Yanga iongeze bidii kujifunza kwa Simba Sc

Yanga iongeze bidii kujifunza kwa Simba Sc

Mada ya shortcut ni direct response ya huyo niliyemjibu ndiye aliongelea kuwa Yanga haitumii shortcuts. Unajua jinsi midahalo inavyofanyika?
Sasa nyie tuwaige kwa kipi au kwa hiki ?
images (38).jpeg

Na kile chajuzi cha kurudisha gari kinyumenyume.

Sisi tunawaiga wanaendesha mpira kisayansi na si nyingi mnayofanya mambo ya ajabu ambayo hamna club yoyote Africa na duniani iliyowahi kufanya.Tukiwaga nyie tutakuwa tunaishia robo kila msimu.
 
Sasa nyie tuwaige kwa kipi au kwa hiki ?
View attachment 2562824
Na kile chajuzi cha kurudisha gari kinyumenyume.

Sisi tunawaiga wanaendesha mpira kisayansi na si nyingi mnayofanya mambo ya ajabu ambayo hamna club yoyote Africa na duniani iliyowahi kufanya.Tukiwaga nyie tutakuwa tunaishia robo kila msimu.
Wewe ndiye mtu pekee duniani leo bado anaongelea hayo mambo ya kinyumenyume. Hata wenzio wameachana nayo maana hayana maana. Mliambiwa mlete ushahidi wa clip tofauti na ile mkapotea.

Eti mtaishia robo kila siku wakati haujaionja robo ya CL toka Nyerere yuko hai mpaka leo 🤣😂🤣
 
Kwai lazima kila msimu msajili wachezaji kumi?na unaweza ukakuta iliyotumika nusu nyingine watu wamepiga cha udalali na ndio maana mmepata magarasa kwa bei ghali.
Unamuita Okrah garasa wakati aliwafunga? Kwani nyie mnafungwa na magarasa?

Na haujaelewa hata naongea nini. Nimekwambia kaangalie mchanganuo uliotolewa na mtu mmoja utaona kiuhalisia hakuna cha ajabu katika manunuzi ya wachezaji kwa pesa hiyo hata bila habari za udalali.
 
Alivyo tufunga leo yupo wapi?

Kwa hiyo mchezaji kuifunga Yanga ndio anajua?

Mchanganuo uliotolewa na mtu mmoja na si muhasibu wa club sasa ni msikilize ili iweje wakati si chanzo cha uhakika.
 
Wewe ndiye mtu pekee duniani leo bado anaongelea hayo mambo ya kinyumenyume. Hata wenzio wameachana nayo maana hayana maana. Mliambiwa mlete ushahidi wa clip tofauti na ile mkapotea.

Eti mtaishia robo kila siku wakati haujaionja robo ya CL toka Nyerere yuko hai mpaka leo 🤣😂🤣
Mbona video na picha zipo na South CAF wakawapiga faini kwa kuharibu uwanja wa wenzenu sasa unataka ushahidi gani.

Na ndio maana hatutaki kukuiga ww na njia zako sababu tutaishia robo.
 
Una mental slavery kuamini kila kitu cha wazungu ni bora labda niku ulize pale Simba mzungu ni nani? Try again?
Hiyo sio mental slavery hiyo ni appreciation and recognition kwamba kizuri lazima kisifiwe, na waasisi waliokianza lazima wapewe sifa zao

Mental slavery ni kumbeba juu juu Hersi kwa ahadi ya kishamba eti "tusipochukua kombe mje mniulize"
 
KUNA wakati huwa hatupendi ukweli. Tunapenda kudanganyana kwa sababu tu ya ushabiki. Ni kama hili la Simba na Yanga kimataifa.

Nimeona tambo za Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho. Wanatamba kuwa watafanya vizuri na kufika mbali.

