yalikua ya kawaida. Tofauti na mikwaruzano miongoni mwao haikuwahi kuisha ila maisha yaliendelea.
Pressure kubwa iliyoleta chuki haikuwa sababu ya wapalestina kuwa waislam, bali walioupeleka Uislam pale, hao ndiyo walipelekea pressure ya kujenga chuki kwa wasioamini mpaka hapo watakapoamini kama wao.

(Tatizo kubwa halipo kwenye hizi dini au mafundisho yake, maana mafundisho ukiona haya tafsiri au nia nzuri au hayajengi, kama Mwanadamu unakuwa na akili na utashi wa kutambua Jema na baya na hivyo kufanya maamuzi sahihi. Tatizo kubwa la hizi dini (zote) ni wahubiri wake, hao ndiyo hupelekea madhara makubwa yanayoonekana kusababishwa au kuletwa na dini).

Waliokua wakiineza dini ndiyo walisababisha shida ma kujenga chuki dhidi ya wengine. Muda ulivyozidi kusonga na uislam kuzidi kujitanua, hali ilizidi kuwa tete, ingawa kwa Wapalestina, nguvu ya ya tofauti na mikwaruzano yao na Wayahudi haikuwa sababu ya utofauti wa dini zao, bali za asili na tamaduni zao ambazo walikuwa nazo hata kabla ya uislam kuja (Ikumbukwe, hata maisha ya Wakristo hayakuwa mepesi mbele ya Wayahudi, Wakristo waliwa treat vizuri sana Wayahudi, wakawakaribisha Ulaya, wakawapa fursa, lakini that has never been the same kwa namna Wayah7di wamekua wakiuchukulia Ukristo).

Kubwa kuliko yote ni wakati imeamuliwa Two State Solution, Israel hakuwa na shida pia wazo hilo lilitoka kwao, Wapaletina nao hawakuonekana kuwa na shida ila nchi za kiarabu ndiyo zilikua na shida, zililipinga hili kwa nguvu zote.

Hali hii ilipelekea Umoja wa Mataifa kuchelewesha Uhuru wa nchi hizo ambao ulikua utolewe tangu mwaka 1947, ndipo Israel wakaona ni upuuzi kuendelea kucheleweshwa kwa pressure za mataifa mengine. Tarehe 14 May, 1948, wakaamua kusimama na kujitangazia Uhuru wakijiita Israel, dunia ikiwa haijaipatapata vizuri hiyo taarifa ili angalau iamue kama waipokee kwa kulia, kushangilia, au namna gani? Ila wakati Israel wakiwa wanasherehekea Uhuru wao, ghafla mataifa matano ya kiarabu (Misri, Iraq, Jordan, Lebanon, na Syria) yakaivamia Israel. Vita ikapiganwa kwa miezi 9, wiki 3 na siku 2.

Vita hiyo ilipelekea nchi ile igawanyike katika sehemu tatu. Taifa la Israel, Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan (West Bank) na Ukanda wa Gaza.

Israel ikitawala eneo la Israel ambalo ndiyo maeneo waliyokua wakiishi, huku Wapelestina wakibaki na maemeo waliyokua wakiishi ya Gaza na Westbank, huku wapalestina wengine wapatao 750,000 wakiondolewa kutoka Israel kupelekwa Gaza na West bank.

Mwaka 1967, mataifa matatu ya kiarabu Misri, Jordan na Syria yakastukiza na kuivamia tena Israel na kupelekea ile vita maarufu ya vita vya siku 6. Katika vita hivi, Israel ikawashinda waarabu, ikaenda mbele zaidi kwa kuikamata Sinai Peninsula yote, Ukanda wa Gaza, West Bank, Jerusalem Mashariki, na Vilima vya Golan (Golan Heights).
Baada ya vita hivyo kelele ziliendelea kuwa nyingi kutoka nchi za kiarabu kuliko Palestina. Hata UN ilipoleta mkataba wa amani wao wakaendelea kuja na madai mapya.

Vita zilizofuata zilikua ni kujaribu kurudisha maeneo yaliyotekwa na Israel, ambapo haikufanikiwa ila kwa yaliyorudishwa yalirudishwa kwa njia ya mazungumzo ya amani.

Kwa kifupi, Israel haijawahi kuwa against two state solution, ila Iran ambao wanaya backup makundi ya kipalestina hawapo tayari kwa hilo.

Wapalestina wenyewe wameshagawanyika tangu ule Mkataba wa Oslo.
Tangu uchaguzi wa mwisho wa Wapalestina uliopelekea HAMAS kushinda kule Gaza, walifutilia mbali habari za uchaguzi na tangu hapo wapo kinyume na utawala wa wapalestina, Gaza ni kama imeamua kujitenga na West Bank na inajiendesha yenyewe kuvyake wakipigana kuvyao.

Ngoja niishie hapa, maana nimeandika hadi ambavyo hukutaka kuvijua wala sidhani kama upo interested.
 
Unamaanisha HAMAS walitegeshewa na wakajaa wenyewe kwa 18 z. Mdogo wake Yoni anaenda kuwafunza adabu hawatokaa warudie tenah
Hawa wafilisti hawana lolote, Enzi za kale Samson alipenda kukata boder na kuchukua mademu kule maana kama mnavyojua watoto wa kiaarabu ni pic kali , kuna siku wakamfungia kwa nje kisha wakazunguka nyumba huku wakitaka atoke laa wanachoma nyumba - jamaa kwa hasira akatoka na mlango kabisa akapanda nao hadi mlimani - akasema kwenye nguvu amfuate.

