Yanga inaweza kua timu ya kwanza kufika nusu fainal CAF kutoka Tanzania

Yanga inaweza kua timu ya kwanza kufika nusu fainal CAF kutoka Tanzania

Du we kiazi kweli.. yaani Yanga ikifika nusu fainali ndo itakuwa timu ya kwanza tanzania kufika hatua hiyo.... hivi kwa nini wenzetu wa upande huo hamnazo kabisa kichwani???
Barikiwa sana
 
Yanga nusu fainali tunafika msimu huu

Mark my words

Only team ambaye nina hofu nayo ni Al Ahly tu sababu ya uzoefu wao.

Uzuri tumepangwa nae kundi moja.. hivyo robo hatukutani nae

Mamelodi hana mpira mkubwa wa kutufunga zaidi ya kutegemea jua la saa tisa mjini pretoria. Na kubebwa na marefa ili kulinda ajira zao sababu rais wa caf ndio mwenye timu.

Uzuri sisi ni weusi jua tunalimudu tutapigana nae kibabe kwenye jua
Mamelodi ule ni moto bora Al Ahly achana na mambo ya jua.
 
Mmeanza wazee wa record za kuokoteza.
Tatizo hamtaki kukubali simba amewazidi kimataifa ndio maana mnashangilia kwenda robo fainali mpaka mnataka kufa haya nendeni kwenye page ya caf mmeambiwa mnaingia robo fainali kwa mara ya kwanza.
 
Hakuna kinachoshindikana. Kila kitu ni mipango tu na malengo.
 
Kwanza niseme mimi si shabiki wa simba wala si shabiki wa yanga, ila ni shabiki wa mpira na timu zote hizi mbili nazifuatilia kuanzia mashindani ya ndani kwa maana NBC premier league.

Azam Federation na michuani ya kimatimaifa kuanzia kombe la shirikisho mpaka ligi ya mabingwa.

Kwa matokeo ha leo ya yanga naiona kabisa yanga inafika nusu fainali kwanza wana ile spirit waliyokua nayo tangu msimu wa mwaka jana walipofika fainali ya shirikisho so ni kitu ambacho wamekifanya kama marking scheme yao, kucheza bila pressure kwakua timu haijapewa malengo makubwa sana ila ndani ya kiwanja wanajituma sana.

Kikosi walichonacho yanga kwa sasa hawana hofu ya kucheza na timu yoyote ukanda huu wa africa now yanga ana uwezo wa kupata matokeo tena mazuri kwa mwarabu si jambo dogo kiukweli.

Haya machache natamka insha'Allah yanga inaweza kufika nusu fainali na kua clanu ya kwanza Tanzania kufika hatua hiyo ligi ya mabingwa Africa.
Matusi,kejeli na makasiriko sikaribishi
Tuibee hivyo
 
Yanga nusu fainali tunafika msimu huu

Mark my words

Only team ambaye nina hofu nayo ni Al Ahly tu sababu ya uzoefu wao.

Uzuri tumepangwa nae kundi moja.. hivyo robo hatukutani nae

Mamelodi hana mpira mkubwa wa kutufunga zaidi ya kutegemea jua la saa tisa mjini pretoria. Na kubebwa na marefa ili kulinda ajira zao sababu rais wa caf ndio mwenye timu.

Uzuri sisi ni weusi jua tunalimudu tutapigana nae kibabe kwenye jua
Sio kweli mamelod wapo vizur
 
Du we kiazi kweli.. yaani Yanga ikifika nusu fainali ndo itakuwa timu ya kwanza tanzania kufika hatua hiyo.... hivi kwa nini wenzetu wa upande huo hamnazo kabisa kichwani???
Sasa wenyewe CAF mwaka jana,kwenye page yao official walisema hivyo.
64E25CB4-EBB1-4C94-9A59-C836EF5379E6 (1).png

Kama unabisha,bishana nao CAF.
 
Tatizo hamtaki kukubali simba amewazidi kimataifa ndio maana mnashangilia kwenda robo fainali mpaka mnataka kufa haya nendeni kwenye page ya caf mmeambiwa mnaingia robo fainali kwa mara ya kwanza.
Kila mtu ana mara ya kwanza hivyo hivyo kwa Yanga sioni tatizo, umeanza wewe umefikiwa na unaweza pitwa , kutangulia sio kufika
 
Kila mtu ana mara ya kwanza hivyo hivyo kwa Yanga sioni tatizo, umeanza wewe umefikiwa na unaweza pitwa , kutangulia sio kufika
Basi heshimu waliokutangulia dharau haikufanyi wewe kuwa bora kuzidi watangulizi wako,bali juhudi zako.
 
Kwani haya matokeo ya jana hakuna Timu toka Tanzania iliyoshinda zaidi ya goli 4 kwenye champions League?Au Yanga ndo Timu ya kwanza kufanya hivyo.
 
Hahaha, Yanga wachunguzwe huenda wanatumia midawa ya kuongeza nguvu maana hata majini hayana zile nguvu.
 
Sema Yanga inaweza kufikia nusu fainali sio timu ya kwanza kufika nusu fainali kutoka Tanzania, Simba ilishafika nusu fainali. Na sidhan Kama wewe ni shabiki wa Simba
Anaongelea "ligi ya mabingwa Afrika" kwani mwaka 1974 Simba ilipofika nusu fainali haikuwa ligi ya mabingwa Afrika.

Please be informed accordingly.
 
Mbona CAF hawana hizo habari au mmesahau post waliyo ipost mwaka jana.
View attachment 2915655
Unakua mbishi wakati hujui kitu, ligi ya mabingwa ilienda inabadilika Jina, hili total energies caf champions ni jipya na Toka iitwe hivyo Simba haijawahi kufika nusu fainali, ila mwaka 1974 Simba ilicheza nusu fainali champions league ila mdhamini hakua total energies.

Nikupe mfano mrahisi, ligi kuu Bara imekua ikibadilika Jina Mara kadhaa iliwahi kuitwa ligi daraja la kwanza, iliwahi kuitwa Vodacom premier league na Sasa inaitwa NBC premier league. Sasa akisema azam haijawahi kuchukua ubingwa Toka iwe NBC premier league hamaanishi kwamba haijawahi kuchukua ubingwa wa ligi kuu ila Toka iwe NBC ndio haijawahi kuchukua ubingwa. Ina maana unaposema Yanga ni mabingwa wa kihistoria wamechukua Mara 29 manake wanahesabu vikombe vyote vya ligi kuu bila kujali Kama ilikua inabadilika Jina. Jina halibadili league, league ni Ile Ile ila majina yanabadilika.
 
Kwa hiyo nyie hamjawahi kuchukua tokewa iwe NBC Premier league?

Ila kuna meno First-Ever, kwa Kingereza changu ni sawa na kusema never in any occasion.Hizo nyingine ni swaga zenu.
 
Back
Top Bottom