Yanga kuvutiwa na jezi ya Al Ahly ni jambo linalofikirisha sana

Yanga kuvutiwa na jezi ya Al Ahly ni jambo linalofikirisha sana

Miaka yote ya nyuma ilikuwa ni mwiko mshabiki wa Yanga kuipenda wala kuonyesha hisia zozote za kuvutiwa na jezi nyekundu kiasi kwamba mashabiki wa Yanga walikuwa wanapata wakati mgumu sana kushabikia timu za Ulaya ambazo nyingi kubwa zinavaa uzi mwekundu.

Sijajua kama haya ni mabadiliko ya tabia nchi ila Yanga ilipokwenda kucheza na Al Ahly hapa juzi kati, viongozi wa Yanga walipokwenda kutembelea makao makuu ya Al Ahly walionekana kuvutiwa sana na jezi zao, yaani walionyesha mahaba ndi ndi ndi na sitashangaa kukuta kuna viongozi ambao walizibusu zile jezi off-camera.

Tuyaache hayo, jambo lililonishangaza ni walivyokuwa wanazisifia zile jezi huku wamepatwa upofu na ububu wa ghafla kwa kushindwa kuona na kuongelea idadi ya matangazo ya biashara katika zile jezi. Kwa misimu kama miwili hivi zilizuka kejeli kuhusu idadi ya matangazo katika jezi za Simba hadi msemaji wa Yanga akaja na jina ambalo mpaka leo wanalitumia kuikejeli Simba.


Jezi ya Al Ahly ina matangazo zaidi ya moja kifuani achilia mbali logo ya Adidas ambaye ni kit supplier, matangazo mawili tofauti kwenye mikono yote miwili, tangazo karibu na makalio na wakati mwingine wanaweka tangazo sehemu ya jina la mchezaji.

Nangojea Al Ahly waanze kuitwa Makolo.
Siyo kila kitu unakiandikia uzi mkuu,nasubiri kwa hamu siku utakayoleta uzi kuhusu JINSI ULIVYOPATA MIMBA
 
Maelezo yote hayo lakini hakuna sehemu ulipoonesha wanavyovutiwa na izo jezi? Wewe ni zaidi ya mbumbumbu
Aiseeh hata mim sijaelewa alitaka kutuambia nin sisi wana jf sports manake kajipiga mitama sana mpaka kapoteza uelekeo.
Hata nyuzi ya kusajiliwa kwa Yao alikuja na porojo million ila kwasasa nadhani anaona aibu kweli Kila akiona ile comment yake.
Umbumbumbu ni kipaji hakizeeki.
 
Back
Top Bottom