Yanga hoi kwa Azam, yasambaratishwa magoli manne bila majibu

Yanga hoi kwa Azam, yasambaratishwa magoli manne bila majibu

Wamepatwa na wauza Ice cream na vitafunwa.

Hakika kila mbabe ana mwamba wake, hivi ninavyoandika hii Dk 45 za first half zimemalizika na kwa kweli Azam ndio waliokuwa juu kwa kila kitu na kila idara.

Kumbe Yanga ni timu mbovu kiasi hiki?

Kama Azam wangekuwa makini mpaka dk hii wangekuwa wako mbele kwa mabao matano, ngoja tuendelee kuangalia .

Kamusoko hoi kwa Salum Abubakar!
========

Yanga imekubali kipigo cha magoli manne bila majibu kutoka kwa Azam FC mjini Zanzibar katika michuano ya mapinduzi inayoendelea ikiwa ni kipigo chake cha kwanza tangu michuano hio ianze.

Sasa Yanga itasubiri mshindi kati ya Simba na Jang'ombe boys ambao watacheza kesho jioni.

USHAURI - YANGA IJITOE KWENYE MICHUANO HII ILI KULINDA HESHIMA YAKE , SIKU IKIKUTANA NA MNYAMA WATAADHIRIKA ZAIDI , HERI LAWAMA KULIKO FEDHEHA .
 
62192d507eeb1fd8556c63cd6d4e1621.jpg
 
Zilikuwa salamu kwa JECHA. Kule Dimani Mbunge alofariki (RIP Hafidh Ally) alikuwa mwana soka kindaki ndaki...... inaweza kuwa ISHARA kuwa "wa kijani na njano" atapata KIPIGOOOOO cha Mapinduzi (Mageuzi)!
 
Duh poleni watani, kwa hizo 4 naona kama kesho mtakata rufaa mmeekewa madawa kwenye maji😛😛😛😛
 
Yanga tumewashika panapouma leo hizi ni salamu tu kwa wenzao wa Simba
 
TUMETOA SALAMU. Simba nanyi mjiandae na watu hawa; BOKKO, YAHAYA MOHAMMED, ATTA AGYEI, MAHUNDI.... Teh teh Raha Sana
 
Back
Top Bottom