Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Lengo la Uzi huu si sana kujutia kupoteza hela, bali ni kuuweka kama funzo kwa wadau wengine kwamba, iko siku hata saa mbovu inaweza kuonyesha muda sahihi.
Kiukweli kwa mara ya kwanza niliganda ubongo, maana sikudhani hata chembe kama Yanga anaweza kuambulia hata sare huko Algeria, achilia mbali kushinda, kujiamini kwangu kulifanya niropoke kwa rafiki yangu wa Chanika ambaye nilimuahidi kumalizia nyumba yake ikiwa Yanga itapata goli Ugenini au hata ikitoka sare, sasa baada ya kuwekeana kamali hii nilimwambia anipe gharama ambayo napaswa kujiandaa nayo ikiwa maajabu hayo yatatokea , nikaambiwa ni 5mil.
Pamoja na ukweli kwamba sikuamini kama yanga yaweza kutoboa, sasa napaswa kulipa gharama hiyo Jumatatu kabla ya saa 6 mchana.
Natoa wito kwa wadau wote kwamba, kabla ya kuahidi jambo muwe makini kuangalia alama za nyakati.
Nalipa lakini siipendi Yanga