Mkuu acha Ubishi,sote mpira tunaangalia,Ukweli ni kwamba,Yanga kwasasa hawachezi vizuri!
Hatuitaji timu ishinde Magoli mengi but mpira uonekane!
Yanga kwasasa inakosa kuwapa pressure wapinzani,mipira mingi wanarudisha nyuma badala ya kupeleka pressure Kwa mpinzani!,Ile timu ya miezi michache nyuma ambayo ilikuwa ikiwapa presha wapinzani Sasa hivi ni kama imefifia!
Pia Gamondi abadilike,aanze kuwaamini wachezaji,sijaona sababu ya Aucho Leo Kucheza,nje una Sure boy na Mkude!
Akiendelea kukaza fuvu na style yake hii ya Uchezaji,Ubingwa utakuwa historia!
Nasredin Nabi alikuwa hatabiriki,japo alikuwa na wachezaji wa kawaida lakini kila Mchezaji alipata nafasi ya Kucheza na akaonyesha Ubora wake!,Tatizo la Gamondi anatabirika na ndiyo maana makocha wengi wameshamsoma!
Nabi alikuwa akikubadilishia wachezaji wawili tu kila kitu kinabadilika,huyu Gamondi yeye akibadili Mchezaji hakuna kinachobadilika!