Nonda alikua mchezaji halali wa Yanga msimu 1994/1995 na Msimu uo Yanga ilitolewa na Black pool ya Zimbabwe katika hatua ya Robo fainali.
Yanga wakiwa toa vaal professional ya South Afrika kwa Agg ya 4-2
Wakaja kuwatoa timu ya Mauritania wakaja kutolewa na Black pool hatua ya Robo fainali.
Baada ya Yanga kutolewa ndipo Vaal professional waka muhitaji Nonda.
Nonda aliuzwa Chini ya Mwenyekiti Mpondela kwa Dola 10,000/= kwenda Vaal professional ya South Afrika
Haiwezekani ITC ya Nonda itoke shirikisho la mpira la DRC wakati mchezaji Nonda alikua amesajiliwa na Yanga.
Haiwezekani Nonda ashiriki michuano ya Kombe la washindi mpaka hatua ya Robo fainali wakati kibali wanacho shirikisho la mpira DRC.
Kama ITC yake ingekua haipo Tanzania (FAT) asingeweza kuchezea Yanga mashindano ya Ligi ya Ndani Wala Mashindano ya kimataifa.
Nonda alikwenda Vaal professional kwa baraka zote za Yanga na Chama Cha mpira wa miguu Tanzania kilituma ITC yake kule South Afrika.