Yanga iongeze bidii kujifunza kwa Simba Sc

Yanga iongeze bidii kujifunza kwa Simba Sc

1. Makolokolo wameingia kiuwekezaji wa kampuni na Mo tangu 2015.

MAFANIKIO YA SIMBA:

Kutinga robo fainali za CAFCL mara 3 na robo fainali ya CAFCC mara 1 ndani ya miaka 7.

2. Yanga FC wameingia kiuwekezaji wa kampuni ya GSM 2021.

MAFANIKIO YA YANGA:

Kutinga robo fainali ya CAFCC baada ya mwaka mmoja na nusu tu.

Je kati ya Simba FC na Yanga FC ni klabu ipi inapaswa iige mfano kwa klabu nyingine kiuwekezaji na kimaendeleo?
Wewe ni kiazi post yako inaenda humu🚮..
 
Sawa. Kwa hiyo mkaona muige? Kwa hiyo mmepoteza uhalali wa kusema hamtumii njia za shortcut.
Kwa hiyo na wewe ulitumia SHORTCUT?

Mkaona haitoshi ndipo mkajiongeza kuingia na kuni na kuota moto katikati ya uwanja ,na kurudi Kinyumenyume.
 
Njia za mkato tumeiba? si tumetumia hela zetu,nyie Mudy katoa 1.5b msimu uliopita mnawaleta watu wa ajabu ajabu,mara Okwa,Okra siju Sawadogo.

Sisi tunatumia hela yetu na tuna sajili kwa kufuata ataratibu.
Bil 1.5 ni hela ndogo saaana sema tu tuko huku nchi za kimaskini na watu wana mawazo ya kimaskini. Kuna uzi mtu ametoa mchanganuo wa manunuzi ya hao wachezaji, nenda kausome. Tena kaweka hadi estimation ya milioni 50 kwa baadhi ya wachezaji na hiyo bil 1.5 inafika.
 
Tubaki kwenye mada iliyoko mezani, tuache kuruka ruka.
Kwa hiyo na wewe ulitumia SHORTCUT?

Mkaona haitoshi ndipo mkajiongeza kuingia na kuni na kuota moto katikati ya uwanja ,na kurudi Kinyumenyume.
 
Acha porojo, Mpira ni uwekezaji na kupata wataalamu sahihi. Kilichokua kinawakwamisha Yanga ni fedha ambayo itakuwezesha kupata watu sahihi wenye uwezo wa kutafsiti mipango ya Taasisi.

Kwasasa Yanga Wana fedha kiasi na imepata watu sahihi ndiomaama wapo vizuri.
Usifikiri Yanga inapata matokeo Kwa kubahatisha, Iliwagharimu kuwekeza fedha Kwa kuwatafuta Laliga na Sevilla katika plani zao na mpaka Sasa wanapata ushauri wa kitaalamu kutoka ughaibuni.

Yanga hawaitaji kujifunza chochote Kwa Simba kwakua njia zote walizokua wakitumia Simba kupata matokeo hazifai Kwa mpira wa kisasa.
Simba wamekua wakitumia njia chafu za mkato Ili wajifurahishe na vilabu vingi vilikua vikilalamika namna mambo yanavyo fanyika wakiwa hapa Kwa Mkapa.

Mwishowake Simba wali umbuliwa na CAF Kwa kupigwa faini kutokana na vitendo vya kishirikina na tabia chafu katika mpira wa miguu.
Yanga imechagua kuwekeza katika wataalamu wa soka na mbinu za kisasa kupata matokeo.
Yanga walisha vuka izo hatua za kulazimisha matokeo Kwa njia chafu za kupuliza madawa na Ulozi wa kiwango Cha CAF.
Yanga itafanikiwa mapema kwakua inapitia njia sahihi ila gharama zake ni fedha katika wataalamu.
Vipi ile mechi ya geita na namungo si ndo zenu kubebwa na marefa
 
Unasema hamtaki njia za mkato wakati mmebeba kikosi kizima cha AS Vita na kukihamishia hapa?
Nashangaa sijui kwanini hili haliongelewi, lakini ni kuishusha hadhi ligi yetu, haiwezekani unachukua karibia kikosi kizima cha wachezaji waliotemwa unaleta kwenye timu yako.
 
Ujinga ni mzigo unaweza kuiga kwa timu isiyo na miundo mbinu ya michezo?, Kipi Cha maana ukichoonesha kinapaswa kuigwa kutoka kwa Simba?. Matokeo ya mpira ni ya muda ambao hata ihefu au Namungo anaweza kuyapata.
Ungeolodhesha yanga aige nini kutoka kwa Simba kwanza kabla ya kuota ndoto ya kuchukua CAF cup wakati timu haina uwezo hata wa kuvunja mkataba wa mchezaji mwenye thamani ya 400m, uchukue ubingwa wa CAF na akina Baleke au Kanoute?

