Yanga iongeze bidii kujifunza kwa Simba Sc

Mada ya shortcut ni direct response ya huyo niliyemjibu ndiye aliongelea kuwa Yanga haitumii shortcuts. Unajua jinsi midahalo inavyofanyika?
Sasa nyie tuwaige kwa kipi au kwa hiki ?

Na kile chajuzi cha kurudisha gari kinyumenyume.

Sisi tunawaiga wanaendesha mpira kisayansi na si nyingi mnayofanya mambo ya ajabu ambayo hamna club yoyote Africa na duniani iliyowahi kufanya.Tukiwaga nyie tutakuwa tunaishia robo kila msimu.
 
Wewe ndiye mtu pekee duniani leo bado anaongelea hayo mambo ya kinyumenyume. Hata wenzio wameachana nayo maana hayana maana. Mliambiwa mlete ushahidi wa clip tofauti na ile mkapotea.

Eti mtaishia robo kila siku wakati haujaionja robo ya CL toka Nyerere yuko hai mpaka leo 🤣😂🤣
 
Kwai lazima kila msimu msajili wachezaji kumi?na unaweza ukakuta iliyotumika nusu nyingine watu wamepiga cha udalali na ndio maana mmepata magarasa kwa bei ghali.
Unamuita Okrah garasa wakati aliwafunga? Kwani nyie mnafungwa na magarasa?

Na haujaelewa hata naongea nini. Nimekwambia kaangalie mchanganuo uliotolewa na mtu mmoja utaona kiuhalisia hakuna cha ajabu katika manunuzi ya wachezaji kwa pesa hiyo hata bila habari za udalali.
 
Alivyo tufunga leo yupo wapi?

Kwa hiyo mchezaji kuifunga Yanga ndio anajua?

Mchanganuo uliotolewa na mtu mmoja na si muhasibu wa club sasa ni msikilize ili iweje wakati si chanzo cha uhakika.
 
Mbona video na picha zipo na South CAF wakawapiga faini kwa kuharibu uwanja wa wenzenu sasa unataka ushahidi gani.

Na ndio maana hatutaki kukuiga ww na njia zako sababu tutaishia robo.
 
Una mental slavery kuamini kila kitu cha wazungu ni bora labda niku ulize pale Simba mzungu ni nani? Try again?
Hiyo sio mental slavery hiyo ni appreciation and recognition kwamba kizuri lazima kisifiwe, na waasisi waliokianza lazima wapewe sifa zao

Mental slavery ni kumbeba juu juu Hersi kwa ahadi ya kishamba eti "tusipochukua kombe mje mniulize"
 
Ligi ya ndani
 

Attachments

  • FB_IMG_1675231441645.jpg
    96.2 KB · Views: 2
  • JamiiForums-277588080.png
    198.7 KB · Views: 2
  • IMG-20230123-WA0149.jpg
    10.5 KB · Views: 2
Miaka 30 bila hata kufika robo afu kumbe kuna sehemu ulikuwa ukijifunza!!!

Ebu tuambie umeanza lini kujifunza kwa laliga?

Kama umekuwa ukijifunza kwa laliga na bado hukuweza kufikia mafanikio makubwa kimataifa kama Simba, basi una kichwa kibovu au ubongo wako ni mdogo sana kuweza ku handle vitu vikubwa.

Au labda utuambie miaka yote hiyo ambayo umekuwa broke basi hicho ndio kitu ambacho laliga alikuwa anakufundisha
 
Mimi ni shabiki wa Simba ila Simba tuna mengi sana ya kujifunza kutoka Yanga.Siku zote sisi ni wasindikizaji, hatuna kombe hata moja.Mafanikio yetu ni kutoa mchezaji bora wa wiki 😄😄😄 Hatuna kombe hata moja, si ligi kuu,fa,mapinduzi,CAFCL,CAFCCL, ngao ya jamii wala ndondo, MUNGU ATUSAIDIE!
 
Alivyo tufunga leo yupo wapi?

Kwa hiyo mchezaji kuifunga Yanga ndio anajua?

Mchanganuo uliotolewa na mtu mmoja na si muhasibu wa club sasa ni msikilize ili iweje wakati si chanzo cha uhakika.
Taarifa rasmi zilizopo ni kuwa Okrah ana matatizo ya kiafya. Au wewe una taarifa tofauti?

Mnatumiaga vigezo vya wachezaji wenu kama Mayele na Aziz kuifunga Simba kama alama ya ubora wao. Sasa unapomuita mchezaji aliyewatungua garasa, nyie mnabaki kuwa nani?

Hautaki kusikiliza watu wanaokupa mwangaza ili at least utoke gizani, wewe unakataa ili tu uendelee kujifariji kwa mambo ya kufikirika.
 
Mbona video na picha zipo na South CAF wakawapiga faini kwa kuharibu uwanja wa wenzenu sasa unataka ushahidi gani.

Na ndio maana hatutaki kukuiga ww na njia zako sababu tutaishia robo.
Kwa hiyo habari za kinyumenyume zilikuwa South? Ok sawa.
 
Mayele msimu uliopita alishika nafasi ya ngapi kwa kuwa na magoli mengi na msimu huu ana magoli mangapi?

Aziz K mpaka sasa kashafunga katika mechi tatu kubwa ya Simba,Azam na ile ya Tunusia na Sub anaingia tunamwona huyo Okrah ahafaamiki hayupo.

Eti Okrah anaumwa.Unamjaji mchezaji kwa mechi moja, bila kuangalia mwendelezo wale wa msimu husika.
 
Kwa hiyo Okrah kwa mtazamo wako ni garasa?
 
Achana na habari za kinyumenyume. Ni ushauri tu nakupa wa kishkaji ili usije ukaendelea kuaibika mbele za watu.
Ushauri upi maana mnayafanya mambo haya hadharani sasa sijui nani anaaibika.
 
Kwa hiyo Okrah kwa mtazamo wako ni garasa?
Angekuwa si garasa tungemuona uwanjani maana kwa sasa hachezi ,hata benchi hayupo, mazoezini hayoupo basi jukwaani kuitizama timu yake napo tumwone hayupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…