Uamuzi ulipitishwa na Baraza Kuu la UN (Nov 1947), ikiwemo Marekani na USSR.
Ardhi ya Palestina zaidi ya nusu (56%) ilikabidhiwa kwa Wayahudi, huku Yerusalemu ikiwekwa chini ya usimamizi wa kimataifa.
Wayahudi walikubali mpango huo, lakini Waarabu wakakataa kuuafiki.
Mapigano ya Wayahudi na Waarabu Palestina yakazuka mara tu baada ya uamuzi wa UN.
Kufuatia vita hivyo, Israeli ilifanikiwa kuchukua maeneo mengi ya Waarabu wa Palestina, ikiungwa mkono na Mfalme Abdullah wa Transjordan (Jordan kwa sasa), ambaye hakupenda Palestina iwe nchi huru kwa sababu ya maslahi binafsi ya kutaka kuimiliki yeye.
Hadi kufikia mwaka 1950 (miaka 3 tu baadaye) Israeli ilikuwa ikimiliki 77% ya ardhi ya Palestina. Mfalme Abdullah alikuwa amejitwalia Mji wa zamani wa Yerusalemu na eneo la kati la Palestina (sasa yajulikana kama West Bank).
Wakati huu ni Waarabu wapatao 160,000 pekee ndio walikuwa wamesalia katika maeneo yaliyokuwa yakitawaliwa na Israeli.