LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Balfour declaration inasemaje, Palestine ni nchi au eneo!?..nini tofauti ya nchi na eneo!?..Tanzania/Tanganyika haikuwepo (sovereign state)kabla ya mjerumani kuja,wakija wakongo,wakawa wanaongea kiswahili au kisukuma na kudai hapa ni kwao,itakua halali!?..Hebrews waliokuwepo Palestine wakiishi vizuri na waarabu na walikua minorities na hawana shida na waarabu na wanapinga uzayuni wa akina netanyahu,netanyahu kuongea kiebrania na kujiita myahudi/Israel hakuhalalishi netanyahu kuwa kweli muebrania,Kama wewe unavyoongea kiingereza haimaanishi wewe muingereza
 
jana hizbullah walifanya vitu vyao miji ya karibu na mpaka kwa kutumia kombora jipya na droni.Leo huenda ni zamu ya Tel Aviv.Fuatilia utujuvye,
Malaria na ustaadh Alwaz, hivi mnafikiri nyie ndio mnaofuatilia huu mtanange pekee yenu? mbna mna mambo ya kijinga hivi, acheni kumbe Israel awashughulikie.

Heri yenu mko Tz but mngekuwa Gaza sahivi mngekuwa shimoni huko, wala jua ungekuwa unasikia tu
 
Yeye kaweka toka kwenye vyanzo vyake,ukiona vinakuwasha weka taarifa nawe zinazokupendeza,hutokosa wafuasi, tofauti na hapo soma,kausha,acha kulalamika
 
Hata wapalestina wangekuwa wakristo kwa asilimia mia kwa walichokifanya 07/10 kinastahili kichapo kizito mno.Gaidi ni kansa kwa ulimwengu wa kileo.Magaidi wawahishwe kwenye bikra 72 tuu
Akili zako ziko matakoni ww mfuasi wa nabii tito.
 
vita hii kuisha hadi kundi hilo la magaidi la HAMAS kusambaratishwa kikamilifu, kinachoendelea Gaza ni balaa kubwa.
Kesho taarifa mpya ipo,kichapo kule kinaendelea usiku weekend j3 kimya wanapumzika.
 
Man of the match,jamaa anapiga kazi kwelikweli
Power & diplomacy ya USA ipo kwenye uso wake
 
Mambo ni mengi mda hautoshi, blinken anahofu sana na yajayo.
Hii picha imepigwa juzi kwenye ndege akielekea Jordan baada ya kumaliza mazungumzo mazito na Netanyahu kuhusu ceasefire
 
Kwa mujibu wa Balfour Declaration, Palestine ya zamani ni eneo la kijiographia (geographical region), sio nchi huru kwa maana ya sovereign state.

Jaribu kutumia mifano ambayo ni realistic. Hakuna Mkongo anayeweza kuwa na uhalali wa kudai yeye ni sehemu ya Tanzania baada ya Tanganyika kupata uhuru. Hata Watanzania wenyewe wana uhalali wa kusema kuwa Tanzania ni nchi yao kwa sababu ya sheria ya kimataifa inayotambua uhuru wao kama nchi huru.

Kabla ya Tanganyika kupata uhuru, eneo lililokuwa sehemu ya Tanzania ya sasa lilikuwa chini ya mamlaka ya wakoloni wakipokezana. Hakuna jamii ndani ya Tanganyika ama kabla ya hapo iliyokuwa na uhalali wa kudai kuwa eneo la Tanganyika ni lao kiasili. Hata mipaka ya Tanzania kabla ya uhuru iliwekwa na wakoloni haohao.

By the way, kuna maeneo kadhaa ambayo yalikuwa ndani ya German East Africa kabla ya kuwa Tanganyika wakati wa Muingereza ila yalimegwa baada ya Mjerumani kushindwa Vita ya Pili ya Dunia sababu Waswahili hawakuwa na mamlaka nayo kwa maana ya sovereignty.
 
tuongee yooote, lakini cha kushukuru ni kwamba, Israel wameikata Gaza katikati, na kuzingira eneo lote ambalo Hamas wamechimba mahandaki, hivyo hawataondoka hapo hadi hamas waishiwe umeme, maji, chakula na makombora, na watawakamata kama panya tu. hilo ndio la msingi. raia wamekimbilia kusini, wale raia waliobaki kaskazini ambako israel imeshazingira wamejitolea kufa na hawatalaumu mtu kwasababu walipewa nafasi ya kuondoka. hamas sasaivi wapo katikati wamezungukwa pande zote. wanajeshi wa Israel kweli watakufa kwasababu vita ya mahandakini ni ngumu ila at the end of the day hata wakiamua kukaa kimyaa bila kupigana kwa miezi kadhaa, hamas watakufa kwa njaa au watajitokeza juu na kukamatwa.
 
Unachoshindwa kuelewa na kuzingatia ni kwamba netanyahu na Zionists wenzie hawana uhusiano wowote na Hilo eneo la Palestine,si kwao,ndiyo maana nikakupa mfano wa lugha na Imani ya kiyahudi,Mimi muislam,siwezi sema saudia kwetu kisa mtume alizaliwa huko,waisriwa 'asili' waliokuwepo wakiishi bega kwa bega na wapalestine wao wakiwa minority,na hao real Jews/Israelis wanawapinga akina netanyahu,Zionism ni political movement iliyochanganywa na dini,netanyahu hapo Palestine Hana uhusiano napo,mfano wa Tanganyika na wakongo usiukwepe,Kuna wanyamwezi walienda Kongo zamani na mpaka Leo wapo huko na lugha yao inashabihiana na kinyamwezi,siku wakirudi tabora na kudai nchi yao itakua sawa!?
 
SHERIA gani ya kimataifa Na wewe, UN si imeanzishwa 1945? Unaweza ukaanzisha kitu 1945 kije kutoa hukumu ya Vitu vilivyotokea kabla? Leo Kuanzishwe Sheria kula Wali haifai halafu tukukamate sababu ulikua Wali mwaka jana ina make sense kwako?
Hiyo ni tofauti na "Palestine" ambayo haikuwahi kuwa nchi huru kabla ya 1947, vilevile hata sasa hivi hakuna nchi huru inayoitwa "Palestina" inayohusisha eneo la Israel ya sasa.
So Ina maana kabla ya Uhuru wa Tanganyika wangepewa Wa Iran Nchi tukafukuzwa sisi according to you Ingekua sawa sio? Sababu 1960 haukuwa na Uhuru.
Nimeongea mambo mengi tu kuanzia miaka ya 1700 wakati Napoleon alipo taka kuwaleta Wayahudi Palestina na Evidence Zipo library ya kiyahudi na link nimekuekea ila Evidence zote unazipotezea na kuandika unachoamini wewe.

Endelea mkuu kuamini unachotaka sometime ngumu kubishana na mtu ambaye ana majibu yake tayari kichwani.
 
Yeye kaweka toka kwenye vyanzo vyake,ukiona vinakuwasha weka taarifa nawe zinazokupendeza,hutokosa wafuasi, tofauti na hapo soma,kausha,acha kulalamika
Umefuatilia hiko chanzo?
Link ina banner peke yake loh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…