LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Unachoshindwa kuelewa na kuzingatia ni kwamba netanyahu na Zionists wenzie hawana uhusiano wowote na Hilo eneo la Palestine,si kwao,ndiyo maana nikakupa mfano wa lugha na Imani ya kiyahudi,Mimi muislam,siwezi sema saudia kwetu kisa mtume alizaliwa huko,waisriwa 'asili' waliokuwepo wakiishi bega kwa bega na wapalestine wao wakiwa minority,na hao real Jews/Israelis wanawapinga akina netanyahu,Zionism ni political movement iliyochanganywa na dini,netanyahu hapo Palestine Hana uhusiano napo,mfano wa Tanganyika na wakongo usiukwepe,Kuna wanyamwezi walienda Kongo zamani na mpaka Leo wapo huko na lugha yao inashabihiana na kinyamwezi,siku wakirudi tabora na kudai nchi yao itakua sawa!?
Nilishauri kwamba tuutazame huu mgogoro katika perspectives zote! Nina maswali kadhaa kwaajili yako:

1) Ni kwa sababu zipi Wayahudi wanaofahamika kama "Zionists" hawana uhusiano na hilo eneo?

2) Je, Wayahudi waliotoka Ulaya na kwingineko na kuhamia "Palestine" chimbuko ama asili yao ni wapi hasa?

3) Ni nani alikuwa na uhalali (legality) wa milki ya eneo lililoitwa "Palestine" wakati wa Zionism?

Mfano wako kuhusu Wakongo nimeshauzungumzia. Sijaukwepa! Tanzania ni sovereign state. Hakuna uhalali wowote wa hao Wakongo kudai "nchi yao" ndani ya Tanzania bila ya Tanzania yenyewe kupoteza uhuru wake kwanza.

Vilevile, Tabora haijawahi kuwa nchi huru yenye mipaka inayotambulika. Kulingana na sheria ya kimataifa, mfano wako hauna uhalisia. Huwezi kudai kurudishiwa kitu ambacho haukuwa nacho hapo awali!
 
Wewe bado hujajua mambo,ni kweli ila Mungu Huwa haachi agano lake hata kama Hawa jamaa walimtenda dhambi,mwisho wa nyakati watarudiwa tena na Bwana
Bado wakristo wengi hawajui Neno la Mungu na wanaishi bado Agano la kale. Yumeshatoka huko na mambo ya kale yamepita na hayatarudi tena.

Kama ambavyo hatutarudi tena kuchinja kondoo na kunyunyiza damu ndivyo mambo ya Israeli wa kale yamepita. Taifa la Mungu sio hao akina Netanyahu bali ni mimi na wewe na wale wamwaminio Yesu Kristo na kuishi utakatifu.
 
SHERIA gani ya kimataifa Na wewe, UN si imeanzishwa 1945? Unaweza ukaanzisha kitu 1945 kije kutoa hukumu ya Vitu vilivyotokea kabla? Leo Kuanzishwe Sheria kula Wali haifai halafu tukukamate sababu ulikua Wali mwaka jana ina make sense kwako?

So Ina maana kabla ya Uhuru wa Tanganyika wangepewa Wa Iran Nchi tukafukuzwa sisi according to you Ingekua sawa sio? Sababu 1960 haukuwa na Uhuru.

Nimeongea mambo mengi tu kuanzia miaka ya 1700 wakati Napoleon alipo taka kuwaleta Wayahudi Palestina na Evidence Zipo library ya kiyahudi na link nimekuekea ila Evidence zote unazipotezea na kuandika unachoamini wewe.

Endelea mkuu kuamini unachotaka sometime ngumu kubishana na mtu ambaye ana majibu yake tayari kichwani.
Vitu gani vilivyotokea kabla? Umetoa mfano ambao ni unrealistic!

Iran haijawahi kuwa na mandate ya eneo la Tanganyika kwa namna yeyote ile. Hakuna Mswahili aliyefukuzwa ili Muirani apewe "nchi". Kihistoria, wafanyabiashara wenye asili ya Uajemi (na Waarabu pia) waliweka makazi yao maeneo mengi ya pwani ya Bahari ya Hindi na kisha kuchanganyika na jamii zingine. Hakukuwa na nchi huru iliyoitwa Tanganyika wakati huo.