Alivyorudi kwao Israel alisimulia kisa hicho, kisha akasema atarudi tena, maana mabinti kwa kule ni warembo.

So waislael kwa waarabu ni mabinti tu warembo 😀 😀
 
🤣🤝🤝✌️
 
kwani ni dhambi kuwa mvaa kobas, mbona umeruka kama kuna ktu kimekugusa kule?
We jamaa punguza utoto bhasi, kama huna hoja si bora unyamaze, unachofanya hapa unatudhalilisha wakristo tunaonekana elimu tunayopewa ni ya mchongo, sababu ya upumbavu wako.
 
Huwa tunaikuza sn israel hila bila misaada na mikopo hata mishahara ya wafanyakazi itawashinda sasa km battle na hamas wameomba msaada halafu ndio huwa wanataka kushambulia iran
Mkuu,mfano wa Ukraine, Russia inapambana na USA,hilo liko wazi. Sasa na upande huu, hata hiyo USA, itaijaribu IRAN kupitia Israel, lakini,mvua imenyesha, panapovuja panajulikana. Af mi nachekeshwa na kitu kimoja. Vyombo vya habari vya Marekani na uraya, vikasifia Iron Dome ya Israel. Kila mtu hata asieijua akawaka moto, Dome ikawa Dome. Leo hii ifahamike kwamba USA na washilika wake,tofauti sana na wale wa zamani. Kibaya zaidi,wabongo wanaumizwa vichwa sana na maandishi kuliko uhalisia wa mambo.
 
We jamaa punguza utoto bhasi, kama huna hoja si bora unyamaze, unachofanya hapa unatudhalilisha wakristo tunaonekana elimu tunayopewa ni ya mchongo, sababu ya upumbavu wako.
mm nimetukanwa matusi ya nguoni kisa tu nimesema waisrael wanajibu mashambulizi na wanapigania ardhi yao, nimeambiwa mpaka mimba yangu ilitungwa kwenye madanguro, mm nikijbu kdogo tu naonekana nina utoto, umesoma kashfa na mitusi niliyoporomoshewa mkuu, samahani kama hyo comment imekukwaza mkuu wangu, kila mtu ana kiwango chake cha uvumilivu.
 
Solution ni tatu either waungane wawe nchi moja au wapalestina watawanywe kwenye nchi mbalimbali za kiarabu wakaanze upya maisha.
Yaani nchi ya Palestine isiwepo.
Waarabu waache ubinafsi wawachukue ndugu zao kuliko kuwaacha wauwawe wengi hawana hatia bali ni wahanga tu wa udhalimu.
Au waachwe wauwane atakaemmaliza mwenzio ndio apewe haki.
Wasomali hawakushaurika waliachwa wakauwana hadi wamechoka kuuwana wamepumzika.
Shetani ndie aletae vita ili kupata damu kwenye vita wanauhakika wa kupata lita nyingi sana za damu tofauti na ajali.
 
Pale si Israel wala Palestina anayetakiwa kuondoka. Wote pale ni kwao kabisa pasipo na shaka.
Wapelestina hawakuwahi kufukuzwa pale. Miaka yote Wapalestina na Wayahudi wamekuwa pamoja kwenye ardhi ile pamoja na kuwa na tofauti zao.
Umesema vyema. Zile jamii zote 2 zilikuwepo pale miaka mingi.

Kihalisi hili suala wengi wameliweka kwenye udini ila ishu kubwa ni ardhi.
 
Umesema vyema. Zile jamii zote 2 zilikuwepo pale miaka mingi.

Kihalisi hili suala wengi wameliweka kwenye udini ila ishu kubwa ni ardhi.
Wapelestina wameruhusu kushikiwa maamuzi na waarabu.
Kwa asili Wapelestina ni watu wazuri sana, binafsi nawakubali kati asili yao.
Wakiachwa wenyewe, Israel na Palestina bila waarabu kuingilia wana uwezo mkubwa wa kukubaliana na kuja na suluhu.
Ila akili na maamuzi ya kufundishwa ndiyo yanayowagharimu.
Kuna kila dalili kuwa sasa hivi huenda Wakaipoteza Gaza mazima na hapo ndiyo amani itarudi.
 
Kwa wataalamu wa usalama, ujasusi na masuala ya kijeshi kwa sasa gumzo lililipo imekuwaje shirika la ujasusi la Israeli MOSSAD, limeshindwa kujua hadi adui anaingia ndani ya taifa lao tena hadi kambi za jeshi?

Hata Marekani imehoji sana mfumo wa ujasusi wa Israel.

Kwa hapa Israel kaonyesha udhaifu mkubwa sana.

Pia mfumo wake wa air defense wa Iron Dome umetiliwa shaka ikiwa missiles zs migambo wa HAMAS zimepenya mpaka Tel Aviv vipi adui akishambulia kwa kutumia hypersonic missiles?

Adui wa Israeli kwa sasa hawaangalii kile anachofanya Mwisraeli kupiga magorofa na kuyaangusha pale Gaza

Ila wanajifunza udhaifu wa Israeli
 
Binafsi kama muda utaniruhusu huenda nikaja na andika kuhusiana na hili la MOSSAD, kuna nadharia nyingi ila katika hili ni ngumu kusema MOSSAD hawakujua, aubShin Bet hawakujua.
Ukiangalia jinsi kambi za jeshi zilivyokutwa zipozipo tu bila ulinzi, na HAMAS wakawa wanaingia na kutoka watakavyo, kuna kitu ambacho unaona si cha kawaida, nabaki najiuliza sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…