Yanga Inafanya Mapinduzi ya Kisoka, SSC bado iko na Mpira wa Siasa

Megalodon

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,534
Reaction score
7,866
Niseme kweli SITOTAMANI kuangalia tena Mpira wa Simba na Yanga hiyo October.

Kwa Mapinduzi na Mageuzi anayoyafanya Yanga ambayo yapo kimkakati kimataifa zaidi, hali itakuwa ni mbaya kwa SSC na itakuwa ni aibu sana SSC atakapokutana na Yanga.

Imagine tu , Kuna Stefano Aziz , kuna Tusila Kisinda , kuna Mayele , Mama yangu ..... kuna yule mwendawazimu Efua Morrison ..... huku kuna huyu Mpemba Feisali..... tuacheni Utani SSC anatoka vipi hapo ? Kwa huyu Dejan ? Tshabalala ? Outara ? Yaani kwa mchezaji gani kwa mfano atakuwa na power ya kumzuia Efua, Tusila, Stefano au Mayele .. hii ni hatari sasa. Hawa wazee wa SSC watapata tabu sana, nasema watapata tabu sana.... maana kipigo chake kitakuwa ni cha mbwa koko.

Simba yeye ana Mzungu na siasa za matangazo bila matendo , hali ni mbaya MSIMBAZI , nasema tena hali ni tete MSIMBAZI .

Timu mpaka sasa bado inafanyiwa MABORESHO kwa mujibu wa Msemaji wa SSC; Ligi imeshaanza, na Champion ligi ina wiki chache kuanza ..... bado tupo kwa maboresho tena ..... Nasema hali ni tete Msimbazi..... Barba Out !

Kikosi cha UTOPOLO cha sasa ni cha Dhahabu na hakika kinakwenda KUSABABISHA. Naiona Yanga kwenye robo fainali ya CAF : naiona SSC ikitolewa Kwenye Preliminary stage round ya pili. Time will tell ,tuupe Muda wakati.

SSC bado inaamini kwenye myth , kwamba wao ni timu kubwa .... wanasahau kuwa mpira ni elasticity na Yanga amesha prove wrong kwa SSC more than 3 times kuwa SSC nyakati zimebadilika..... lakini SSC ina Act Kama MANDONGA.

Kwenye akili ya mandonga yeye ni MSHINDI na yeye anaweza kumpiga yoyote na kuwa alipigwa kwa kuotewa.... yaani ameiaminisha ujinga akili yake out of knowing the reason why ..... ndiyo inachofanya SSC.

Ni suala la Muda mchache sana ukweli utajulikana na ni muda mchache sana Barba Gonzalenz itamlazimu ajitafakari upya na utendaji wake pamoja na strategy zake.

Nina rudia tena, Barba ame focus zaidi Kwenye matangazo na siasa za Mpira kuliko investment na performance ya timu.

Time will tell very soon , Hali ya Msimbazi ni Mbaya sana hasa ukizingatia usajili uliofanywa ni kama vile Management haikujifunza kupitia last season. Ni dhahiri kuwa Yanga ilijifunza kitu na ina isuprize dunia very soon. Hongera Engenear. Mwanaume ndiyo kichwa cha familia.

Poleni wanasimba. Yule mwendawazimu wa mbio ameingia mjini, kazi ipo !
 
Tusila ni reject. Alivyocheza mara ya kwanza yanga alishinda nini?
 
Mapinduzi Makubwa ya Kumpindua Mapinduzi Balama yanaonekana Lkn Sio Mapinduzi Ya Soka.

Mapinduzi Ya Soka huwezi Kuyafanyia 'Gezaulole KIMBIJI'.! Kule Kuna Mapinduzi Ya Kilimo cha Nyanya.
 
Mwezi October naona kabisa tutakavyo mfukuza Barbra na Coach wake kwa matusi na chupa za maji, simba tunaenda kuingia ktk migogoro isiyoisha na tutapoteza kilakitu tena... Simba tunajidanganya kwa kusafiri kwenda nje kucheza friend match wakat kikosi chetu ni mauzauza tu yamejazana. Mpira wa sikuhiz sio kama zaman hadi ucheze na team kubwa ili ujue kikos chako kikoje...
 
Sisi mashabiki wa Simba ukweli kabisa pamoja na uongozi nimeamini hatuna akili.
Kushabikia mzungu na huyu kocha mpumbavu ni aina ya upunguani mkubwa.

Yaani timu inacheza pasi fupi za nyuma zisizo na madhara halafu kuna wapumbavu wanasifia eti el hilal ni timu ngumu tumejitahidi kufungwa goli moja?

Sijawahi kuona mashabiki hopeless kama wa timu yangu Simba.
 
Ni suala la muda tu wanasema wao wanajiandaa zaidi na mechi za kimataifa kwa kucheza mechi za kirafiki na timu kubwa kwaiyo wale wanaocheza mechi za kirafiki na kmc awatofika mbali kimataifa hizo ndo akili za mbumbumbu, sasa ngoja tuone ni nani atafurushwa mapema kwenye michuano ya kimataifa maana mpira unachezwa hadharani timu yenye kikosi bora itajulikana soon, mambo ya kukariri maisha yalishapitwa na wakati
 
Kunywa soda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…