Kuhusu boka ni Mchezaji mzuri kwenye mikimbio kutoka eneo la chini kwenda eneo la juu ila mipira yake mingi haina usahihi, anaweza kupiga cross 6 ikafika moja zingine zinatoka nje, zinakuwa blocked na mabeki au ziende kwa kipa, bado hana pass accuracy.
Kuhusu viungo vya juu kwa sasa wamekosa ubunifu, tukimtoa pacome the rest wanategemea kutumia mbinu ya mwalimu kwa asilimia 98 ili kuleta production kwenye timu ila pacome na max huwa wanajaribu kufanya vitu binafsi nje ya mfumo wa mwalimu kitu ambacho huwafanya waonekane ni wachezaji wenye umuhimu mkubwa na hatari zaidi kwenye timu.
Ila kingine ninachokiona kwa yanga uwepo wa mastar wengi wenye uwezo mkubwa kunamchanganya Mwalim hajui aanze na nan na nan ili apate kitu kilichobora kitu ambacho kinampelekea kila siku kurotate kikosi akitafuta 11 bora.
Hadi sasa Yanga haina first 11 inayotambulika.