Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Klabu ya Yanga imesema kuwa adhabu ya Ofisa Habari wao, Haji Manara kufungiwa miaka miwili kujihusisha na soka na faini ya Tsh. Milioni 20 siyo ya haki na adhabu ni kubwa.
Yanga wametoa tamko na kueleza kuwa inamuunga mkono Manara katika kudai haki yake kwenye vyombo vya juu zaidi vya kimamlaka. Adhabu ya Afisa huyo imetangazwa leo Julai 21, 2022 na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania.