Yanga hii ya Lwandamina, hapana

Yanga hii ya Lwandamina, hapana

Hawezi kuwa Yanga huyo - iwe shabiki au mwanachama. Two games kwenye ligi anaongea sana. Majeruhi ya Tambwe, Chirwa na hata Ngoma msimu uliopita hayaoni hata kidogo. Mpira hauko hivyo

Kila msimu kuna timu huanza na nguvu za soda na huanza kuisha katikati ya msimu. Yanga imekuwa na tendancy ya kuanza taratibu na ku pick kadri muda unavyoenda. Yeye hajui yote hayo.

Tusipoteze muda na matopeni wanaojifanya Yanga.
Timu haikuanza kudorora msimu huu tu,bali tangu alipifika lwandamina soka ikavurugika kabisa,tulichukua ubingwa kwa sababu tu ya mistake za simba na matokeo mazuri aliyoanza nayo pluijm.nyie ndio mashabiki ambao ukichunguza ni mashabiki wa arsenal pia,mashabiki wenye subira iliyopitiliza mpaka pale timu ikishadhalilika kiasi cha kupitiliza ndio mtastuka labda.
 
Hawezi kuwa Yanga huyo - iwe shabiki au mwanachama. Two games kwenye ligi anaongea sana. Majeruhi ya Tambwe, Chirwa na hata Ngoma msimu uliopita hayaoni hata kidogo. Mpira hauko hivyo

Kila msimu kuna timu huanza na nguvu za soda na huanza kuisha katikati ya msimu. Yanga imekuwa na tendancy ya kuanza taratibu na ku pick kadri muda unavyoenda. Yeye hajui yote hayo.

Tusipoteze muda na matopeni wanaojifanya Yanga.
Gonganeni wenyewe huku huku acheni kuhusisha timu fulani. Aliyekuwa akinunua mechi hayupo, unadhani timu itakuwa poa hapo?
 
Kuhusu lengo lamleta uzi

Kwanza kabisa nimesoma uzi na kushindwa kabisa kuelewa nini hasa lengo/maudhui ya mleta mada. Huwa ni vigumu sana kuchangia uzi zilizobeba hisia kuliko zile zenye hoja.

Nilichokiona hapo juu ni hisia za mwanajangwani (ila sina uhakika kama ni mwanajangwani).

Ukijaribu kusoma tena kwa mara ya tatu mpaka 5 kichwa kinajaa kizunguzungu na unaanza kuhisi kama unachanganyikiwa, hii yote ni kutaka kulazimisha akili kuelewa jambo ambalo hata mleta mada ameshindwa namna ya kulileta.

Nikijaribu kujibu/kudadavua hisia zamleta uzi "Hivyohivyo"

Bw four eyes anaonekana kujawa na hofu + wasiwasi kuhusu kiwango cha timu yake na anaonekana kumtupia Lawama mwalimu GL na lawama zaidi akizielekeza kwa Utawala wa Klabu.

Wakati huo huo anataka utawala uvunje mkataba na GL kwa sababu haridhishwi na uchezaji wa timu, na anajua wazi kuwa kuvunja mkataba ni gharama kubwa na suala la ajabu mleta mada mwenyewe anajua kuwa hali ya uchumi wa klabu sio sawa. (Kwa ujumla hapa sijaelewa lengo la mleta mada).

Cha kushangaza mleta mada anasema/anafikiri kuwa ipo siku Klabu itashuka daraja. (hapa kidogo nilicheka kwa kicheko cha Sokwe pori, ndio maana nikasema sina uhakika kama ni mwanajangwani).

Kuhusu "Haya ya mwisho": Mleta mada anadai alihoji, sasa sijui alihoji viongozi wa yanga au ni wenzake wa vijiweni. Kama alihoji wenzake wa vijiweni hapo sina la kujibu ila kama amehoji viongozi wa benchi la ufundi na akapewa jibu hilo basi huenda walimpuuzia na kumpa jibu la namna hiyo.

"Hitimisho"

Kuna shabiki na Mwanachama, sasa sijui yeye yuko upande gani? Kama uko upande ambao hauna hata nafasi ya kutolea mchango wa kifedha klabu yako, basi huna haki ya kushauri nini kifanyike klabuni.

Unadai GL avunjiwe mkataba, Je fedha za kuvunja mkataba wake zinatoka wapi? (Mwambie mleta uzi ajibu hili swali).

Ni sawa na mwanaume anamuacha mke wake bila fedha asubuhi lakini akirudi nyumbani jioni anataka akute Wali+Mayai+Matunda+Mboga za majani nk

Kwa kuwa tayar Kuna mtu amekujibu kwa niaba yangu sitahangaika sana nawewe ila umeongea mengi na ukasahau kueleweka wewe pia sababu hata mm sijaelewa lengo LA comment yako,nilitegemea kama nilichokiandika si sahihi basi ungekipinga kwa hoja za ufundi maana unaonekana ni mpenz sana WA hoja za kiufundi,

ungedadavua kiufundi jinsi gani nakosea kumshutumu lwandamina na kutuaminisha ubora wake huku ukitoa sababu za performance isiyolidhisha,

naona umejipa tu kaz ya kuchambua nilichoandika Aya kwa Aya Bila kuleta utofauti wowote Kati yangu niliyeandika kisichoeleweka nawewe mjuzi zaidi.

kimsingi nimekuweka ktk group lile lile LA mashabiki vipofu ambao wanazidiwa na huba na mahaba kiasi cha kushindwa kuuona hata ukweli,

Sina Shaka wewe ni mshabiki wa arsenal ndio imebarikiwa mashabiki wavumilivu ktk kiwango kilichopitiliza.umefika mahala umejipa Hati miliki ya club hii ya wote ukihoji nimepata wapi haki ya kuhoji matokeo na mwenendo ikiwa sichangii,

hoja hiyo imeshajibiwa na mtangulizi wangu
 
Mlete mada sio punguani kama mnavyolazimisha aonekane. Ana hoja, pengine ameshindwa kuijenga kisomi,lakini kama sio mnazi you can understand what he was trying to write.

Kiukweli niliangalia mechi ya jana, niliishiwa nguvu, itanichukua muda kuangalia tena mechi za Yanga kwenye TV au kwenda Taifa. Nilichokiona, kiwango cha mpira kilichoonyeshwa na timu ya Yanga ni cha chini, Utafikiri watu wameokotwa kwa makonda/Kolomije na kuletwa mjini.

Kama timu inataka kupata backing wa mashabiki, basi icheze soka la kuvutia sio Rugby.
 
KOCHA WA SIMBA PIA BOMU TU

Na Baraka Mbolembole

KATIKA uchambuzi wa kwenye makaratasi, Simba SC walionekana kuwa na kikosi cha ‘kutisha’ na tena walikuwa na wachezaji wengi ‘maarufu’ kuliko Azam FC, lakini hayo hayakuweza kumsaidia kitu kocha wa timu hiyo Mcameroon, Joseph Omog kufikia ‘matarajio.’ Naamini hilo baada ya mchezo kumalizika kwa suluhu-tasa Jumamosi iliyopita.

‘Ubutu’ wa washambuliaji wa omog haukuanza leo

Kuna mengi yamebadilika katika safu ya mashambulizi ya Simba tangu kuondoka kwa Mrundi, Amis Tambwe mwezi Disemba, 2014. Elius Maguli na Emmanuel Okwi walisajiliwa katikati ya mwaka 2014 mara baada ya uongozi wa Evance Aveva na Geofrey Nyange Kaburu walipoingia madarakani.

Maguli alikuwa ametoka kufanya vizuri katika kikosi cha Ruvu Shooting, na Okwi alisajiliwa akitokea Yanga SC ambako alicheza kwa miezi sita msimu wa 2013/14. Usajili huu ‘niliuita usio wa kimpira’ kwa sababu tayari Simba ilikuwa na vijana kama Edward Christopher, Ibrahim Ajib na Mbaraka Yusuph huku Tambwe akitoka kufunga magoli 19 na kushinda tuzo ya ufungaji bora msimu wa 2013/14.

Maguli alifeli Simba kwa maana alifunga magoli manne tu, huku Okwi akifunga 12 kwa msimu mzima na Tambwe ambaye aliondoka wakati wa usajili wa dirisha dogo na kujiunga Yanga akimaliza msimu akiwa na magoli 15, huku mawili tu akifunga akiwa Simba.

‘Angaika angaika’ ya usajili ikifanikiwa kupata suluhisho katika safu ya mashambulizi ya Simba baada ya kumsaini Mganda, Hamis Kizza, lakini jambo la ajabu Kizza alikja kuachwa mwishoni mwa msimu licha ya kufunga magoli 23 katika ligi (magoli ( 19) na michuano ya FA (magoli manne)

Kiiza aliachwa kwa sababu za ‘kufikirika’ kuwa ‘mtu wa Yanga’ na mashabiki wakasapoti hilo bila kutazama idadi ya magoli yake aliyofunga. Ujio wa Mrundi, Laudit Mavugo katikati ya mwaka 2015 ulimuondoa Kizza,huku ujio wa Kizza Julai, 2015 ukimuondoa Okwi, na ujio wa Okwi ukimuondoa Tambwe.

Naweza kusema bila shaka yoyote kuwa katika kipindi cha misimu hii minne Simba ndiyo timu iliyotumia kiasi kikubwa sana cha pesa kusajili washambuliaji lakini imekuwa ‘butu’ kuliko safu za mashambulizi za Yanga na Azam FC kwa misimu hii ya karibuni.

Na yote haya wakati mwingine yanachangiwa na ‘usajili wa kina Mr.Kazinyingi’ ndiyo maana licha ya ujio wa majina makubwa na wafungaji waliofanya vizuri katika timu nyingine ‘Msimbazi hapo’ pamekuwa ‘chungu cha moto.’

Mavugo nilimuhurumia msimu uliopita alipoangaika kutimiza ahadi yake ya kufunga magoli 30 katika msimu mmoja wa VPL. Maskini aliishia kufunga magoli nane tu na sasa amekuwa ‘mkosa magoli hatari’ wa Simba na kuwachosha hadi mashabiki wa timu yake ambao walimlinda sana na kusema ‘apewe muda zaidi.’

Upande sutaki kuona Mavugo akipewa muda bali tujiulize kwa nini washambuliaji waliofanikiwa zaidi Simba ndani ya misimu minne iliyopita hawakupewa muda, na tuwape muda ‘wachovu’ waliosajiliwa kwa matakwa Fulani Fulani tu ya watu?

Sioni kipya kutoka kwa Mrundi huyu, na itakuwa mafanikio sana kwake kama atafunga magoli nane msimu huu kama tu timu hiyo itaendelea kunolewa na Omog ambaye naweza kusema alikubali usajili ambao ‘hawezi kuufanya utoe matunda’ kwa timu yake.

Kukubali rundo la washambuliaji wenye majina makubwa nchini si kigezo cha timu nyingine kupoteza mechi vs Simba. Labda kama Omog alikubali ujio wa Okwi, Mghana, Gyan, John Bocco, Mavugo, Juma Liuzio kwa kuamini majina yake yatampa ushindi katika mechi.

Lakini kama alihitaji ushindi baada ya washambualiaji wake kufunga hakupaswa kuwa na washambuliaji wote hao wakati alishuhudia viungo wake Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim na Muzamiru Yassin wakifunga zaidi ya magoli 25 msimu uliopita. Katika hili hawezi kukwepa lawama, kamani usajili wake watu wanataka kuona matunda haraka kwa maana walishamsubiri msimu uliopita. Omog amejipa mzigo mkubwa sana na ataangaika sana kupata pacha ya mashambulizi hadi atakapofukuzwa.

Angeamua tu kuchagua washambuliaji watatu. Sasa tangu wakati wa maandalizi ya msimu Simba hii ‘mnayosema ya kutisha’ imekuwa na tatizo kubwa la ufungaji, lakini linaweza kutatulika ikiwa wachezaji wa kikosi hicho watapata kocha mpya haraka kwa sababu mbinu za Omog haziwezi kuwafanya wafungaji wafunge, labda siku kikosi kikipangwa na msaidizi wake Mganda, Jackson Mayanja ambaye yeye hupendelea soka la kushambulia na kuzuia kwa kutegemea umiliki wa mpira.

Njia mbadala ya simba kupata magoli

Vikosi vya Omog pale Azam FC havikuwa na makali katika ufungaji, msimu wake wa kwanza Simba timu ilikuwa butu kiufungaji. Tatizo hapa ni yeye na mbinu zake. Kwa aina ya wachezaji alionao Omog anapaswa kushikilia zaidi mfumo wa 4-3-2, na kuutumia mfumo wa 4-4-2 wakati anapohotaji kuwatumia washambuliaji wawili.

Katika 4-3-3 hapa, haitaji kuwa na mfungaji asilia lakini atahitaji wachezaji kama Okwi, Kichuya, Mohamed Ibrahim ambao wana ‘unyumbulifu’ mkubwa ambao unaweza kupasua ngome ngumu kama ile waliyokutana vs Azam FC Jumamosi iliyopita ama Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii. Wote hawa wana shabaha, wanapenda kufunga magoli na kupiga pasi zisizotarajiwa.

Mara ya mwisho niliiona Simba kali wakati Okwi,Haruna Moshi ‘Boban’ wakicheza katika 4-3-3 wakimzunguka Mzambia Felix Sunzu. Nyuma yao kulikuwa na viungo wachezesha timu wenye ubunifu mkubwa marehemu, Patrick Mafisango, Mwinyi Kazimito na SalumMachaku.

Najua, Omog anahofia kumuweka benchi Okwi,na amekuwa akimuamini sana Kichuya ndiyomaana Mo Ibra amekuwa akikosa nafasi ya kuanza, lakini angetambua umuhimu wa Mo Ibra katu hasingeweza kumuweka benchi mchezaji huyo ambaye alimnyanyua sana msimu uliopita.

Jonas Mkude ameshapoteza nafasi yake kwa Mghana, James Kotei na mambo yanakwenda, kumuacha nje ya kikosi cha kuanza mchezo Muzamiru ni sawa na kuinyima ushindi timu yako, na si rahisi kuona Mnyarwanda, Haruna Niyonzima akikosa nafasi ya kuanza kikosi anapokuwa fiti kimwili na kiakili.

Kotei, Haruna, Muzamiru hapa tayari Omog amefanikiwa katika 4-3-3, lakini bado ameshindwa jinsi ya kupanga watatu watatu wa mbele katika mashambulizi, na hofu ya mapokeo ya mashabiki ndiyo inampa shaka ya kupanga vizuri safu ya mashambulizi kwa kudhani atalaumiwa sana ikiwa wachezaji Fulani watashindwa kuanzishwa.

Ningekuwa katika nafasi yake ningewapanga, Okwi, Kichuya na Mo Ibra na kama ningetumia mfumo wa 4-4-2 ningewapanga Kotei, Haruna, Muzamiru na Mo Ibra huku Bocco na Okwi, ama Bocco na Liuzio, ama Okwina Liuzio, nap engine Mavugo na Okwi.

Mo Ibrahim atamfukuzisha kazi haraka Omog

Endapo Simba itashindwa kufunga walau magoli manne katika michezo yake mitano ijayo si ajabu Omog akawa nje ya kikosi baada ya mchezo vs Yanga . kabla ya kuwavaa mahasimu wao hao Simba itacheza na Mwadu FC katika uwanja wa Uhuru, itaenda nje ya Dar es Salaam kwa mara ya kwanza kucheza na Mbao FC Septemba 21, watapia Sinyanga kucheza na Stand United kasha kurejea Dar kucheza na Mtibwa Sugar FC, Mjombe FC na Yanga.

Ni ratiba nyepesi kwa timu inayopangwa vizuri kama Simba lakini kwa aina ya mchezo wa kikosi hicho chini ya Omog ratiba hiyo itakuwa ngumu na huenda ‘ikamsomba’mtu kama mafuriko. Omog akubali kuwa Mo Ibra hapaswi kuwekwa benchi anapokuwa timamu kimwili na kiakili. Akiendelea kuwakumbatia mastaa wasio na msaada kifungaji mashabiki hao hao anao wahofu wataanzisha kelele za kushindwa kwake.

Mo Ibra anacheza upande wa kushoto vizuri sana, anajua kushambulia akitokea kulia na mpigaji wa pasi bora za mwisho akitokea katikati ya uwanja. Sawa Ndemla anahitaji kusuburi, lakini ni hatari kufanya hivyo kwa wakati mmoja ukimuhisha na Mo Ibra.

Huyu anaweza kmtete kocha asiye na mbinu bora za ufungaji pale Simba, lakini ni huyu huyu Mo Ibra ambaye atamuondoa haraka Omog pale Simba. Mpe nafasi kijana huyu atengeneze utulivu katika ufungaji.
 
Ila kiukweli Yanga mwaka huu ni majanga matupu,jaribu kuangalia hizi mechi mbili walizocheza ni hamna kitu.Mpira haueleweki kabisa.Kama ile mechi na Njombe mji tumshukuru kipa,vinginevyo tulikuwa tunafungwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawezi kuwa Yanga huyo - iwe shabiki au mwanachama. Two games kwenye ligi anaongea sana. Majeruhi ya Tambwe, Chirwa na hata Ngoma msimu uliopita hayaoni hata kidogo. Mpira hauko hivyo

Kila msimu kuna timu huanza na nguvu za soda na huanza kuisha katikati ya msimu. Yanga imekuwa na tendancy ya kuanza taratibu na ku pick kadri muda unavyoenda. Yeye hajui yote hayo.

Tusipoteze muda na matopeni wanaojifanya Yanga.


Ni shida aisee!

Jamaa anasema amezoea kuona Yanga ikidondosha kipigo cha mbwa mwitu, na kwamba sasa halioni hilo. Anashindwa kujua kuwa kadiri ligi inavyoingia msimu mpya ndio inakuwa ngumu zaidi ya msimu uliopita..

Alafu anaonekana sio mwanamichezo kabisa, yeye anataka Yanga mua wote tu iwe inashinda na kucheza soka safi, anasahau kuwa huu ni mpira wa miguu kuna matokeo ambayo yanatakiwa yakubalike for the sake of the game.
 
Back
Top Bottom