Yanga na Simba zote zina hiyo tabia ya kujazana klabuni asubuhi. Ila wale wa Yanga naona wamezidi. Kuna jamaa aliacha ajira nzuri Kigoma ili tu awe anashinda pale klabuni Jangwani.
Ningekuwa na uwezo ningeenda kuwachapa bakora hao mashabiki. Jumatatu hii muda wa kazi hakuna pa kukanyaga mitaa ya Jangwani na Twiga kisa droo ya CAFCL, hizi timu ni msiba.