Yanga 1-1 (7-6 penati) Geita Gold | Azam Sports Federation | Estadio de Bejamin Mkapa

Yanga 1-1 (7-6 penati) Geita Gold | Azam Sports Federation | Estadio de Bejamin Mkapa

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Azam Sports Federation utapigwa usiku huu ambapo Yanga atawakaribisha Geita Gold katika dimba la Benjamin Mkapa.

Kwa live updates tukutane hapa saa 1::00 usiku

=================

Mchezo umeanza na timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Dk ya 20: Geita wanacheza kwa kuvizia kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Dk ya 30: Geita Gold wanacheza vizuri na kufanikiwa kufanya mashambulizi kadhaa

Dk ya 40: Yanga wanaongeza kasi ya kushambulia lakini ulinzi wa Juma Nyosso na Kelvin Yondani unakuwa imara.

MAPUMZIKO

Kipindi cha pili kimeanza.

Dk ya 60: Yanga wanaonekana kuongeza presha ya mashambulizi.

Dk ya 70: Yondani anamfuta Mayele wanajibizana baada ya Mayele kumchezea faulo Yondani

Dk ya 75: Mayele anakosa bao baada ya shuti lake kumgonga mlinzi wa Geita na inakuwa kona.

Dk ya 80: Makambo ameingia, ametoka Mauya, mabadiliko upande wa Yanga.

Dk ya 83: Yanga wanafanya mashambulizi mawili makali ndani ya muda mfupi. Presha imeongezeka mchezoni.

Dk ya 86: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Geita wanapata bao. Mahadhi anaifungia Geita baada ya pasi nzuri walizocheza.

Dk ya 90: Yanga wanapata penati baada ya beki wa Geita kuushika mpira.


DK ya 90: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Yanga wanasawazisha kupitia kwa Djuma Shaban kwa penati.


Dakika 90 zimekamilika mwamuzi anapuliza filimbi.

Muda wa penati.

Yanga wanashinda kwa penati 7-6, hivyo wanafanikiwa kusonga Hatua ya Nusu Fainali.
 
Back
Top Bottom