Yanga kufika nusu fainali Klabu Bingwa Afrika 2022/23?

Yanga kufika nusu fainali Klabu Bingwa Afrika 2022/23?

Gordian Anduru

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2021
Posts
369
Reaction score
747
YANGA KUFIKA NUSU FAINALI KLABU BINGWA 2022/23?

Mwaka 1974 Klabu ya soka ya Simba ilipewa jukumu la kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika. Simba ambao walipata tiketi hiyo baada ya kutwaa ubingwa mwaka 1973 walijikuta wakiwa na deni kubwa kwa vile watani zao Yanga walikuwa wamefanya mambo makubwa yafuatayo:

Kwanza Yanga walikuwa wamechukua ubingwa wa Tanzania mara tano mfululizo (1968,69,70,71 na 72)

Pili walikuwa wametinga na robo fainali mbili za klabu bingwa (1969 na 1970) robo fainali ambazo zote Yanga ambazo zote mbili Yanga ilijikuta ikicheza na Asante kotoko ambao ndiyo waliochukua ubingwa wa afrika (1970)

Hata hivyo Simba hawakutishwa na rekodi za Yanga waliingia mashindanoni na kwenda moja kwa moja hadi nusu fainali ambapo walitolewa kwa matuta na Mehalla Al-Kubra ya Misri kwa lugha nyingine Simba walilipa deni na kuweka rekodi mpya.

Mwaka huu (2022/23) Yanga inaingia kwenye mashindano ya klabu bingwa wakiwa na deni kubwa kwa watani zao ambao nao wamefanya yafuatayo:

Kwanza wamechukua ubingwa Tanzania mara nne(04) mfululizo

Pili wameingia robo fainali mbili za klabu bingwa(2019 na 2020/21) Katika robo fainali mojawapo Simba imetolewa kwa matuta na Orlando Pirates wakati Robo fainali nyingine Kaizer Chiefs waliomba mpira uishe. Pia wameingia robo fainali ya kombe la shirikisho

Je, Yanga atafanya alichokifanya mtani wake mwaka 1974 kwa kulipa deni na kuweka rekodi mpya? Yetu macho.
 
The war is there hey fight fight we have already finished outside war fight fight ila manara ni mnafiki alijua mpira ni propaganda kama alivyokuwa simba yanga mkisimama wenyewe mtafika mbali ila kama manara ndo mshauri wenu basi subirini mcheze mechi 2 mrudi avic town mkaogelee.
 
Hizo record zinawafanya makolo wachague cha kucomment
Simba ilishacheza final club bingwa na Stella abadjan. Muulize huyo topolo mwenzako kwann hajaiweka???

Utopoloooo hamna cha kutamba mbelee ya mnyamaaa, yaan kwenye records tumewapiga KO za kwendaaa.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] byuti byuti.
 
Back
Top Bottom