SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Tunajua upande wa pili bado wamepigwa na butwaa wa hizi sajili zinazoendelea pale Msimbazi. Msimu huu ulioisha kuna mambo yaliyotokea katika ligi na hasa mashindano ya kimataifa ambayo kwa kweli yalituumiza sana wanaSimba. Sitaongelea sana ligi ya NBC maana huku tulikuwa tunawamudu ni basi tu kuna steps chache tuliteleza ila nitagusia mashindano ya kimataifa.
Ni kweli Yanga walifika fainali ya shirikisho kwa ubovu wa timu walizokutana nazo ila haipingiki kuwa Yanga msimu uliopita walikuwa na focus na nidhamu ya hali ya juu uwanjani na nje ya uwanja. Tulipowakumbusha hata sisi fainali tulifika, hawakutaka kusikia hili wala lile na nguvu yao ilikuwa kubwa sana kupinga kumbukumbu hiyo. Hawa washenzi wako vizuri kwenye idara ya propaganda. Huko CAF mambo yao yalikuwa yanakwenda yamenyooka kama rula. Dua zetu zilikuwa wakwame ila kila hatua kenge wale walikuwa wanatembea tu, kwa kweli tulipata ahueni sana walipokosa lile kombe maana daah!! Kamba tu zile walizopata wamekuja kutupulizia mimoshi pale Msimbazi, ingekuwa ndoo je?
Safari hii hatutaki hali ile ijirudie, huu ni wivu wa maendeleo tu. Hatutazuia wala kuwafanyia fitna wanachofanya wao ila tutahakikisha mafanikio yetu kimataifa yanazidi yao. Hii ndiyo siri ya usajili huu wa kutisha na wa hasira. Na hivi CAF wamehakikisha janja janja ya kudondokea shirikisho haiwezi kuwepo, basi tupo tayari kupimana makali.
Kila la kheri.