Una uhakika na hili?
Wewe je una uhakika mababu zako wametoka kwenye nchi uliyopo sasa na unayoitambua kama nyumbani?...
.je ukifukuzwa uambiwe ufuate chimbuko lao urudi huko, upo tayari kwa hilo?
Pale si Israel wala Palestina anayetakiwa kuondoka. Wote pale ni kwao kabisa pasipo na shaka.
Wapelestina hawakuwahi kufukuzwa pale. Miaka yote Wapalestina na Wayahudi wamekuwa pamoja kwenye ardhi ile pamoja na kuwa na tofauti zao.
Kulikua na Wapalestina Wakristo, wapagani pia wengi tu walioabudu katika Uyahudi, hata ulipokuja Uislam na wapalestina wakaamua kuupokea uislam, bado maisha yalikua ya kawaida. Tofauti na mikwaruzano miongoni mwao haikuwahi kuisha ila maisha yaliendelea.
Pressure kubwa iliyoleta chuki haikuwa sababu ya wapalestina kuwa waislam, bali walioupeleka Uislam pale, hao ndiyo walipelekea pressure ya kujenga chuki kwa wasioamini mpaka hapo watakapoamini kama wao.
(Tatizo kubwa halipo kwenye hizi dini au mafundisho yake, maana mafundisho ukiona haya tafsiri au nia nzuri au hayajengi, kama Mwanadamu unakuwa na akili na utashi wa kutambua Jema na baya na hivyo kufanya maamuzi sahihi. Tatizo kubwa la hizi dini (zote) ni wahubiri wake, hao ndiyo hupelekea madhara makubwa yanayoonekana kusababishwa au kuletwa na dini).
Waliokua wakiineza dini ndiyo walisababisha shida ma kujenga chuki dhidi ya wengine. Muda ulivyozidi kusonga na uislam kuzidi kujitanua, hali ilizidi kuwa tete, ingawa kwa Wapalestina, nguvu ya ya tofauti na mikwaruzano yao na Wayahudi haikuwa sababu ya utofauti wa dini zao, bali za asili na tamaduni zao ambazo walikuwa nazo hata kabla ya uislam kuja
(Ikumbukwe, hata maisha ya Wakristo hayakuwa mepesi mbele ya Wayahudi, Wakristo waliwa treat vizuri sana Wayahudi, wakawakaribisha Ulaya, wakawapa fursa, lakini that has never been the same kwa namna Wayah7di wamekua wakiuchukulia Ukristo).
Kubwa kuliko yote ni wakati imeamuliwa Two State Solution, Israel hakuwa na shida pia wazo hilo lilitoka kwao, Wapaletina nao hawakuonekana kuwa na shida ila nchi za kiarabu ndiyo zilikua na shida, zililipinga hili kwa nguvu zote.
Hali hii ilipelekea Umoja wa Mataifa kuchelewesha Uhuru wa nchi hizo ambao ulikua utolewe tangu mwaka 1947, ndipo Israel wakaona ni upuuzi kuendelea kucheleweshwa kwa pressure za mataifa mengine. Tarehe 14 May, 1948, wakaamua kusimama na kujitangazia Uhuru wakijiita Israel, dunia ikiwa haijaipatapata vizuri hiyo taarifa ili angalau iamue kama waipokee kwa kulia, kushangilia, au namna gani? Ila wakati Israel wakiwa wanasherehekea Uhuru wao, ghafla mataifa matano ya kiarabu
(Misri, Iraq, Jordan, Lebanon, na Syria) yakaivamia Israel. Vita ikapiganwa kwa miezi 9, wiki 3 na siku 2.
Vita hiyo ilipelekea nchi ile igawanyike katika sehemu tatu. Taifa la Israel, Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan (West Bank) na Ukanda wa Gaza.
Israel ikitawala eneo la Israel ambalo ndiyo maeneo waliyokua wakiishi, huku Wapelestina wakibaki na maemeo waliyokua wakiishi ya Gaza na Westbank, huku wapalestina wengine wapatao 750,000 wakiondolewa kutoka Israel kupelekwa Gaza na West bank.
Mwaka 1967, mataifa matatu ya kiarabu Misri, Jordan na Syria yakastukiza na kuivamia tena Israel na kupelekea ile vita maarufu ya vita vya siku 6. Katika vita hivi, Israel ikawashinda waarabu, ikaenda mbele zaidi kwa kuikamata Sinai Peninsula yote, Ukanda wa Gaza, West Bank, Jerusalem Mashariki, na Vilima vya Golan (Golan Heights).
Baada ya vita hivyo kelele ziliendelea kuwa nyingi kutoka nchi za kiarabu kuliko Palestina. Hata UN ilipoleta mkataba wa amani wao wakaendelea kuja na madai mapya.
Vita zilizofuata zilikua ni kujaribu kurudisha maeneo yaliyotekwa na Israel, ambapo haikufanikiwa ila kwa yaliyorudishwa yalirudishwa kwa njia ya mazungumzo ya amani.
Kwa kifupi, Israel haijawahi kuwa against two state solution, ila Iran ambao wanaya backup makundi ya kipalestina hawapo tayari kwa hilo.
Wapalestina wenyewe wameshagawanyika tangu ule Mkataba wa Oslo.
Tangu uchaguzi wa mwisho wa Wapalestina uliopelekea HAMAS kushinda kule Gaza, walifutilia mbali habari za uchaguzi na tangu hapo wapo kinyume na utawala wa wapalestina, Gaza ni kama imeamua kujitenga na West Bank na inajiendesha yenyewe kuvyake wakipigana kuvyao.
Ngoja niishie hapa, maana nimeandika hadi ambavyo hukutaka kuvijua wala sidhani kama upo interested.