Kuna dhana mbili. Moja ni kuwa mashbiki wa Yanga huvua kandambili zao na kuzishika mkononi wakisukuma basi lao kutoka Karume au taifa mpaka Jangwani. Wakawa wanaitwa kandambili.
Dhana ya pili, ni wakati wa mgawanyiko, Kina Shiraz na Mangara wakawa wanawaambia wachezaji waliobaki na Tambwe Leya kuwa achaneni na hao kandambili., jina walilokuwa Malo kabla ya mgawanyiko mje huku Raizoni.
Mashbiki wa Simba pia walikuwa wakijiita Raizoni.
Halafu Yanga hatuchukii tukiitwa kandambili. Tulipokea jina hilo with pride kutoka kwa wazee wetu. Nakumbuka tawi la Yanga mtaa wa Mkumba Temeke lilikuws linaitwa "Msichoke" na lilikuws na picha ya Kandambili kubwa tu ya kuchora kwenye ubao.