Yanga ipo miguuni mwa mtu huyu mmoja

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Yanga kwa sasa inaweza kukupa burudani ambayo hata mpenzi wako hawezi kukupa, inafurahisha eeh?

Wana umoja, hawakati tamaa kizembe, spirit ya kufight. Na safu nzuri ya ulinzi. Wanapewa sifa wengi lakini wanamsahau bwana mdogo mmoja.

Well, utaona tu yanga wanapopata goli, kocha kaze anamuita huyo bwana mdogo pekee huku wengine wakishangilia ila anamuita yeye tu na kumpa maelekezo. Umegundua eeh?

Sio mwingine ni bwana mdogo Feisal salum (fei Toto)

Huyu bwana mdogo Yanga sasa ipo miguuni mwake.

Ukiona yanga imetulia inacheza mpira mzuri, ujue hiyo ni miguu na akili ya fei Toto.

Yeye ndo anaamua team icheze vipi, mipira mirefu ama mifupi ama nini.

Ni kazi yake.

Anafanya kazi ya kuunganisha pivot ya mabeki na viungo wenzake kwenda mbele kutokea chini.

Fei anaficha sana madhaifu ya mukoko sergi tonombe"

Fatilia utagundua mukoko bila Feisal sio kitu.

Anafanya soka linakuwa rahisi sana kwa yanga, uwezo wake wa kupiga pasi za rotation ni bab kubwa.

Leta chama na wenzake fei pekee anatosha.

Haka ka bwana mdogo katafika mbali sana.

Pancho
 
Well said.....Fei Toto.
 
Fei Toto?

Hii Thread ameandika mwana yanga? Na ni mfuatiliaji mzuri wa muenendo wa timu?

Mimi karata ya kwanza kabisa naitupa kwa CEDRIC KAZE.

Karata ya pili naitupa naitupa kwa bek za kati za Yanga.

Fei toto hata asipocheza, nafasi ile akaa Haruna bado mambo yanakwenda vizuri.
 
Fei ni kiungo wa chini tangu lini haruna akacheza chini ?

Haruna anabadilishana namba na kina farid huko juu bwana ...fei na mukoko wapo chini..

Fei ni holding midfielder
 
Lakini kiukweli Kaze anaujua mpira aisee, acha tu.
 
Mtoa mada apimwe mkojo !!
Yaani kale ka Fei ?Fei kale kenye macho ya kurembua kama mwanaasha wa Tanga !kimtu kinajiangusha kama gunia la viazi vibichi !kimtu akina Stamina aisee wwe rudia kuangalia mpira ndo uje na porojo nyngne znazoshawishi
Wakati unandika ulishirikisha akili sawa sawa, jibu hoja acha personalities, Fei Toto, anaibeba timu vizuri sana, Kaze ajajua hilo, kadri anacheza anaimarika.

Fei ni hazina kwa Taifa pia

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mtoa mada apimwe mkojo !!
Yaani kale ka Fei ?Fei kale kenye macho ya kurembua kama mwanaasha wa Tanga !kimtu kinajiangusha kama gunia la viazi vibichi !kimtu akina Stamina aisee wwe rudia kuangalia mpira ndo uje na porojo nyngne znazoshawishi
Nadhani huwa unaangalia huo mpira peke ako ..

Kuna watu huwa mnafosi vitu ambavyo hamvijui..
Kiufupi hujui soka kuna wachezaji wanaopiga kazi na hawaonekani lakini kazi yao inaonekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…