Maana yake ni kuwa, kama kulikuwa na population inayotambulika ya wazaliwa wa Tanganyika wenye asili ya Iran ndani ya eneo la Tanganyika, ilikuwa halali na wao pia kuwa Watanzania baada ya uhuru. Pia ni halali kuwa raia wa Tanzania kwa mtu yeyote yule ambaye alirejea Tanganyika kabla ya uhuru kama mzawa [wa asili] wa eneo la Tanganyika (na Zanzibar vilevile).

Tukirejea Palestine ya zamani, hiyo barua ya Napoleon unayoisema haithibitishi utaifa wa "Palestine" kama nchi huru ya Wapalestina wa sasa. Isitoshe, "Palestine" inayotajwa humo ni "land of ancient Israel" kipindi Wayahudi wakiwa uhamishoni kutokana na umateka wa madola yaliyokuwa yakiitawala "Palestine".

Nadhani haya sio mabishano tu. Wengine tupo hapa kuelimishana!
 
Una Mahaba ,Kajiunge na Taifa Teule ,mshambulie maadui zenu.
Wale hawaitaji watu kujiunga Kama mlivyojiunga kule misri na waarabu wenzenu. Kilichotokea misri ataki kusikia juu ya kupigana na Israel zaidi ya mazungumzo tu
 
tuongee yooote, lakini cha kushukuru ni kwamba, Israel wameikata Gaza katikati, na kuzingira eneo lote ambalo Hamas wamechimba mahandaki, hivyo hawataondoka hapo hadi hamas waishiwe umeme, maji, chakula na makombora, na watawakamata kama panya tu. hilo ndio la msingi. raia wamekimbilia kusini, wale raia waliobaki kaskazini ambako israel imeshazingira wamejitolea kufa na hawatalaumu mtu kwasababu walipewa nafasi ya kuondoka. hamas sasaivi wapo katikati wamezungukwa pande zote. wanajeshi wa Israel kweli watakufa kwasababu vita ya mahandakini ni ngumu ila at the end of the day hata wakiamua kukaa kimyaa bila kupigana kwa miezi kadhaa, hamas watakufa kwa njaa au watajitokeza juu na kukamatwa.
Kazi yao Hamas imekwisha, Israel ni wahuni sio wajinga watatumia sumu kali humo,sema tu mateka wako kwenye hizo tunnels🤣🤣🤣🤣🤣

Israel nguvu yake ni kubwa na pia wana teknolojia, yaani hadi bulldozers za kijeshi😁😁😁😁😁 armored bulldozer aise Israel nomaaaa!!!!

Wawe makini tu wasidhuru raia, ila wale wajuu angani walioshusha mabomu siku za mwanzoni mwanzoni walitumia mihemuko na hasira sana walioua sana raia🤭🤭🤭🤭🤭🤭🤭🤭
 
Hizo mipicha yalipigwa kipindi hawajavamia Israel na kuchinja watoto ustaadh, saiz hakuna Hamas mtaani Gaza usitudanganye bibie🤣🤣🤣

Hamas hawezi vaa gwanda saiz na ajitokeze hadharani, wote wako chini ya ardhi ila wanafuatwa huko huko na wahuni wa IDF
Mwambie saa hizi Hamas wanavaa baibui na ushungi Kama yeye.uwezi tofautisha maana wote wanaonekana Ni wa kike
 
lakini ina ushawishi na wafuasi ndani ya West Bank vilevile.
Lakini haina active militants wa Hamas wala tunnel networks kufanya mashambulizi. But they equally get rough treatment kama Gaza tu from the zionist regime.
Labda kuwepo na hoja na ushahidi kwamba hayo mauaji yanayofanyika West Bank ni ya makusudi
Mkuu ina maana hujui kuna drone attacks zinafanyika West Bank?

Mind you kila siku aettlers wanaletwa huku nyumba za palestinians zikivunjwa!! Ila unakuta mtu anakomaa kuwa "Hamas" ndio chanzo!!
 
1:6 SRUVDC​

Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waiiteka nyara kabila nzima, wawatie katika mikono ya Edomu,Bwana atatuma moto juu ya Gaza uyateketeze majumba; Always bible prophecy Huwa inatimia

SRUVDC: Swahili Revised Union Version
Shirikisha
Mambo ya wafilisti na palestina wapi na wapi? Unabii wa Edomu na leo hayo makabila yameshapotea na yanayoendelea palestina wapi na wapi? If that's the case niambie kwanini kabila la Dani limefutwa ilihali Mungu aliahidi kutowaacha wana Israel milele? Ukielewa ndii utajua Bible is dynamic usikariri.
 
