PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
Two State solution inaonekana haitawezekana tena sababu walichokifanya waarabu ni kufanikiwa kuwafanya Wapalestina kuwachukia waisrael, kitu ambacho wamefanikiwa sana.Nimekupata mkuu, Ila hii ndoto ya two states solution ni kama vile imeshajifia tu, hata Israel hawaitaki tena ndio maana mazungumzo yote kuhusu hili yamekwama sababu ya kuendelea kwa upanuzi wa maeneo ya 'settlers' wa Israel kwenye ardhi za Wapalestina.
Wapalestina walishakuwa na maeneo yao ambayo ndiyo wangeyatawala, lakini waarabu hawataki kabisa kulisikia hilo, wanachofundishwa ni Israel kufutwa kabisa, huku gharama ya misimano hiyo ikibebwa na wapalestina.
Kizazi cha sasa cha Wapalestina, kimeshasahau historia yao na sasa kimezaliwa na kukuzwa katika misingi ya Chuki.
Israel na wao wamelazimika kuwaonya watu wao kuhusiana na wapalestina, kwamba wale kiasili ni adui zao wenye lengo la kufanya kila wawezalo ili kuwafuta hivyo wanapaswa kuwa makini nao sana.
Wapalestina walikuja na mbinu ya kuanzisha mahusiano na waisrael na kupelekea kuoana. Lengo lao lilikua ni kuwa naturalised kama waisrael na kuupata haki zote na baadaye warudi kati maeneo waliyokua wakiishi kabla ya ile first Arab - Israel war.
Israel ilistukia mpango huo, ikaweka sheria inayoondoa naturalization. Wanasema Israel ni ya Wayahudi na itabaki kuwa hivyo. Ingawa sheria hii imekua ikilalamikiwa kuwa ni ya kibaguzi, inawabagua Waisrael wasio Wayahudi. Kuna 15 - 18%ya waisrael ambao ni waarabu hivyo sheria hiyo itakua inawabagua.