Kipindi vita ya Ukrein na Urusi inapamba moto, Mitandao mbalimbali kama Facebook, YouTube, Instagram na mingineyo ilipiga marufuku kabisa habari zozote za kuunga mkono Urusi au kupost habari yoyote ya kuonesha Urusi inashinda. Walitaka muda wote habari za Ukrein ndio zioneshwe hili kila mtu haiunge mikono Ukrein kwa sababu Urusi ndio alikuwa mvamizi wa ardhi na muonezi dhidi ya mwenzake.
Lakini katika vita hii ya Israel na Palestina, Israel hana tofauti yoyote na Urusi kwa sababu wote ni wamelazimisha kushambulia ardhi za nchi nyingine, na Palestina ni kama Ukrein kwa sababu yeye ndio anakula kichapo mpaka ndani ya ardhi yake, na maeneo yao kuzidi kutekwa.
Mbona hapa Mitandao hii haikutaka kusimama na Palestina kama ilivyosimama na Ukrein. Mitandao hii haijaamua kuchagua upande wowote na imeruhusu habari za pande zote mbili kuwekwa mitandaoni humo. Mitandao hii inajua fika palestina anapelekewa moto, ila imeamua kukaa kimya na kutokumsapoti.
Inaonekana kabisa hii mitandao hipo kwa ajili ya kulinda masilahi ya Marekani, Ulaya na washirika wao wanaowaunga mkono kama Israel. Lakini kama wewe unatoka Asia au Afrika ukaleta ushubwada kutaka kuzingua washirika wa ulaya na Marekani, jua kabisa utapigwa vita mpaka mitandaoni.
Palestina haijapigwa vita mitandaoni kama Russia kwa sababu walioanzisha mashambulizi sio Nchi bali kikundi tu, hivyo inakuwa ngumu kwa mitandao hii kufungia habari za palestina. Japo mpaka sasa habari nyingi tunazopewa ni za kumpamba Israel ili aonekane anaonewa na hivyo anavifyeka vikundi vya kigaidi.