Wanatamba kuwa wao ni bora kuliko timu yoyote nchini kwa sasa. Ni kweli. Matokeo ya Ligi ya ndani yanaonyesha hilo. Ni wazi kuwa Yanga iko katika kilele cha ubora wao.
Tangu msimu uliopita mpaka sasa wamepoteza mechi moja tu ya ligi. Ni rekodi bora sana. Hakuna timu nchini imewahi kufanya hivyo.

Yanga imekuwa vyema sana ndani na nje ya uwanja. Haipotezi mechi kizembe. Ni ngumu kutabiri inapoteza mchezo lini. Inapendeza sana.

Lakini ukweli ni kwamba pamoja na uimara ilionao Yanga sasa bado ina mengi ya kujifunza katika michuano ya kimataifa.

Huku kwenye mechi za CAF, Simba ina dunia yake. Imejenga ufalme ambao hautikisiki kirahisi.

Ilianza ikiwa hovyo lakini imekwenda ikiimarika siku hadi siku. Sasa wamekuwa wababe hasa wakiwa nyumbani.

Baada ya miaka 15 bila kuingia hatua ya makundi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, miaka hii mitano iliyopita imebadilisha kila kitu.

Ilionekana kama imebahatisha ilipofuzu robo fainali mwaka 2019. Ni kweli haikuwa na timu imara sana kama sasa. Lakini ilikuwa na hesabu kali.

Pamoja na kufungwa 5-0 na AS Vita pale Kinshasa. Ikapigwa tena kipigo kama hicho na Al Ahly pale Cairo. Bado Simba iliweza kupenya. Iliweka hesabu kali na mipango ya kushinda nyumbani.

Leo hii Simba ni kati ya Timu 10 bora Afrika. Unajua Simba Sc inaelekea wapi. Kituo kinachofuata ni kunyakua kombe la kulitua juu ya mlima Kilimanjaro-Visit Tanzania. Kuna baadhi huleta dhihaka kwamba Simba imechukua kombe gani Afrika?!! Ni kweli hajachukua lakini ni nani anayeweza kutoka 1 ghafla akafika 10 bila kupita 2 na 3? Kwa hiyo Yanga wanayo ya kujifunza zaidi ya mengi ambayo mpaka sasa wamejifunza.

Kwanza kabisa wameingia kwenye kuendesha timu kiuwekezaji kama ilivyofanya Simba Sc na Mo Dewji. Hatimaye GSM amewekeza Yanga na matunda yameanza kuonekana. Pili wamekuwa na msukumo wa kuhakikisha wanatumia vizuri uwanja wa nyumbani kupata matokeo. Hii ndiyo ile Simba wanaita Kwa Mkapa hatoki mtu.

Leo hii katika point 46.5 za Tanzania CAF Simba ina point 39 na Yanga ina 10 pekee. Nasema izidishe bidii kujifunza ili kuvuna point nyingi zaidi na kufika viwango vya Simba Sc. Ikazane kwa sababu wote walikuwa ligi ya mabigwa Afrika lakini Simba anakuwa mkiwa bila mdogo wake Yanga ambaye hatimaye amedondokea Kombe la Shirikisho.

My Take
Wivu wa maendeleo ni jambo jema, ila wivu wa chuki ni dhambi itakufa kifo kibaya
Ligi ya ndani
 
Attachments

  • FB_IMG_1675231441645.jpg
    FB_IMG_1675231441645.jpg
    96.2 KB · Views: 2
  • JamiiForums-277588080.png
    JamiiForums-277588080.png
    198.7 KB · Views: 2
  • IMG-20230123-WA0149.jpg
    IMG-20230123-WA0149.jpg
    10.5 KB · Views: 2
Watu ujifunza Kwa walio fanikiwa hajalishi mzungu au mwafrika, Yanga imejifunza kwa Laliga na Sevilla utaalamu wa kisayansi jinsi soka linavyo endeshwa. Kwasasa wanatafuta mtaji wa wanachama na Mashabiki zote izo ni njia za kitaalamu kupelekea kujitegemea.
Sasa Yanga wajifunze Nini Kwa Simba, Kuwasha moto uwanjani, kupuliza madawa vyumbani au kutoa makafara na kufukia uwanjani!!
Miaka 30 bila hata kufika robo afu kumbe kuna sehemu ulikuwa ukijifunza!!!

