Dunia tangu kuumbwa kwake inatawaliwa na yule yule aliyeiumba na siku zote haitoki nje ya kanuni zake.
Sheikh anasema hizi ni dalili kutoka kwa Allah kwa wale wanaoishi baada ya Firauni na wale wanaoishi maisha aliyoishi Firauni kutokana na hukumu aliyoipata Firauni.
Firauni alikuwa akipiga ardhi kwa miguu kutokana na kiburi chake cha kutaka kuwamaliza wana wa Israel (sio Mayahudi)
Alipoinua miguu yake ili awamalize kabisa,hapo Allah akaingilia kati kuwatetea wanyonge na akammaliza Firauni.
Hivi ndivyo wanavyofanya mayahudi wa Israel sasa.Maliza kabisa wapalestina! Ondoa kabisa wapalestina Gaza, Wapeleke Sinai, Ua wote waliobaki kwa mabomu, njaa na kiu.
Sheikh akamalizia kwa kusema "Historia lazima itajirudia.Najua ndani ya Israel kuna watu wenye ubinadamu na huruma kwa wenzao.
Ni wakati sasa wa kuhama mara moja kutoka humo kabla Allah hajaingilia kuwatetea wanyonge kwa kushusha balaa ambalo halitakuwa na wa kulizuia"