LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Sasa ulitaka Hamas wakae tu ili wanajeshi wa Israel wawauwe?
Israel anacho ambiwa ni afuate sheria za vita na sio kupiga piga hovyo kama ni kupambana apambane na hamas awaangamize kama anavyo sema na sio kuuwa raia.
Vip upande wa Hamas hawafanyi mauaji ya raia?
Vip zile rocket 🚀 walizo kua wanarusha wanachagua target 🎯? Military bases au mpaka kweny makazi ya raia?
 
Mkuu nenda telegram search chanel inaitwa "Intel Slava Z"

Hii chanel ni ya Warusi na ni pro Putin, nenda kaone wanaposti jinsi hamas wamavyopelekewa moto.

Pamoja na kwamba ni chanel ya pro hamas na Putin lakini post zao 99% ni za IDF ikipeleka moto kwa hamas.

Yani mmekaa hapo msikiti wa kwa mtoro mnadanganyana eti israel inapigwa na hamas?
[emoji23] [emoji23]
Kwa hiyo huo ndo udhibitisho wa picha kutoka IDF?
 
Jeneral wa Jeshi la Urusi Bwana Andrei Gorolyov ambaye pia ni afisa mwandamizi huko Urusi amekiri kuwa kwa taarifa zake rasmi ni kuwa wanajeshi zaidi ya 500 wa Israel washaangamizwa hadi sasa!!

Jenerali wa Urusi Andrei Gorolyov [emoji635]: "Kulingana na taarifa zangu, idadi ya wanajeshi wa Israel waliouawa ni takriban 500." "Ufadhili wa Hamas unatoka Uturuki na Qatar, hiyo ni kweli.

Kwa sababu fulani, kila mtu anazungumza juu ya Irani, kwa hivyo lengo ni Iran? Wanataka kuiingiza Iran kwenye mzozo na kuishinda ili kulishinda taifa hilo?

. Katika miongo kadhaa iliyopita, Iran imepata maendeleo makubwa katika uzalishaji wa silaha za kisasa, na ndio maana hata aircraft carrier za kubebea ndege ya Marekani hawafurukuti lakini Wamarekani hawajali hasara na uharibifu utakaotokea.

Bali wanataka Israel kupigana na kila mtu, kwa hivyo tuko vitani na America na amani haitakuja.

BREAKING[emoji599][emoji599]: Russian General Andrei Gorolyov [emoji635]: “According to my information, the number of Israeli army personnel killed is about 500.” “Hamas’ funding comes from Türkiye and Qatar, that’s true.
For some reason, everyone is talking about Iran, so the target is Iran? They want to drag Iran into the conflict and defeat this republic.
Over the past decades, Iran has made serious progress in the production of modern weapons, and that is why the American aircraft carrier groups do not approach, but the Americans do not care about the losses and destruction that will occur.
Rather, they want Israel to fight everyone, so we are at war with the United States, and peace will not come. On Earth, there is only a multipolar world and the departure of the hegemonic power.”View attachment 2799627

Israel ni maji, usipoyanywa, utayakoga.
 
Idadi ya wanajeshi wao waliokufa jana tu ni zaidi ya 70 lakini wanaficha data na ukweli sijui kwanini wamekua na hii tabia tokea zamani?

Wanajeshi zaidi ya 500 washauliwa tokea hii vita ianze kwa Hezbollah pekee wanajeshi wa Israel waliokufa kwenye majibizano na Hezbollah tokea tarehe 07 October ni zaidi ya 120!

Hii vita inaenda kumuelemea sana masaa yajayo mbeleni. Nasema haya kwasababu ijumaa Hezbollah watatoa tamko rasmi la kujiunga na hii vita rasmi na wametoa matamko kabisa kuwaambia Israel kuwa mwisho wa kuamua kusitisha mashambulizi ni Ijumaa asubuhi.

Jana Yemen wametangaza kujiunga na hii vita na usiku walirusha makombora kama manne Israel mawili yalilenga shabaha kikamilifu!

Na tunafahamu ukweli kuwa Israel hawezi kusimama mwenyewe, hapo Gaza tu kapewa misaada ya matrilioni ya pesa, silaha za bure na wanajeshi kutoka US na UK lakini bado hajaweza kuteka hata kilometa moja!! Sasa ubora wa hawa watu unatoka wapi?

Jeshi gani hili?Kwa jeshi la anga wapo vizuri sana, hilo nakiri kabisa kuwa Israeli wana jeshi bora la Anga pale Mashariki ya kati!! Lakini jee vipi kuhusu jeshi la nchi kavu?Wanachojua ni kupiga angani tu na kuua wanawake na watoto!!Hivi Hamas wangekua hata na kifaru kimoja au magari ya kijeshi matano tu Telaviv pangekalika?

Hivi mnaosema Israel wana jeshi bora mnalizungumzia jeshi lipi?Wanajeshi wapi hao? Hawa maticktoker na maslay Queen? Israel hajawahi kupigana mwenyewe na hawezi kusimamia vita mwenyewe bila misaada!

Sasa soon atapigana na Hamas, Hezbollah na Answarullah ya Yemen! Hapo ndio ataanza kuzidiwa mwenyewe tu.

