Yanga epuka mpango wa kusajili washambuliaji dirisha dogo, walioko wanatosha kabisa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kuna wadau wanaotaka Yanga kuongeza washambuliaji dirisha dogo. Siungi mkono kwakuwa walioko wanatosha na kupitiliza. Timu ya Yanga Ina magoli mengi ya kufunga kuliko timu nyingine ya ligi hivi sasa kwenye ligi.

Kwenye mashindano ya CAF timu zote hata zile kubwa zenye washambuliaji Bora ikiwemo Pyramids ambayo Mayelle anachezea bado zinapata shida sana kupata magoli pia.

Tusiingie hasara ya kuvunja mikataba ya wachezaji dirisha dogo eti kwa sababu ya kutafuta strikers, sio kweli kabisa. Maana hata akina Baleke na yule wa bil 10 wa Al Ahly bado nae anakosa magoli; hafungi. Mzize, Musonda na Konkon wanatosha kabisa, wapewe muda TU.

Ni Mfumo TU wa Mwl Gamondi hautegemei washambuliaji pekee kufunga magoli. Kama ni wachezaji waongezwe wale wa namba 6, namba 7 kwa moloko na namba 11 kusaidia Nzenheli.

Kama mkimwacha kizembe Hafiz konkon na akichukuliwa na ihefu mtaona atakavyosumbua timu zote.
 
Musonda akipunguza sigara anaweza kuwa straika mzuri mbeleni.
Sio Yanga TU bali timu zote hakuna magoli, hivyo hatuwezi kuwalaumu sana Musonda, Mzize na konkon kuwa hawafungi. Na kama yupo striker ambae akililetwa Yanga atafunga sana basi atakuwa ghali mno mno mno maana hata Al Ahly, pyramids na wydad watamtaka kwa dau lolote lile ambalo hatutakuwa nalo sisi kushindana nao. Tusiingie kwenye mtego.
 
Viongozi wanapokea taarifa ya kocha na wasaidizi wake kabla ya kufanya usajili na sio vinginevyo .
 
Hakuna kocha asiyetamani kupewa mchezaji kama Halaand, mbape, Ronaldo au Benzema kwenye kikosi chake. Je, Gamondi akitawataka wachezaji hao mtampatia? Siku zote lazima tujikumbushe kila wakati kuwa wachezaji wazuri sana wanakwenda ligi za Ulaya na wazuri wa wastani kama Mayelle wanakwenda ligi za kaskazini mwa Afrika, hawaji ligi zetu hizi. Tunaweza kufanya sisi ni kuchukuwa wachezaji wasiokuwa na majina tuwapike ili wakiiva tuwatumie na wakiiva kabisa tuwauze tupate pesa kabla hawajaondoka kama wachezaji huru., Hatuna namna yoyote Ile ya kuwazuia wasiondoke.
 
Zamani wakati navuta sigara nilikaa chini nikajiuliza kwa nini napata hamu ya kula moto nilipokosa majibu nikaacha sikuhizi napata hamu ya kula chakula.
Hahaha!
 
Viongozi wanapokea taarifa ya kocha na wasaidizi wake kabla ya kufanya usajili na sio vinginevyo .
Kwa bei zetu sisi hakuna striker mzuri tutakaempata anaewazidi ubora Mzize, Musonda na Konkon. Ni walewale TU wanazidiana kidogo sana kutokana na matumizi na mfumo wa kocha kwenye mechi husika.
 
Zamani wakati navuta sigara nilikaa chini nikajiuliza kwa nini napata hamu ya kula moto nilipokosa majibu nikaacha sikuhizi napata hamu ya kula chakula.
Utakuwa umenenepa mkuu
 
Kwa bei zetu sisi hakuna striker mzuri tutakaempata anaewazidi ubora Mzize, Musonda na Konkon. Ni walewale TU wanazidiana kidogo sana kutokana na matumizi na mfumo wa kocha kwenye mechi husika.
Tatizo Linaloikumba yanga na timu nyingine Tanzania vile vipaji vya kina Edibily , Ngasa nk siku hizi havipo .
 
Sema tu kocha Miguel Garmond naye siyo mtu wa kucheza na mind games! Kwenye mechi na Medeama, Hafiz Konkoni alitakiwa kuanza. Maana alikuwa yuko nyumbani. Hivyo asingekubali kucheza chini ya kiwango.