Nani kakudanganya Wapalestina wote ni waisilamu?
Wapalestina Wakristo hata 3% hawafiki, ni negligible asilimia chache kuliko hata Wakristo wa Saudi Arabia. So tukisema takribani Wapalestina wote ni Waislamu hiyo sio ajabu.
Na si useme tu kweli Usa ndio kasababisna Wakristo wengi wakimbie Lebanon?
Si ni kama hivi umesema unavyohisi, au ulitaka niseme kila kitu cha Wakristo Palestina? Mbona hujasema wanavyonyanyaswa uko Gaza hadi wapo wachache, au nayo hii tumlaumu USA. Almost Wakristo wote wa Palestina wapo West Bank.
 
1:6 SRUVDC​

Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waiiteka nyara kabila nzima, wawatie katika mikono ya Edomu,Bwana atatuma moto juu ya Gaza uyateketeze majumba; Always bible prophecy Huwa inatimia

SRUVDC: Swahili Revised Union Version
Shirikisha
Huelewi chochote.
 
Kazi yao Hamas imekwisha, Israel ni wahuni sio wajinga watatumia sumu kali humo,sema tu mateka wako kwenye hizo tunnels🤣🤣🤣🤣🤣

Israel nguvu yake ni kubwa na pia wana teknolojia, yaani hadi bulldozers za kijeshi😁😁😁😁😁 armored bulldozer aise Israel nomaaaa!!!!

Wawe makini tu wasidhuru raia, ila wale wajuu angani walioshusha mabomu siku za mwanzoni mwanzoni walitumia mihemuko na hasira sana walioua sana raia🤭🤭🤭🤭🤭🤭🤭🤭
Ni jambo baya lakini, ukisikiliza media za ndani ya Israel, raia wa kawaida wanatamani Netanyau adondoshe bomu kubwa lifute Gaza afu ajiuzulu. ni ajabu nimesikia hivyo, itakuwa ni kosa kubwa sala na kivita na wataongeza chuki. najuahilo hawatakuja kufanay hata siku moja. pia, wanajeshi wengi wa Israel wanakufa ila wamejitolea kufa as long as at the end of the day Hamas atafutwa. Hamas walijiandaa kwa muda mrefu sana na ni makomandoo wa ukweli sio wa mchezo mchazo kiasi kwamba wangekuwa na nguvu sawa za kijeshi, israel asingechukua hata wiki wangeshaimaliza, sasa zana ndio wanakosa ila uwezo wa mmoja mmoja wanao mkubwa na wametrain kwa muda huko Iran na maeneo mengine duniani. what we are praying ni kwamba, Hamas wajisalimishe na amani ipatikane, maisha yaendelee kwasababu wapalestina wengi sana wanakufa, na Mungu hafurahii wanavyokufa hata kama wamemkataa wakamkubali allah asiye mungu wa kweli. Mungu wa Israel hafurahii kifo cha mwenye dhambi hata siku moja anatamani kila mtu aifikirie toba ili apote, upendo wake kwetu ni sawa kwa wote generally (though wale wanaompokea ndio huwa watoto wa karibu zaidi nani mboni ya jicho lake).
 
Wapalestina Wakristo hata 3% hawafiki, ni negligible asilimia chache kuliko hata Wakristo wa Saudi Arabia. So tukisema takribani Wapalestina wote ni Waislamu hiyo sio ajabu.

Si ni kama hivi umesema unavyohisi, au ulitaka niseme kila kitu cha Wakristo Palestina? Mbona hujasema wanavyonyanyaswa uko Gaza hadi wapo wachache, au nayo hii tumlaumu USA. Almost Wakristo wote wa Palestina wapo West Bank.
Mkuu rudi tu kwenye mambo yako ya silaha haya mambo hata huyajui kila ukifungua midomo kuandika unaandika data za uongo.

1. Hizo data za asilimia 3 ama 2 ni data za Wakristo wa Sasa ambao wanaishi Palestina ambao bado hawajafukuzwa na sio wapalestina wote Wakristo, kila kundi la wapalestina lina namna yake ya kupigana na Wakristo wengi wameenda Lebanon na South America.

2. Estimation Asilimia za Wapalestina Wakristo ni zaidi ya 10, na kama nilivyokuambia juu na sehemu nyengine wapalestina wengi Wakristo wapo South America na wao wanafanya mapambano yao kwa njia nyengine, kama Umeona hii vita Nchi za kwanza kufukuza Mabalozi na wanadiplomasia wa Israel ni za south America. Chile pekee kuna Wapalestina 500,000.

