Wakati Wayahudi wanauliwa na Adolf Hitler, Urusi alikuwa mstari wa mbele kabisa kusimama na Israel kuhakikisha wanapata haki yao, wakawatetea kwa nguvu zote na ndiyo maana tangu zamani mpaka sasa hivi Israel na Urusi huwa wanaheshimiana sana.
Sasa bhana! Unajua kwa nini vita na Ukraine ilikuwa ngumu sana mpaka kuamua kupumzika? Mlango wa nyuma, Israel alikuwa anamsaidia silaha Ukraine, na pia alikuwa anahakikisha jamaa wanaingia katika muungano na NATO.
Hili lilimkera sana Urusi, alimuona Israel kama msaliti! Kwa nini umsaidie Ukraine? Kwa nini unataka kumuingiza kwenye uanachama na NATO? Sasa ishu ya Palestina, wamewekwa kama chambo, nyuma yake yupo Urusi na Iran.
Kundi dogo kama Hamsa limefadhiliwa na kupewa silaha na kila kitu, ndio maana wameweza kutamba mbele ya israel.
Iran anaingia kama kutaka kulipa kisasi, bado kumbukumbu zake za kupigwa na Israel, kuuliwa kwa wanasayansi wake inawaumiza sana kichwa. Wamesema wapo nyuma ya Palestina, je, wataendelea kuwa nyuma yake ama watamuacha mambo yakichanganya?
Saudi Arabia naye ameingilia, anasema yupo nyuma ya Palestina, je, ataendelea kuwa nyuma yake Israel akiamua kupiga Waarabu wote kama alivyofanya kipindi cha nyuma? Hatujui. Ngoma bado mbichi. Tuombe Mungu tu majibu ya Israel yasiwe makubwa kama ya kipindi kilichopita na kumaliza watu wengi wasio na hatia.
Majira ya jioni tarehe 7/10/2023, Marekani imetangaza kuunga mkono tangazo la Israel la kujilinda kwa kuendesha vita ya Kigaidi katika ardhi ya nchi zingine HURU za Palestine, Syria nk, Wakati huo Marekani hiyohiyo inapingana Urusi kujilinda. Kumbaaaafu kabisa, Ukiunga mkono Israel kujilinda, unga mkono pia Urusi kujilinda.
Utawashangaa watu walivyo brainwashed na Media za kimagharibi na udini juu, hasa waswahili wa Bukoba na Mbarali huko waliokuwa wakilishwa propaganda kuwa Urusi imefanya kosa kubwa kuvamia nchi huru ya Ukraine kwa hoja kuwa Urusi inajilinda dhidi ya maadui, Leo watu walewale wako Israel wanaunga mkono Israel kujilinda dhidi ya maadui.
Ifahamike, kabla ya mashambulizi ya jana ya Hamas, Kwa miezi zaidi ya miezi 15 Israel ameendesha Oparesheni Palestine, Syria, Jordan nk kwa kile alichosema anasaka magaidi. Anafanya mashambulizi katika nchi huru bila idhini ya nchi husika. Hoja yake kuu ni kuwa analinda maslahi ya Israel, akaungwa mkono na mjombo wake USA, lakini Umoja wa mataifa ukawa kibogoyo...
Alichokuwa anafanya Israel ndicho alichokifanya Urusi kwa miezi zaidi ya 18 huko Donbass. Lakini Marekani na vibaraka wake wakasema Urusi anafanya uvamizi... Urusi akaweka hoja ileile iliyotolewa na Israel kuwa analinda maslahi ya Moscow.
Sasa kelele za nini juu ya majibu ya Hamas? Dunia itulie kila mtu alinde maslahi yake kwa kudhibiti wakorofi wote duniani ambao ni Manazi wa Ukraine wakiongozwa na kibaraka Zelensky na magaidi wa Hamas chini ya Mamlaka ya Palestine.
Hatutaki kelele za huruma za Israel baada ya kubondwa, watulie waendelee na Oparesheni yao. Binafsi siku zote mimi huunga mkono taifa lolote linalojilinda, na nimekuwa hivyo naunga mkono Israel kujilinda kwa 100% vivyo hivyo naunga mkono Urusi kujilinda kwa 100%. Marekani ni mchokozi kila kona ya dunia na ndie muundaji wa makundi yote ya Kigaidi duniani akiyaita ni wapigania Demokrasia ama utaifa, akichoka kuyatumia anayabatiza jina la Ugaidi.