Club ya Yanga imetoa tamko lake kuhusu hukumu aliyopewa Msemaji wake Haji Manara na kusema hajatendewa haki hivyo inamuunga mkono katika kudai haki yake kwenye vyombo vya juu zaidi vya kimamlaka.
“Uongozi wa Club umepokea kwa masikitiko makubwa uamuzi wa Kamati ya maadili ya TFF, adhabu hii inakwenda kuathiri moja kwa moja mchango wa Ndugu Haji Manara katika maendeleo ya mpira wa miguu kwenye Club yake, Ligi Kuu Znz, Ligi Kuu Tanzania bara na Nchi jirani (Burundi) ambazo amezihudumu” imeeleza taarifa ya Yanga.
My take: Karia wewe ni mtu mdogo sana, nazidi kumsihi ndugu Majaliwa aliye kuweka hapo kuwa akupigie simu kukujulisha kuwa wewe ni mdogo sana. Namkumbusha ndugu Majaliwa kuwa alikupigia simu wewe baada ya yeye kupokea simu toka sehemu nyingine. Atafakari.