Watoto wawili wa Gaza wamewakilisha wenzao kuomba chakula kwa mtindo wa kupanda juu ya nguzo za umeme ili wasikiwe na askari wa Israel upande wa pili wa ukuta unaotenganisha Gaza na nchi hiyo.
Tunakaribia kufa,tunaomba chakula walisikika wakisema huku wakibembelezwa na wakubwa wao washuke hizo ni nguzo zina umeme ,
Baada ya hapo watoto hao waliendelea kupaza sauti na kuzitaja nchi kadhaa za kiarabu moja baada ya nyengine wakizitaka ziwaokoe na vifo kwa kuwaletea chakula.
Enyi watu wa Saudia na Oman tuleteeni chakulaa.....