Yanga ataishangaza dunia

Yanga ataishangaza dunia

MIMI NAJUA YANGA WATAPIGAA HATA WACHEZE UCHI.


BRO MSHANA NITAKUSHAMBILIA SANA BAADA YA MPIRA KUMALIZIKA.

Mara ya mwisho yanga ALIKULA
4-0
 
Pamoja na woga wa kafara la maji(mvua) kuna uwezekano mkubwa wa kumfunga mwarabu kwao na kuondoka na kombe la shirikisho kwa mara ya kwanza katika historia ya soka nchini

Yanga inawakilishwa na rangi ya kijani ambayo kiasili ni rangi inayowakilisha uhai, kiroho rangi ya kijani ni rangi yenye nguvu mno!
Kijani hakiwezi kusitawi bila maji, na maji hutokea kwa namna nyingi na mojawapo ni mvua! Ni maji ya mvua pekee ndio huleta ustawi wa kijani kwa ukubwa na kwa haraka na bila gharama!

Kafara la maji kwa yanga kutoka SIMBA huwa linafanikiwa kwakuwa SIMBA ni rangi nyekundu kiwakilishi cha moto! Kijani kwenye nyekundu hakina nguvu kabisa!
Kama Yanga hawajafanya kafara lolote la kumwaga damu leo gemu ni lao


Mark my words!

Sent using Jamii Forums mobile app
aminia mzee
 
Hahahaha tunakueshimu kaka mvua iyo iyo ndo iliwaua mbili taifa kwanini isingegoma hapo, yn kaka leo kilingeni pako yale matunguli yako yamekuongopea. All in all, njia pekee ya yanga kuchukua hili kombe ni kwa kuliiba tu. Mshana Jr
 
Wengi wao wanachezea timu za ufaransa naona
Kuwafunga ni kazi labda tutumie na ngumi
 
Yanga msimu huu hajawahi fungwa game mbili mfululizo
 
EPUKA MATAPELI
HUYU MGANGA PANZI NDO ALITUKOLEZA SISI UTOPOLO ETI KWAMBA KIPINDI KILE JEZI YETU ILIKUWA NA MIZIMU MINGI MPAKA SANAMU LA ASKARI WA POST NI MZIMU ETI AKASEMA JEZI YA YANGA(UTO) NI NZITO SANA KWAIYO WATAKUWA NA MSIMU MGUMU SANA CHA AJABU UTO TUKABEBA NDOO

KAMA HAITOSHI...HUYUHUYU SANGOMA AKASEMA JEZI YA YANGA(UTOPOLO) HII AWAY KIT NYEUSI INAMIZIMU YA GIZA NA TAKATAKA GANI SIJUI KWAIVO KILA WAKIIVAA WATAFUNGWA LAKINI IKAWA KINYUME CHAKE

OGOPA MATAPELI
UTO HATUTOBOI MWARABU ANATUBANDUA GOLI 7 KWA UCHACHE
 
Hii ndio raha ya soka...
Yaani tambo tu za mashabiki ni burudani tupu.

Leo Mshana Jr kawatabiria wana Yanga mema, viva Simba...!

😂😂😂
 
Mimi ni Simba damu...
Ila kama mfuatilia soka nilimwambia jamaa yangu wa Yanga kuwa watabeba ndoo... Atulie asubiri ila yeye sasa, kihoro kama chote.

Kesho asubuhi magazetini

YANGA YAMALIZA KAZI ALGERIA

YANGA YAUA

YANGA BINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO

YANGA YAFANYA MAAJABU AFRIKA

ALICHOFANYA YANGA HAKITASAHAULIKA

HAO NDIO YANGAAAAA!
 
Back
Top Bottom