Yanga hii ya Lwandamina, hapana

four eyes

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2017
Posts
905
Reaction score
1,408
Dah! Kila ninapo itazama timu yangu ikicheza nakosa raha kabisa, sioni timu iliyosifika kwa lile soka tamu ya kampa kampa tena. Timu ipoipo tu sasa hivi na inacheza mradi inacheza

Najua viongozi wanaliona hili lakini wanashindwa kumtimua Lwandamina sababu timu haina pesa Sasa hivi na kuvunja nae mkataba ni gharama kubwa sababu itabidi wamlipe kwahiyo wameamua kubaki wakitizama tu.

Kilichobaki ni kusubiri tu mpaka timu ishuke daraja sasa maana ndiko tunakoelekea, wachezaji hata morali hawana tena japo wapo wachache wanaojitahidi kujituma lakini Mipango hamna kabisa.

Ukihoji unaambiwa story za kwamba sijui timu ilikuwa ikiwategemea kina Msuva kushambulia tokea pembeni. Sasa hivi hawapo kocha bado anatafuta mfumo, atautafuta mpaka mwisho wa ligi kwa staili hii.
 
ni kweli yanga imebalika sana !
naumia kuona inacheza bila matumaini ya ushindi...
ila tatizo si kocha pekee ila hata hata wachezaji hawana uwezo mkubwa...
mfano kamusoko akiwa nje team inayumba sana..
lakini tuamini tu [HASHTAG]#YANGA[/HASHTAG] [HASHTAG]#MBELE[/HASHTAG] [HASHTAG]#DAIMA[/HASHTAG]
 
Tatizo ni mlimtegemea sana Manji, msitafute mchawi mwingine bali ni uongozi kujisahau na kumtegemea Manji, yaani Manji alikuwa akisema anaachia ngazi mnaenda kumpigia magoti! Sisi Simba tumeshazoea shida, raha ikija poa tu ila barabara zote tunapita fresh tu!
 
Hahaha! Sawa ni mtazamo wa utani wa jadi lakini mpira ni mpira,porojo ni porojo tu kama manara na team yenu
 
Ukweli kama huu wapo akina moniccca na demigod hawataki kuusikia kabisahttps://www.jamiiforums.com/members/demigod.266869/
 
Ukweli kama huu wapo akina moniccca na demigod hawataki kuusikia kabisa

Kuhusu lengo lamleta uzi

Kwanza kabisa nimesoma uzi na kushindwa kabisa kuelewa nini hasa lengo/maudhui ya mleta mada. Huwa ni vigumu sana kuchangia uzi zilizobeba hisia kuliko zile zenye hoja.

Nilichokiona hapo juu ni hisia za mwanajangwani (ila sina uhakika kama ni mwanajangwani).

Ukijaribu kusoma tena kwa mara ya tatu mpaka 5 kichwa kinajaa kizunguzungu na unaanza kuhisi kama unachanganyikiwa, hii yote ni kutaka kulazimisha akili kuelewa jambo ambalo hata mleta mada ameshindwa namna ya kulileta.

Nikijaribu kujibu/kudadavua hisia zamleta uzi "Hivyohivyo"

Bw four eyes anaonekana kujawa na hofu + wasiwasi kuhusu kiwango cha timu yake na anaonekana kumtupia Lawama mwalimu GL na lawama zaidi akizielekeza kwa Utawala wa Klabu.

Wakati huo huo anataka utawala uvunje mkataba na GL kwa sababu haridhishwi na uchezaji wa timu, na anajua wazi kuwa kuvunja mkataba ni gharama kubwa na suala la ajabu mleta mada mwenyewe anajua kuwa hali ya uchumi wa klabu sio sawa. (Kwa ujumla hapa sijaelewa lengo la mleta mada).

Cha kushangaza mleta mada anasema/anafikiri kuwa ipo siku Klabu itashuka daraja. (hapa kidogo nilicheka kwa kicheko cha Sokwe pori, ndio maana nikasema sina uhakika kama ni mwanajangwani).

Kuhusu "Haya ya mwisho": Mleta mada anadai alihoji, sasa sijui alihoji viongozi wa yanga au ni wenzake wa vijiweni. Kama alihoji wenzake wa vijiweni hapo sina la kujibu ila kama amehoji viongozi wa benchi la ufundi na akapewa jibu hilo basi huenda walimpuuzia na kumpa jibu la namna hiyo.

"Hitimisho"

Kuna shabiki na Mwanachama, sasa sijui yeye yuko upande gani? Kama uko upande ambao hauna hata nafasi ya kutolea mchango wa kifedha klabu yako, basi huna haki ya kushauri nini kifanyike klabuni.

Unadai GL avunjiwe mkataba, Je fedha za kuvunja mkataba wake zinatoka wapi? (Mwambie mleta uzi ajibu hili swali).

Ni sawa na mwanaume anamuacha mke wake bila fedha asubuhi lakini akirudi nyumbani jioni anataka akute Wali+Mayai+Matunda+Mboga za majani nk
 
DaaaaH umeongea point Sana jamaaa ujue watu wengi sasa wanaendeshwa na mihemko wanashindwa kutambua kuwa mambo yanawakat.. huwez kuwa bora kipnd chote ni lazma tujifunze kuwa wavumilivu kama kocha mbovu itajulikana tu hakuna haja ya kuwa na jazba kwasabab ya mechi mbili za mwanzo
 
Hao wanaotumia sababu ya kutowepo msuva hawana akili timamu.

Tangu Lwandamina akabidhiwe timu , timu imekuwa mbovu sana na huyo Msuva pia alikuwepo .

Na mbaya zaidi tulimaliza msimu tukiwa na magoli 57 tu kutoka 72 kipindi cha Pluijm.
 

Hawezi kuwa Yanga huyo - iwe shabiki au mwanachama. Two games kwenye ligi anaongea sana. Majeruhi ya Tambwe, Chirwa na hata Ngoma msimu uliopita hayaoni hata kidogo. Mpira hauko hivyo

Kila msimu kuna timu huanza na nguvu za soda na huanza kuisha katikati ya msimu. Yanga imekuwa na tendancy ya kuanza taratibu na ku pick kadri muda unavyoenda. Yeye hajui yote hayo.

Tusipoteze muda na matopeni wanaojifanya Yanga.
 
Mkuu mleta mada anaweza asiwe katika nafasi ya kuichangia timu kifedha moja kwa moja ila akawa na mchango usio Wa moja kwa moja kupitia kulipa viingilio uwanjani. Unadhani wale mashabiki wanaojaa uwanjani Yanga inapocheza wote wana kadi za uanachama? Ukifuatilia utagundua robo au nusu tu ya wale washabiki ndio wenye kadi. Mkuu ulichokisema ni sawa na kwamba kama raia hana kadi ya chama cha siasa basi asijihangaishe na masuala ya kupiga kura. Mleta mada ana haki ya kutoa maoni juu ya akionacho na kiukweli hata Mimi huwa sielewi viongozi Wa Yanga walimleta Lwandamina kwa vigezo gani. Kwa kifupi tangu yule Mwalimu aichukue timu inacheza vibaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulijiuliza ni uwanja gani wanacheza? Hali ya baridi ya Njombe uliitafakari? Siku ya Simba na Yanga ulifurahi ama hukufurahi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa najiandaa kumjibu huyu punguani lakini Mara tu nilipoona jibu lako nimetosheka kwamba umenijibia kiasi cha kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…