Yanga mpende msipende lazima turudi kwenye bakuli

Yanga mpende msipende lazima turudi kwenye bakuli

Kwa hiyo huyo mbadala wake Sven anakuja kufanya kazi bure?
Hafanyi kazi bure, ila si kwa pesa zile alizokuwa akilipwa Aussems ilihali alikiuka masharti ya mkataba wake wa mwaka mmoja.
Alitakiwa kujitoa ama kupunguza kiwango cha mshahara wake nimeshawahi kueleza hili kwa kina humuhumu fatilia.

Hii kitu ni hesabu ambazo hazina uhalisia my friend.
Tupo hapa tutaona.
This is Simba brother, sio chura churani, mapato ya Simba ni makubwa makubwa sana kama viongozi wa klabu wakiamua kuyatilia maanani
 
Nafikiri bakuli lirudishwe kwa masharti maalum ili Yanga ipite salama kwenye kipindi hiki kigumu. Wanachama wachangie lakini viongozi wapewe muda na masharti kuwa ifikapo mwezi fulani timu iwe imeshapata mwekezaji/wawekezaji.

Viongozi nao wawe waungwana warudi kwa akina Mavunde na Mkuchika wawaombe waongoze tena zoezi la kubwa kuliko awamu ya pili ili kuokoa jahazi. Vinginevyo viongozi wakiwa wagumu timu inaweza kuingia kwenye matatizo zaidi kwani kuindesha timu kama Yanga ni gharama kubwa sana.
 
Kwa yaliyotolewa na mwenyekiti wa klabu ya Yanga,aisee inasikitisha,boat inaendelea kuzama

Hali ya kipesa ni mbaya zaidi kwenye klabu hii ya wananchi

Madeni zaidi ya bilioni 2 ni hatari hata kama ni mwekezaji ataogopa madeni ya Yanga

Tunaomba uongozi wa Yanga urudishe bakuli kwa wananchi kuokoa jahazi

Tarehe 4 January nitasafuri nje ya nchi kwa wiki
usiondoke kwanza mzee baba subiri game lipigwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe acha uongo hatukubebwa tuliwafunga tukaepuka kushuka daraja

Kama mlituachia kwa nini mlipiga Sahau Kambi mpaka keaho yake gazeti maarufu wakati huo likaandika
"SAHAU HATOSAHAU"
Sahau alipewa muamala na nyie mngeshuka daraja leo kama red stars
 
Kuwa mkwe
Simba haiendeshwi kwa mfumo wa Manji Comrade au unajisahaulisha?
Manji aliifanya chura churani kuwa dhamana ya mikopo yake kila kitu alikuwa anafanya yeye bila maandishi.
.
Mfano mzuri Simba SC imetenga billion 6+ kwa ajili ya sajili 2019/2020 wakati huo wanajua wataingiza billion 5+ kwenye vyanzo vya mapato mbalimbali vya klabu, na hili linatokea kutokana na timu kuwa na mashindano machache na yasiyo na fedha nyingi.
.
Muwekezaji wetu bwana Dewji anatoa pesa kutoka kwenye ule uwekezaji wake ndani ya klabu ambazo anafanyia biashara na pia anatoa pesa zingine kama shabiki au mwanachama anavyoweza kutoa kusaidia club hivyo ikitokea siku kaondoka kivyovyote Simba itaendelea kuwa under MeTL pamoja na Simba sports club company mpaka itakapoamuliwa vinginevyo!
6B kwa wachezaji gani..Kashata ambaye Kenya Harambee stars hawamtaki..wale wabrazil wahindi au yule mkongo pengine Shiboub kweli 6B au mnampiga Kanjibai
 
Yanga wakubali kubadilika, na kusema kweli wameshachelewa sana, wasiendelee kuchelewa.Tumekuwa tukisema haya kwa karibu 5 years now lakini watu wanajifichia kwenye historia za miaka ya kugombania uhuru. Dunia imebadilika!!!

Gharama za uendeshaji timu ni kubwa sana, huu sio wakati wa kusajili wachezaji kwa kuwanunulia redio au vitanda. S
Mikia mnatoa hela wapi?kwa ajili sportpesa mnapata pungufu ya Yanga labda MO anatoa hela ya familia thats wrong
 
Kipindi hicho cha bakuli yanga mtakua mnajifariji na wimbo wa wajina wenu aitwae Mc yanga chief hip hop artist kutoka sauzi na wimbo wake wa not enough al maarufu kwa not enuff

 
Kuwa mkwe

6B kwa wachezaji gani..Kashata ambaye Kenya Harambee stars hawamtaki..wale wabrazil wahindi au yule mkongo pengine Shiboub kweli 6B au mnampiga Kanjibai
We kweli king'asti katika wachezaji Shiboub ndio umemuona mchezaji?😝😝😝 huyo msimu ujao hatumuhitaji luckily ana mkataba wa mwaka mmoja tu.
.
Sijawahi kuwaona Wabrazil -Wahindi toka nizaliwe, Francis Kahata ni bonge moja la midfielder alikuwa bado haja_gain momentum tu sasa hivi nadhani unaona, Deo Kanda age yake ni kubwa ila bado ni mchezaji mzuri luckily naye ana mkataba wa mwaka mmoja ukiisha kwao
 
sasa ni dhahiri kabisa kwamba bila PESA mpira haupo. Poleni wana YANGA....maana ngalawa yenu ndiyo hiyo ishaanza kuchota maji.
 
Back
Top Bottom