Platinum member hovyooo kabisa [emoji28]
Yanga anaiga kila anachofanya mume wake Mnyama
 
Tunajifunza kwa wanaojua na wanao tumia sayansi ya mpira kupata ushindi kama Mamelodi,Aly Ahly,Esperence nk ni si kama hawa .
View attachment 2562723
Mara waote moto ,mara Kinyume nyume.
Aisee!! Cha kushangzmaza, kwenye hii mechi, na ile ya basi ya basi kurudi kinyume nyume; walifungwa!

Aisee ni vizuri Yanga wakachagua hayo mambo ya kujifunza. Wasichukue kila kitu! Maana wataishia tu kuaibika.
 
Kwa hiyo na wewe ulitumia SHORTCUT?

Mkaona haitoshi ndipo mkajiongeza kuingia na kuni na kuota moto katikati ya uwanja ,na kurudi Kinyumenyume.
Vipi nyie wachezaji wenu mbona ni ma papai kabwili
 
Bil 1.5 ni hela ndogo saaana sema tu tuko huku nchi za kimaskini na watu wana mawazo ya kimaskini. Kuna uzi mtu ametoa mchanganuo wa manunuzi ya hao wachezaji, nenda kausome. Tena kaweka hadi estimation ya milioni 50 kwa baadhi ya wachezaji na hiyo bil 1.5 inafika.
Sasa unabishana na Mo katoa hela,sasa huyo ambaye katoa huo mchanganuo ndiye aliyetoa hizo hela?
Screenshot_20230323_170920_Instagram.jpg

Yaani hela atoe mwengine mchanganuo afanye mwengine ambaye sio hata muhasibu wa club.
 
Umeshakula ngada wewe,sasa ulitaka wawazae kwanza?
Nitajie mchezaji wa Yanga ambaye amelelewa pale klabuni hadi leo ni tegemeo. Na usiniambie sijui Mzize au Feisal maana hao hawajakulia Yanga.

Point yangu ni kuwa mnapojisifu kwa mafanikio ya haraka, kwa njia mliyotumia ni wazi mafanikio yatakuja haraka zaidi kwa sababu unachukua ambacho tayari kimestawi. Simba wametumia muda mrefu kujitafuta huko CAF, Yanga wana advantage ya kuona nini wafanye na nini wasifanye kwa kuwaangalia Simba.

Tunaposema Yanga wajifunze kwa Simba haimaanishi tu kuiga mambo ya kufanya lakini poa nini wasifanye. Kiburi chenu kinawakatalia msikiri hilo.
 
Tubaki kwenye mada iliyoko mezani, tuache kuruka ruka.
Nani arukeruke kwani hii mada ya shortcut kaingiza nani? yaani wanaongea ulicho ongea ww unasema shortcut ina maana hata ww unacho kiongea hukifaham.
 
Sasa unabishana na Mo katoa hela,sasa huyo ambaye katoa huo mchanganuo ndiye aliyetoa hizo hela?
View attachment 2562798
Yaani hela atoe mwengine mchanganuo afanye mwengine ambaye sio hata muhasibu wa club.
Kwani nimebisha bil 1.5 haijatumika? Nimekwambia kwa pesa hiyo uende kusajili wachezaji karibia 10 utategemea wachezaji wa quality ipi?

Wazungu wanasema "you get what you paid for".
 
Nani arukeruke kwani hii mada ya shortcut kaingiza nani? yaani wanaongea ulicho ongea ww unasema shortcut ina maana hata ww unacho kiongea hukifaham.
Mada ya shortcut ni direct response ya huyo niliyemjibu ndiye aliongelea kuwa Yanga haitumii shortcuts. Unajua jinsi midahalo inavyofanyika?
 
Yanga anaiga kila anachofanya mume wake Mnyama
Nimesema ujinga ni mzigo... Mafanikio hayaigwi it's a matter of investment..!
Unaweza kuiga kwa mtu asiye na nyumba ya kulala?, Ungesema Simba imejenga uwanja na Yanga akajenga sawa... Kwahiyo mlitaka yanga asiingie robo fainal kisa Simba alishaingia?. Rage hakukosea, orodhesha Mambo amabyo Simba ameyafanya yenye tija na maendeleo ya mpira amabyo yanga anapaswa kuiga... Matokeo Wala kufika robo fainal sio Jambo la kuiga ni issue ya uwekezaji.
 
Kwani nimebisha bil 1.5 haijatumika? Nimekwambia kwa pesa hiyo uende kusajili wachezaji karibia 10 utategemea wachezaji wa quality ipi?

Wazungu wanasema "you get what you paid for".
Kwai lazima kila msimu msajili wachezaji kumi?na unaweza ukakuta iliyotumika nusu nyingine watu wamepiga cha udalali na ndio maana mmepata magarasa kwa bei ghali.
 
Back
Top Bottom