Yanayotokea Kenya ni matokeo ya Viongozi kutokusikiliza matatizo ya wananchi na kujiona wao ndiyo kila kitu

Smith Rowe

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2018
Posts
4,319
Reaction score
9,003
Wakenya walianza kulalamika mda sana kuhusu Zakayo kusafiri sana kutafuta mikopo lakini maisha yao bado ni magumu.

Vijana wako mtaani mambo yao ni magumu ajira hamna, mazingira ya biashara ni magumu, hawasikilizwi, wakilalamika viongozi wanajifanya viziwi.

Viongozi kutwa kucha kupitisha miswada ya kujilimbikizia mali, kujinunulia magari ya kifahari, kuiba mali za umma na kufanyia biashara zao.

Matokeo yake kila mtu analalamika mitaani bado wakakataa finance bill lakini viongozi wanawaona wao hawajui kitu wakaipitisha na hayo ni madhara yake.

Na Tanzania asilimia 100 yanayofanyika ni sawa na Kenya tofauti ni kuwa tuu Watanzania hawajaingia barabarani.
Kusikia kwa kenge ni paka atoke damu.

Nachoweza kusema ni kuwa Amani ni tunda la haki.

Viongozi wa kisiasa wakishachaguliwa wanasahau walio waweka madarakani ni wananchi na watakao watoa madarakani ni wananchi ikiwa hawataenda sawa na matakwa ya wananchi, either kwa kura au kwa damu.
 
Hakuna mtu Muoga kama Mtanzania. Hata mimi ni muoga sana. Kwanza natumia ID feki 🤣
Tena natumia jf nikiwa nimejificha kwenye uvungu wa kitanda 🤣🤣

Ushujaa wa wakenya ni next level
 
itoshe tu kusema uwoga wa watz ni wa kiwango cha lami.
 
Tanzania kufanana na Kenya bado, sijui labda patokee kiongozi awape sababu vijana na ujasiri.

Ukitaka kuamini nenda Nairobi zunguka siku nzima halafu njoo Dar zunguka siku nzima.

Utagundua yafuatayo:
1. Kenya wana njaa. Suala la chakula ni shughuli. Ile nchi wataftaji wasio na kitu kazi wanayo. Hapa dar chakula kipo, mihogo, vutumbua hujakaa sawa ndizi mishkaki, mara pweza na supu yake ndo maana watu bado hawapo tayari kufa kuipigania nchi. Kijana akipata elfu mbili tu anashiba anasuburi kesho. Kenya chakula ni gharama, ndo maana unaona serikali imeleta jambo la kuongeza gharama pamewaka. Hapa kwetu ukikaa sehemu wanapika ndizi na mishkaki ukaomba hata kusafisha vyombo upewe msosi unapata.

2. Suala la ardhi. Huku kwetu una M5 unapata ardhi karibu na jiji la DSM km 100 kutoka city centre tena unalipa kwa awamu? Nilikuwa Nairobi Kenya miezi kadhaa iliyopita kibiashara kule kama wazazi wako hawakushika ardhi imekula kwako, ardhi ni kipengele. Vijana hawana ardhi. Hapa kwetu ukitoka na laki tano yako ukaingia porini mikoani unapata ardhi ya kulima msimu mzima hata eka 5 ila si Kenya. Vijana kule hawana options kama huku ndo maana Serikali yao inapaswa kuwa makini. Wakijisahau tu lazima kuwake moto maana unakuwa umewasukumizia vijana ukutani kwa nia ya kuwadhuru na hawana option tena zaidi ya kupigana.

3. Historia yetu imebebwa na ujamaa na undugu, wazee wetu walikuwa watiifu mno kwa serikali. Sasa hivi angalau kidogo ndo hii gen mpya inahoji.
 
Wakenya walianza kulalamika mda sana kuhusu Zakayo kusafiri sana kutafuta mikopo lakini maisha yao bado ni magumu.

Vijana wako mtaani mambo yao ni magumu ajira hamna, mazingira ya biashara ni magumu, hawasikilizwi, wakilalamika viongozi wanajifanya viziwi.

Viongozi kutwa kucha kupitisha miswada ya kujilimbikizia mali, kujinunulia magari ya kifahari, kuiba mali za umma na kufanyia biashara zao.

Matokeo yake kila mtu analalamika mitaani bado wakakataa finance bill lakini viongozi wanawaona wao hawajui kitu wakaipitisha na hayo ni madhara yake.

Na Tanzania asilimia 100 yanayofanyika ni sawa na Kenya tofauti ni kuwa tuu Watanzania hawajaingia barabarani.
Kusikia kwa kenge ni paka atoke damu.

Nachoweza kusema ni kuwa Amani ni tunda la haki.

Viongozi wa kisiasa wakishachaguliwa wanasahau walio waweka madarakani ni wananchi na watakao watoa madarakani ni wananchi ikiwa hawataenda sawa na matakwa ya wananchi, either kwa kura au kwa damu.
Unamsema chalamila au ? Maana kile kiburi kwa wale watu wa karia kioo, mpka unaeza jiuliza alienda kutatua au kuchochea tatizo?
 
Majirani zetu are severely allergic to Bullshit, and easily triggered..
 
Wakenya walianza kulalamika mda sana kuhusu Zakayo kusafiri sana kutafuta mikopo lakini maisha yao bado ni magumu.

Vijana wako mtaani mambo yao ni magumu ajira hamna, mazingira ya biashara ni magumu, hawasikilizwi, wakilalamika viongozi wanajifanya viziwi.

Viongozi kutwa kucha kupitisha miswada ya kujilimbikizia mali, kujinunulia magari ya kifahari, kuiba mali za umma na kufanyia biashara zao.

Matokeo yake kila mtu analalamika mitaani bado wakakataa finance bill lakini viongozi wanawaona wao hawajui kitu wakaipitisha na hayo ni madhara yake.

Na Tanzania asilimia 100 yanayofanyika ni sawa na Kenya tofauti ni kuwa tuu Watanzania hawajaingia barabarani.
Kusikia kwa kenge ni paka atoke damu.

Nachoweza kusema ni kuwa Amani ni tunda la haki.

Viongozi wa kisiasa wakishachaguliwa wanasahau walio waweka madarakani ni wananchi na watakao watoa madarakani ni wananchi ikiwa hawataenda sawa na matakwa ya wananchi, either kwa kura au kwa damu.
shida ya viongozi wa afrika ndiyo hiyo.unajifanya mbabe na wakati huna pa kwenda kuiba mali ili uwahudumie wananchi wako.wajifunze kwa PK wa NCHI jirani.baada ya kutoka kwenye ile genocide eti leo haiko kwenye list ya nchi maskini za africa.kumbe jamaa mjanja anaende kwa nchi jirani anapora mali na kuja kuwahudumia wananchi wake.wataacha kumwabudu kweli?
 
Tanzania hatuna njaa kama Kenya,,Mfumo wetu wa elimu,ulinzi na usalama pamoja na katiba yetu,malezi yetu haviruhusu umavimavi.Katiba ya Kenya ni copy and paste kutoka USA, ya kwetu na ya Zimbabwe ni copy and paste from China.
 
Sijawahi kuona maandamano Africa yanayodhuru viongozi.
Wanaoumiaga mwishowe ni wananchi wa kawaida
 
Back
Top Bottom