Ebu tuambie umeanza lini kujifunza kwa laliga?

Kama umekuwa ukijifunza kwa laliga na bado hukuweza kufikia mafanikio makubwa kimataifa kama Simba, basi una kichwa kibovu au ubongo wako ni mdogo sana kuweza ku handle vitu vikubwa.

Au labda utuambie miaka yote hiyo ambayo umekuwa broke basi hicho ndio kitu ambacho laliga alikuwa anakufundisha
 
Mimi ni shabiki wa Simba ila Simba tuna mengi sana ya kujifunza kutoka Yanga.Siku zote sisi ni wasindikizaji, hatuna kombe hata moja.Mafanikio yetu ni kutoa mchezaji bora wa wiki 😄😄😄 Hatuna kombe hata moja, si ligi kuu,fa,mapinduzi,CAFCL,CAFCCL, ngao ya jamii wala ndondo, MUNGU ATUSAIDIE!
 
Alivyo tufunga leo yupo wapi?

Kwa hiyo mchezaji kuifunga Yanga ndio anajua?

Mchanganuo uliotolewa na mtu mmoja na si muhasibu wa club sasa ni msikilize ili iweje wakati si chanzo cha uhakika.
Taarifa rasmi zilizopo ni kuwa Okrah ana matatizo ya kiafya. Au wewe una taarifa tofauti?

Mnatumiaga vigezo vya wachezaji wenu kama Mayele na Aziz kuifunga Simba kama alama ya ubora wao. Sasa unapomuita mchezaji aliyewatungua garasa, nyie mnabaki kuwa nani?

Hautaki kusikiliza watu wanaokupa mwangaza ili at least utoke gizani, wewe unakataa ili tu uendelee kujifariji kwa mambo ya kufikirika.
 
Mbona video na picha zipo na South CAF wakawapiga faini kwa kuharibu uwanja wa wenzenu sasa unataka ushahidi gani.

Na ndio maana hatutaki kukuiga ww na njia zako sababu tutaishia robo.
Kwa hiyo habari za kinyumenyume zilikuwa South? Ok sawa.
 
Taarifa rasmi zilizopo ni kuwa Okrah ana matatizo ya kiafya. Au wewe una taarifa tofauti?

Mnatumiaga vigezo vya wachezaji wenu kama Mayele na Aziz kuifunga Simba kama alama ya ubora wao. Sasa unapomuita mchezaji aliyewatungua garasa, nyie mnabaki kuwa nani?

Hautaki kusikiliza watu wanaokupa mwangaza ili at least utoke gizani, wewe unakataa ili tu uendelee kujifariji kwa amambo ya kufikirika.
Mayele msimu uliopita alishika nafasi ya ngapi kwa kuwa na magoli mengi na msimu huu ana magoli mangapi?

Aziz K mpaka sasa kashafunga katika mechi tatu kubwa ya Simba,Azam na ile ya Tunusia na Sub anaingia tunamwona huyo Okrah ahafaamiki hayupo.

Eti Okrah anaumwa.Unamjaji mchezaji kwa mechi moja, bila kuangalia mwendelezo wale wa msimu husika.
 
Kwa hiyo Okrah kwa mtazamo wako ni garasa?
 
Achana na habari za kinyumenyume. Ni ushauri tu nakupa wa kishkaji ili usije ukaendelea kuaibika mbele za watu.
Ushauri upi maana mnayafanya mambo haya hadharani sasa sijui nani anaaibika.
 
Kwa hiyo Okrah kwa mtazamo wako ni garasa?
Angekuwa si garasa tungemuona uwanjani maana kwa sasa hachezi ,hata benchi hayupo, mazoezini hayoupo basi jukwaani kuitizama timu yake napo tumwone hayupo.
 
Back
Top Bottom