Ila kwa bahati mbaya ndiyo hivyo tena! Alimuingiza dakika ya 85 ya mchezo, na bado madhara yake yalikuwa ni makubwa kuliko hata yale ya Musonda na Mzize waliocheza kwa vipindi vyote viwili vya mchezo.

Huyu mchezaji alitakiwa apewe mechi za kutosha, ndiyo ingekuwa rahisi kumfanyia tathmini. Binafsi siamini kama ni mshambuliaji mbaya.
 
Sio kweli, hata hao hawajawahi kuleta vikombe vya CAF nchini Wala kwenye clubs zao walizokuwa wanazichezea. Yanga imeingia makundi kwa mara ya kwanza mwaka baada ya kupita 25 years, hao akina edibily walikuwa wapi?
 
Nimesoma nikatafakari je huyu ana nia nzuri kweli na Yanga? Mpira ni mchezo wa wazi, Yanga ina uhitaji wa mshambuliaji aliyekamilika anayejua kujiposition na kulijua lango.
Mshambuliaji huyo (gold standard) ni kama yupi? anachezea timu gani Sasa hivi? Je, hiyo timu yake imeingia makundi CAF champions? Kama imeingia imeshinda mechi ngapi na yeye amefunga magoli mangapi kati ya hayo?.
 
Kuna wadau wanaotaka Yanga kuongeza washambuliaji dirisha dogo. Siungi mkono kwakuwa walioko wanatosha na kupitiliza. Timu ya Yanga Ina magoli mengi ya kufunga kuliko timu nyingine ya ligi hivi sasa kwenye ligi.

Kwenye mashindano ya CAF timu zote hata zile kubwa zenye washambuliaji Bora ikiwemo Pyramids ambayo Mayelle anachezea bado zinapata shida sana kupata magoli pia.

Tusiingie hasara ya kuvunja mikataba ya wachezaji dirisha dogo eti kwa sababu ya kutafuta strikers, sio kweli kabisa. Maana hata akina Baleke na yule wa bil 10 wa Al Ahly bado nae anakosa magoli; hafungi. Mzize, Musonda na Konkon wanatosha kabisa, wapewe muda TU.

Ni Mfumo TU wa Mwl Gamondi hautegemei washambuliaji pekee kufunga magoli. Kama ni wachezaji waongezwe wale wa namba 6, namba 7 kwa moloko na namba 11 kusaidia Nzenheli.

Kama mkimwacha kizembe Hafiz konkon na akichukuliwa na ihefu mtaona atakavyosumbua timu zote.
Konkoni juzi kule Ghana alikuwa wa moto sana nilitamani angeliingia dakika ya70 japokuwa mechi za caf siyo za kuthubutu kujaribu wachezaji inaweza kula kwako
 
Sio Yanga TU bali timu zote hakuna magoli, hivyo hatuwezi kuwalaumu sana Musonda, Mzize na konkon kuwa hawafungi. Na kama yupo striker ambae akililetwa Yanga atafunga sana basi atakuwa ghali mno mno mno maana hata Al Ahly, pyramids na wydad watamtaka kwa dau lolote lile ambalo hatutakuwa nalo sisi kushindana nao. Tusiingie kwenye mtego.
Unaposema sio Yanga tu ni timu zote kubwa Afrika nakushangaa, Yanga ana point mbili na goli mbili, ni timu gani kubwa Afrika ambayo ina goli mbili na point mbili?
 
Sema tu kocha Miguel Garmond naye siyo mtu wa kucheza na mind games! Kwenye mechi na Medeama, Hafiz Konkoni alitakiwa kuanza. Maana alikuwa yuko nyumbani. Hivyo asingekubali kucheza chini ya kiwango.

Ila kwa bahati mbaya ndiyo hivyo tena! Alimuingiza dakika ya 85 ya mchezo, na bado madhara yake yalikuwa ni makubwa kuliko hata yale ya Musonda na Mzize waliocheza kwa vipindi vyote viwili vya mchezo.

Huyu mchezaji alitakiwa apewe mechi za kutosha, ndiyo ingekuwa rahisi kumfanyia tathmini. Binafsi siamini kama ni mshambuliaji mbaya.
Labda kwenye mazoezi hakuonyesha yupo vizuri
 
Back
Top Bottom