Yanga kufungwa na Azam kumeiongezea umakini na makali

Yanga kufungwa na Azam kumeiongezea umakini na makali

Sasa wamefungwa tatu na Tabora aisee ndio watazidi kuwa makiniiiii balaaa
Bacca, yao, job, Boka na Andabwile wote walikosekana kwa wakati mmoja. Ujidanganye kuwa Yanga imeshuka Ili kutafuta furaha bandia.
 
Narudia tena,Makolo vipigo mfululizo vikianza hatutaki kuskiaa zile story za kina Mangungu tuachie timu yetu..
 
Oyaa kaliwa tena yanga vi2 vya nguvu haahaah umakini my foot? Makali my ass? Haahaahaahaahaaaaa
 
Yanga ilifungwa na Azam lakini wanaYanga wanaona poa tu. Kufungwa huku sio udhaifu bali ni mwanzo wa wachezaji na walimu kuongeza umakini na juhudi kwenye mechi.

Bila ya hivyo kiburi na kujiamini kulikopitiliza kungetamalaki kikosini. Hata wasanii wa hovyo walitunga nyimbo za kuwaaminisha wachezaji, walimu, viongozi na mashabiki kuwa Yanga haiwezi kufungwa, bila shaka nyimbo za aina hii zimejimaliza zenyewe baada ya Yanga kupoteza mechi dhidi ya Azam.

Hata hivyo, pamoja na kufungwa lakini Azam ndio waliokuwa wanaomba mechi iishe kwa ushindi wa tugoli tumoja dhidi ya Yanga yenyewe wachezaji pungufu.

Hii ni kuonyesha kuwa timu zote nchini zinaiheshimu sana Yanga.

Natabiri kuwa baada ya mchezo ule Yanga haitapoteza tena na itafungua ukurasa wa magoli mengi dhidi ya wapinzani na hkuna mchezaji atakaeshangaa wala kuhoji kama Gamondi atamsugulisha mbao ndefu kikosini.

Amepata sababu ya kuwanyima namba wachezaji wasiojituma na wanaopoteza nafasi za wazi.
Sio kweli kumeifungulia mikosi,Nuksi, na laana
 
Mechi zijazo msishangae tabora alitumia paketi moja,kuna atakayetumia hata mbili
Hata Juma Mgunda alikuwa na mawazo kama Yako. Alikaribia kabisa kufungwa 5 kama mambo yangekwenda vizuri.

Anaesema Yanga imeshuka kiwango hajui mpira.
 
Back
Top Bottom