Yanga inambidi amfunge Medeama goli 5 ili kufufua matumaini ya kufuzu

Yanga inambidi amfunge Medeama goli 5 ili kufufua matumaini ya kufuzu

Niwe mkweli siwezi nikamuombea Yanga apite makundi.

Ntamuombea ashinde mechi lakini sio afike robo

Robo ambayo Simba kwa miaka minne amekuwa akiingia lakini yeye amekuwa mtu wa kwanza kunidhihaki na sasa kanitungia jina Mwakarobo.

Hapana siwezi kuwa mnafiki.

Lazima ajue kwanini kuna ugumu kwenye haya mashindano, lazima atambue kwanini kufika hapa ilimchukua miaka 27.

Hii ndio nidhamu ya mpira ambayo anatakiwa kujifunza na sio kupiga domo kwa timu pinzani na kuzipa mbinu za kumfunga Simba.
Ndio maana timu yako mbovu sana 😁🤣😁
 
View attachment 2847530


Ki ukweli japo mi shabiki wa Simba nataka pia Yanga apite robo, sababu itakuwa heshima kwa TZ kuwa na timu mbili robo fainali, katika timu 8 (Hata Misri ni mara chache anafanikiwa kuingiza timu 2 robo fainali)


Ili Yanga awe na nafasi ya kufuzu robo sio tu amfunge Medeama bali anatakiwa kumfunga kwa goli 5 au zaidi

Likely Scenario ipo hivi


Yanga anagombea nafasi ya pili na C.R.B huku yanga akiwa na goal difference ya -3 wakati CRB ana +2

Yanga akishinda goli 5 atakuwa na pointi 5 na G.D ya +2 na CRB akitoa draw na Ahly kule Algeria (likely scenario) naye atakuwa na pointi 5 na G.D yake ikibaki +2 na Yanga kuwa nafasi ya tatu

Mechi ya 5 Yanga dhidi ya Ahly kule Misri akijitahidi akifungwa 2-1 bado atakuwa na pointi zake 5 bado na goal diffence ya +1

CRB akimfunga Medeama kule Algeria 2-0 naye atakuwa na pointi 8 na G.D ya +4

Mechi ya mwisho Yanga dhidi ya CRB anamfunga goli 3-0 kwa Mkapa anakuwa na pointi 8 na G.D ya +4 huku CRB akibaki na pointi nane pia na G.D ya +1 na Yanga anapitaa kwa kuwa na magoli mengi

So mechi ya kesho ndio mechi pekee ambayo Yanga ana nafasi kubwa ya ushindi, ushindi basi uwe mnono....
20240311_212032.jpg

Usishindane na Yanga Sc
20240309_101920.jpg
 
Ebwana eeeh huu uzi niliusoma ila sikuuzingatia sana maana bado nilikuwa kwenye vibe la ushindi wa jana. Kumbe safari ya Yanga inaweza kuisha rasmi leo au kabla hata ya mechi za mzunguko wa 5 wa timu zote? Yaani ili kujua kama atafuzu inabidi kuumiza vichwa kwa Tuki Waki Table, kwani mlitulipia ada?

Tuombee Medeama ampunguzie maumivu mgonjwa wetu mahututi kwa kunyofoa waya ili kuimaliza safari yake leo. Kama ndugu tuombee hilo. Ikishindikana saana basi CRB amfunge au atoke sare na Al Ahly katika mechi iliyoahirishwa iliyokuwa ifanyike jana. Ni suala la Yanga kuchagua tu anataka kufa kifo gani 🤣😂🤣
Kumbe 😂😁🤣😂😂 Cc adriz Evelyn Salt Nifah ephen_ njooni huku tuwacheke Hawa makolo
 
Back
Top Bottom