Itafika mahali wataomba Ceasefire wao wenyewe tu pale maji yatakapowafika shingoni.

Hamas walivyosema Gaza itageuka makaburi na kuzimu kwa Wazayuni hawakutani!Wanaenda wanajeshi 50 wa Israel Gaza wanarudi 15 sasa si uwendawazimu huo?Wewe unapiganaje vita na watu waliokubuhu kwenye mapigano?

Unajua Israel hii vita itamcost sana na sasa hivi duniani hana support ya jamii yoyote ile katika mitazamo ya watu.

Imagine uungaji wa Palestina kidunia umepanda mpaka 80% kutoka 44% mwaka 2014.

Jana mmeona mkutano wa Bilinkelin umevamiwa na wanaharakati? Soon tutaongea lugha moja tu!! Walijificha nyuma ya media safari hii wanaumbuka mchana kweupe ziko wapi zile story za Hamas beheaded 40 Israel babies?

Nikiwaambia safari hii hadi propaganda zao zimefeli huwa namaanisha kabisa. Sasa dunia imebadilika sana labda waje kuwadanganya baadhi ya wafia taifa lao huku Africa ambao wengi shule na uelewa hamna.

Aibu ambayo Israel ameanza kuipata ni noma tupu subirini Hezbollah wajiunge na hiyo vita ndo Wazayuni watajua hawajui.
Mzee tulia kwanza unywe maji. Mbona kama unafukuzwa.
 
Kufa vitani hiyo sio hoja, hata manati inaweza kukuua
Hoja ni kuwa hicho ni kikundi cha watoto wadogo kinapambana na jeshi la wayahudi lenye mafunzo bora duniani huku wakisaidiwa na mashoga na mabwana zao wa USA.
 
Huu ni wakati wa Serikali ya Tanzania kuvunja mahusiano na Israel haraka sana kwa yanayoendelea huko Gaza!!

Huko nyuma tuliwahi kusema kuwa "kila mtu anastahili haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake". Pia tulisema kwamba kila watu wana haki ya kuwa na mahali ambapo watakuwa salama kutoka vitisho vyovyote vya utu wao na nafasi yao kama jamaa.

Tokea enzi za Nyerere tuliamini ya kwamba hakuna mwanadamu mwingine ambaye ana haki ya kumtawala kwa nguvu mwanadamu mwingine kwa kisingizio chochote kile. Hii ilikuwa ni falsafa yetu dhidi ya ukoloni.

Leo hii tunashuhudia yanayoendelea Palestina ambapo karibu maelfu ya watu wameshauawa. Je, Bunge linapokutana siku chache zijazo zilaani mauaji hayo? Je, serikali ilaani pande zote mbili kwa kusababisha mazingira ambayo yanamnyima mwanadamu nafasi ya kuwa huru kufanya lolote? Tunapaswa tuungane na nchi nyingine mfano Bolivia ambazo zimevunja uhusiano na Israel kutokana na suala la Gaza

Hatuwezi kuendelea kulisapoti taifa la kigaidi ambalo lina mchango mkubwa wa ubaguzi wa Rangi na.ambalo limeshiriki kuwaangamiza Waafrika wengi mfano wakati wa makaburi walitoa misaada ya kila aina kwa makaburu ili waendelee kuwauwa watu weusi kule Africa ya kusini bado zile cases za waafrika waethiopia kufungwa vizazi wasizae kwa nguvu!

Kwa yanayoendelea naiomba serikali ivunje uhusiano mara moja na huu utawala katili wa Israel View attachment 2799632View attachment 2799631View attachment 2799633View attachment 2799634
C umesema Israel anapata kichapo kutoka kwa Hamas au umejizima Data tena
 
Mlishaambiwa Gaza itakuwa graveyard Kwa mvamizi yoyote , nadhani mmeshaanza kuona uhalisia ni jinsi special forces za Marekani na mashoga wa Kizayuni wanavyoshikishwa ukuta
Ngoja muone balaa
 
Wayahudi waliwahi kusema askari wao mmoja sawa na Wapalestina elfu moja.

Jinsi askari wa kiyahudi wanavyouliwa kuna majenerali wa IDF wameshamgeuka netanyahu, wanasema jeshi lao ni la ulinzi siyo la mashambulizi.
 
Kwenye uhalisia wa hoja usirudie tena kuleta singeli za "unge, inge" sababu wewe mwenyewe usingezaliwa duniani ungekuwa si chochote.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Nimekosoma na nimeitwa wenzangu wamesoma ulichoandika lakini wote wamesema itakuwa kaandika kinyarwanda au kule kwa kina TP Mazembe. Hatukuelewa kitu, degree holder
 
Funny Russia hajui idadi ya askari wake waliokufa huko Ukraine ila yupo busy na vifo vya askari wa IDF
Jamani si tulikubaliana russia kuna jews wengi kwahiyo yupo upande wa israel imekuwaje tena, tatizo bado wakristo wa tanzania hawajajua chanzo cha huu mgogoro wao na maaskofu wao wanadanganyana tu , russia ,china , north korea na waarabu wote wameungana wanawavizia magharibi wakosee tu wamalize kazi
 
Back
Top Bottom