Yanga inambidi amfunge Medeama goli 5 ili kufufua matumaini ya kufuzu

Belouzdad anachekea chooni, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Belouzdad anachekea chooni, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mleta uzi kaleta hesabu za vidole (assumption) lakini kashindwa kufanya assumption katika scenario zote. Mwelekeo wa Yanga utapatikana katika mechi ya kesho dhidi ya Medeama. Akishindwa kumfunga basi hana mwendo tena. Ila akishinda basi katika moja ya sala na maombi yake ni Al Ahly amfunge Belouizdad.
 
sio kweli yanga inahitaji ushindi hata wa goli moja tu
 
Yaan panga pangua, Al ahly na Belouzdad wanaenda Robo.
 
Asec hata akitoa draw na Simba bado atakuwa na uhakika wa kuongoza kundi

Asec hana ubora wa kutisha sana kumzidi Simba
 
Ndugu yangu adriz hili faili vipi halifai kuwekwa hapo masijala kweli?

#Kwamatumiziyabaadae. 😀
 
Ha ha ha nimecheka kama mazuri
 
Mwakarobo kwa sababu amekuwa kubwa jinga miaka yote hajifunzi akakwama hapohapo mfano wake ni sawa jamaa ambaye kila siku anaingia chumbani na mkewe wanakuwa faragha na kusaula lakini hafanyi chochote ataonekana kolo kuliko jamaa mwengine ambaye anajitafuta bado hajaoa bado lakini anaesema siku nitakapo mpata mweza kitaumana na ikawa hivyo hakufanya uzembe alipojipata.
 
Safari ya Yanga robo fainali ni ngumu, ni ngumu sababu ya kuruhusu zile goal 3. Huku cha kwanza wana angalia H2H na mshindani wako ikiwa point mpo sawa. Mshindani wa Yanga ni CR B hivyo Yanga anatakiwa kumfunga CR B 3 au zaidi kitu ambacho ni kigumu.
Hata kama akimfunga Medeama 10 ila akishindwa kumfunga CR B goal 3 hapa kwa Mkapa ajiandae safari yake ndio imeiva arudi kucheza na Mashujaa na marefa wake wa mchongo kina Kheri Sasi.
 
Sasa mpira wa kutegemea sala kwenye mechi nyingine ni mpira mgumu sana...Yanga hatahitaji hizo sala kama akimfunga Medeama goli 5 akafunga na CRB goli 3 halafu akatoe draw kule Misri...... hata CRB akimfunga Ahly bado Yanga atapita
 
Ndio nimesema pia itabidi amfunge CRB goli 3 kwa 0
 
Kinachoitajika ni point 3 ayo mengine ya goli 5 ya kwako, hesabu zako za tuki na waki hazina nafasi!
 
Wakilingana point na timu yoyote katika group stage, kinachoangaliwa next ni 'superior head-to-head rule', yaani timu hizo mbili zilipokutana zenyewe katika mechi mbili ni ipi ilikuwa na matokeo bora ikiwemo goal difference na away goal(s) baina ya hizo timu, bila kujali matokeo ya mechi nyingine.

Kwa mantiki hiyo, hata kama Yanga ikishinda 7-0 dhidi ya Medeama halafu ikaja kushinda 4-1 dhidi ya Belouzdad na wakalingana points na Belouzdad, basi itakayokuwa juu ya mwenzake ni Belouzdad kwa ajili ya goli la ugenini. Kwa hiyo mabao mengi dhidi ya Medeama yataisaidia Yanga iwapo watalingana point na Medeama, sio na Belouzdad

 
Niwe mkweli, lolote baya limkute utopolo tz tufurahi
 
Ebwana eeeh huu uzi niliusoma ila sikuuzingatia sana maana bado nilikuwa kwenye vibe la ushindi wa jana. Kumbe safari ya Yanga inaweza kuisha rasmi leo au kabla hata ya mechi za mzunguko wa 5 wa timu zote? Yaani ili kujua kama atafuzu inabidi kuumiza vichwa kwa Tuki Waki Table, kwani mlitulipia ada?

Tuombee Medeama ampunguzie maumivu mgonjwa wetu mahututi kwa kunyofoa waya ili kuimaliza safari yake leo. Kama ndugu tuombee hilo. Ikishindikana saana basi CRB amfunge au atoke sare na Al Ahly katika mechi iliyoahirishwa iliyokuwa ifanyike jana. Ni suala la Yanga kuchagua tu anataka kufa kifo gani 🤣😂🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…