Yanga waachane na hii formation ya 4-2-3-1 kwani viungo wao hawana uwezo wa ku-press ili kutengeneza nafasi nyingi kwa mshambuliaji wao kuweza kufunga labda wacheze 4-3-3 ambayo angalau ni mfumo unaoweza kuwafanya washambulie zaidi.
Badala yake mshambuliaji mara nyingi anabaki kisiwani huku hakiwa hawezi kupata mipira. Yanga wanatakiwa wapate utility mid-fielders wenye uwezo wa kumiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga jambo ambalo ilikosekana kwenye mechi yao na Simba.
Pia naona kama kocha pia bado hayuko vizuri kimbinu, huwezi kuweka timu ijihami wakati hata goli bado hujafunga huku pia hauna mpango wa kufanya devastating counter attacks na badala yake unajihami kwa shabaha ya kutafuta sare, huu mkakati ni wa hovyo sana.
Kama Yanga wasipofanyia kazi hilo basi hawawezi kufika mbali kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika.