LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Hii clip ukiisikiliza vizuri kuna kitu lazima utang'amua, lakini wanasiasa wa Israel walipumbazwa na mkataba wa amani kati yao na waarabu.
Your browser is not able to display this video.
 
Huenda ikawa mwanzo wa 'intifada ya 3' nini ?....Au ni mpaka Hamas na Islamic Jihad wapate uungwaji mkono mkubwa kutoka nje (Jambo ambalo bado halijaonekana) ?
 
Wameanzisha ngoja tuone kama hawawezi. Israel kuanzisha ground operation ni kupunguza collateral damage inayotokana na airstrikes.

Hezbollah ilidai wakiingia Gaza inashambulia, Iran ilidai wakishambulia Hezbollah nayo inawasaidia.
Operation ya kama hiyo waliifanya mwaka 2014 lakini haikufua dafu ngoja tuone na hii
 
Ti
Tiyari Israel ina battalions 31 ziko mpakani na Gaza zinaingia. Hao Hezbollah waje nchi yao izidi kufanywa third world country, 97% ya makombora waliyorusha mwaka jana yalikuwa intercepted na mifumo ya Israel. Wao hawana uwezo wa kuzuia shambulizi la anga waje mguu kwa mguu wakutane IDF mpakani na Lebanon.

Kila mmoja ana hasara hapo ila hatutaki lawama wakipigana, wakiambiwa wafanye mazungumzo hawawezi.
 
We jamaa unafanya kama movie watu wakauwane kichwakichwa.
Bro,haya mambo hayakwepeki. Wote ni vichwa ngumu,hawaelewani,hawaelewi. Tufanyeje? Kila mmoja anajiona ndo bora. Ingelikuwa vita ya viongozi wanaoandaa hayo mashambulizi bila kuhusisha raia wa kawaida
 
Huenda ikawa mwanzo wa 'intifada ya 3' nini ?....Au ni mpaka Hamas na Islamic Jihad wapate uungwaji mkono mkubwa kutoka nje (Jambo ambalo bado halijaonekana) ?
Mkuu ebu tuachane na hayo hebu toa neno MOSAD kutokana na shambulizi hili.
 
Operation ya kama hiyo waliifanya mwaka 2014 lakini haikufua dafu ngoja tuone na hii
Operation ya 2014 unairudia ukidai haikufua dafu, unajua walienda kufanya nini?
Hamas iliteka Wayahudi, Israel ikafanya arrest ya mamia ya Hamas fighters na Waarabu, Hamas ikarusga makombora.

Israel ikaanzisha operation kuzuia Hamas isirushe makombora. Mwisho wa operation ukaisha Hamas haikuendelea kurusha makombora, Israel ilipoteza watu 70 hivi na Gaza ikapoteza watu zaidi ya 2,000 wakiwemo Hamas na raia plus majengo mengi yaliyofanywa magofu.

Operation haikufua dafu gani hilo unalotaka wewe?
 
Hizbollah sio hamas
 
Hao Hamas kama kweli wanapigania ardhi yao,hakika ni wazalendo wa kwelikweli.
 
Subiri wayahudi wa Tandahimba waje kukushambulia....

Wengi wao wanajua wayahudi ni wakristo...au wanamtambua Yesu ..
Kumbe wayahudi hata huyo Yesu wanamtukana ..wanamuita tapeli ...
Hii mbona ipo biblically mkuu ni kwa vile tu haujui na kwa taarifa yako tu Kuna wapelistina wengi wakristo kuliko wayahudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…