3. Kwa data za 1922-1947 population yao ili range asilimia 9-11,

Pia mkuu Data hazidanganyi, unahisi hao Wakristo wa Palestina ni mabubu? Nimekupa Phrase ya Raisi mkristo akielezea kwanini wanaungana na Kina Hezbollah

Hii ni Survey Ilifanywa kwa hao Wakristo, Asilimia 88 walishiriki so ni Almost wote

As far back as 1993, 88 per cent of Christian Palestinians surveyed about emigration specified the economic situation. In a 2006 survey, 78 per cent of Christian respondents to a Bethlehem-based poll said “Israeli aggression and occupation are the main cause of emigration”, while only 3.1 per cent exclusively blamed the “rise of Islamic movements” (12.1 per cent said it was a combination of the two). More than half of those Christians surveyed had at least one relative whose land had been confiscated by Israel.

So asilimia 78 ya Wakristo wa Palestina wanaamini Israel ndio Amewafanya hadi leo wapo hivyo Ila wewe upo huku Tanzania hata hujui Hezbollah ni Sunni ama shia unajifanya unajua na Unawasemea wanachopitia?
 
Vitu gani vilivyotokea kabla? Umetoa mfano ambao ni unrealistic!

Iran haijawahi kuwa na mandate ya eneo la Tanganyika kwa namna yeyote ile. Hakuna Mswahili aliyefukuzwa ili Muirani apewe "nchi". Kihistoria, wafanyabiashara wenye asili ya Uajemi (na Waarabu pia) waliweka makazi yao maeneo mengi ya pwani ya Bahari ya Hindi na kisha kuchanganyika na jamii zingine. Hakukuwa na nchi huru iliyoitwa Tanganyika wakati huo.

Maana yake ni kuwa, kama kulikuwa na population inayotambulika ya wazaliwa wa Tanganyika wenye asili ya Iran ndani ya eneo la Tanganyika, ilikuwa halali na wao pia kuwa Watanzania baada ya uhuru. Pia ni halali kuwa raia wa Tanzania kwa mtu yeyote yule ambaye alirejea Tanganyika kabla ya uhuru kama mzawa [wa asili] wa eneo la Tanganyika (na Zanzibar vilevile).
Ina Maana hujui Historia ya kilwa kwamba Iliuzwa kwa Prince wa Iran?
Tukirejea Palestine ya zamani, hiyo barua ya Napoleon unayoisema haithibitishi utaifa wa "Palestine" kama nchi huru ya Wapalestina wa sasa. Isitoshe, "Palestine" inayotajwa humo ni "land of ancient Israel" kipindi Wayahudi wakiwa uhamishoni kutokana na umateka wa madola yaliyokuwa yakiitawala "Palestine".

Nadhani haya sio mabishano tu. Wengine tupo hapa kuelimishana!
Mkuu unabishana vitu obvious hayo mambo yako ya Sovereign ni vitu vya sasa ni vitu ambavyo vimetengenezwa karibuni, kama sio Berlin Conference basi ni baada ya UN kutengenezwa.

Palestina as Palestina ipo maelfu ya miaka, hata kabla Yesu hajaja.
1. Palestina imetajwa Ancient Greek na Historians wao
2. Palestina Imetajwa Ancient Egpty na Ramesses III
Wote hao kabla ya Yesu kuja.

Kama hao wagiriki sio tu wameitaja hadi mipaka imetajwa hii Ramani ambayo imetengenezwa karne 5 kabla ya kuja Yesu
HERODOTUS(1897)_p2.387_THE_WORLD_ACCORDING_TO_HERDOTUS.jpg

Hii ni Tablet ya Ancient Egpty ikionesha walikua wanafanya biashara na Palestina

Egyptian_-_Statue_of_a_Vizier,_Usurped_by_Pa-di-iset_-_Walters_22203_-_Back.jpg

Hii ni Picha Ya Mateka wa Palestina nayo pia ipo Ancient Egpty
800px-Bas_relief_de_prisonniers_philistins_sur_la_facade_sud_du_deuxième_pylône_(2).jpeg

Ushahidi upo mwingi mno, huo wote ni kabla ya Roma hawajaja, then Wakaja Roma, Then Waisilamu, then British hadi leo.
 
Back
Top Bottom