Yanga kuna tatizo

Yanga kuna tatizo

Kwanza napenda kukiri kuwa mimi ni mpenzi wa Simba, hata hivyo kuna mambo mawili yamejitokeza wiki hii katika klabu ya Yanga ambayo yanafikirisha sana, na kutia shaka kama kuna weledi
  1. Kutoweka kwa benchi la ufundi; tangu Yanga imeanza pre season hakuna kinacho eleweka rasmi wako wapi wasaidizi wa kocha mkuu (Kocha msaidizi na kocha wa viungo). Wengine wanasema wamesusia kambi kwa sababu ya malimbikizo ya bonasi, wengine wanasema mikataba yao imeisha hivyo wanatafutwa wengine na wengine wanasema mchakato wa kuongeza mikataba bado hajakamilika. Kwa kweli haiingii akilini hata kidogo timu imeenda pre season na sasa inarejea haina hata kocha wa viungo, ni mazoezi gani wanafanya.
  2. Kichekesho kingine ni pre season ya siku nne Morocco, huku ni kuchezea pesa tu, utoke Tanzania na utumie siku 4 kusafiri (2 kwenda 2 kurudi) halafu ukae siku 4 tu pre season. Ni bora mara mia wangeenda hata pemba ambako wangefanya mazoezi ya muda mrefu. Huko Morocco walikoenda hata mechi 1 ya kirafiki hawakupata, wachezaji kama Aucho na Bangala wamefanya mazoezi siku 1 tu. Awali tulielezwa Yanga wangeondoka Morocco tarehe 27 na kufika tarehe 28 hivyo kuwahi mchezo wao wa wiki ya mwananchi tarehe 29. Kisingizio cha wachezaji 8 kuitwa timu za taifa hakina mantiki kwani Yanga ilikuwa na wachezaji 28 Morocco, na hata wakirejea kesho siwezi kuamini kwamba Yanga hawatafanya mazoezi bali watasubiria wachezaji wa timu za taifa. Mbona Simba yenye wachezaji 13 timu za taifa bado ipo Morocco.
Kuna tatizo Yanga, lakini bado haiwekwi wazi, na waandishi uchwara wa sports media za Tanzania wamewekwa mfukoni na hawafukuruti, yangetokea Simba haya ingekuwa ni scandal kubwa na big headings kwenye front pages, wachambuzi uchwara nao wangekesha kuchambua na kuisema vibaya Simba.
Tatizo unalo wewe usiejielewa, Una uhakika yanga inarudi bila mocha ata mmoja au usimba wako ndo umekutuma uongee hizo porojo zako za kwenye mitandao, maana kwa ulichokiandika inaonekana kabisa hauna taarifa za kutosha juu ya yanga isipokuwa chuki na taarifa udaku ndo umetuletea apa, unasema yanga kuna tatizo liseme basi hilo tatizo maaana pengine unalijua!
 
Tatizo unalo wewe usiejielewa, Una uhakika yanga inarudi bila mocha ata mmoja au usimba wako ndo umekutuma uongee hizo porojo zako za kwenye mitandao, maana kwa ulichokiandika inaonekana kabisa hauna taarifa za kutosha juu ya yanga isipokuwa chuki na taarifa udaku ndo umetuletea apa, unasema yanga kuna tatizo liseme basi hilo tatizo maaana pengine unalijua!
Mocha ndio nani, mi simjui, lakini Kama ulikuwa na maana ya kocha, sijasema Yanga haikuwa na kocha, ila benchi la ufundi halikukamilika kwa maana ya kocha wa viungo na kocha msaidizi hawakuwepo kambini Morocco
 
... unasema yanga kuna tatizo liseme basi hilo tatizo maaana pengine unalijua!
Mkuu, mbona ameshakuonyesha dalili za tatizo? Wachezaji wanapotoka katika mapumziko, huwa wanaanza na mazoezi ya viungo ili kuuweka mwili fit kwa kupokea mafunzo. Sasa kama timu haina kocha wa viungo, huko pre season ilianzaje hiyo programme? Nini kilikwamisha kocha asiwepo huko?
 
Mapungufu haya yangekuwa yako upande wa Simba wale vibaka wa E-FM wakiongozwa na mchichamwiba Kijola wangekesha hata siku tatu kupiga madongo.
leo Kitenge alikuwa anageuka msemaji wa yanga wenzake kila wakihoji anawakatisha anasema taarifa rasmi ila kiukweli mji walioenda una corona, makocha wasaidizi wamekimbia si ajabu walitegemea ofa mwenyeji wao akawatolea nje.
 
Back
Top Bottom