Yanga na Simba kuingia Robo Fainali katika mashindano yao wanayoshiriki siyo mafanikio

lufungulo k

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Posts
2,601
Reaction score
2,058
Mimi nikiwa ni mdau wa soka, Nashangazwa na sifa ,majigambo na majivuno wanayojipatia mashabiki , wapenzi , viongozi na waandishi wa habari za michezo kuwa HATUA YA ROBO FAINALI YA MASHINDANO YA AFRIKA yaliyofikiwa na vilabu hivi eti tunaita MAFANIKIO.

Huo ni UONGO, UZEMBE NA UDWANZI, mafanikio yoyote katika mashindano ni kutwaa MATAJI. Kama timu yako haijawahi kutwaa taji katika mashindano inayoshiriki USIITE MAFANIKIO.

Hio ni KUSHIRIKI tu. Lakini sababu ya UONGO, UZEMBE NA UDWANZI ndo maana eti TUNATAMBA NA KUITA mafanikio kitendo cha kufika ROBO.

Sasa unafika ROBO halafu unajisifia! Jiulize hivi GEITA GOLD kwenye kombe la FA ilipofungwa na YANGA mwaka jana pale LUPASO walifurahia. Eti kwa sababu wametolewa ROBO fainali? Hakuna walisikitika kwa sababu MAFANIKIO NI KUBEBA KOMBE.

TUACHENI, UONGO, UZEMBE NA UDWANZI pesa ya mama ni kichocheo cha kuhakikisha tunafikia mafanikio ambayo ni KUBEBA MAKOMBE.
 
Una hoja ya msingi lakini...

Any way, kwenye kushindania gari na pikipiki , ukiishia hatua ya kushinda pikipiki nayo ni hatua ya mafanikio japo hajafikia mafanikio kamili. Si sawa na ambae hajapata kabisa.

Robo fainali wanapata commission kutoka CAF.
 
Ni ushamba tu unawasumbua, vilabu viliozoea kufika fainali wala husikii waandishi wao na mashirikisho yao ya mpira wa miguu yakipoteza muda kujidadavua kwamba timu zao zimefika robo fainali. Ama kweli masikini akipata ........ Kama vipi wafike fainali na wachukue kombe, hapo walau italeta maana kwa kuwa ni mara yao ya kwanza
 
Naomba nichangie mada.
Naomba kutoa mfano. Wewe ni mzazi, na mwanao tangu darasa la kwanza hafaulu au hafanyi vizuri kwenye mitihani yake. Anapata D na F kila somo (wanatolewa hatua ya awali ya mashindano ya CAF kila mwaka). Unatoa msaada wa kumpa moyo na msaada wa kusoma zaidi na pia kulipia madarasa ya ziada (wadhamini wanaanza kujitokeza kama Mo Dewji na GSM). Hatua kwa hatua anaanza kufaulu madarasa yake na anaanza kupata B na C kila somo(kufika hatua ya makundi na robo fainali). Nina uhakika kama mzazi utafurahi sana na kumpa moyo zaidi ili aweze kufaulu zaidi na kupata A (kufika nusu fainali/fainali/kombe ya CAF). Punde atakapokuwa anapata A tu, hutakuwa na mshangao mkubwa kwani unaona alipotoka na anapoenda. Hii ndio simulizi ya mpira wa Tanzania toka uhuru.
Hapa ni ndipo walipo Simba na Yanga. Walitoka kutokuwa washindani kabisa wa mashindano ya Africa na sasa wana mawazo ya kuingia nusu fainali/fainali na siku za mbele hata kubeba kombe. Mie ninakaribia miaka 50 duniani. Nakumbuka mafanikio ya simba na Yanga yalikuwa kufungana wao kwa wao tu. Hakuna aliyejali mashindano ya kimataifa kwa sababu walikuwa sio washindani kabisa. Mie ninaishi Marekani na sasa napata fursa ya kuwaangalia wote wawili (ingawa mie ni mpenzi mkubwa wa Simba SC) kupitia TV live (beIN Sports kwa mashindano ya Africa) na app ya Azam kwa ligi ya Tanzania. Ingawa nimeishi hapa miaka zaidi ya 25, sikosi kuangalia mechi zao. Kwa kweli mpira wa Tanzania umetoka mbali sana.
Kwa mzazi wa mtoto anayepata A darasani (Al Ahly, Zamalek, Esperance, Wydad, Raja, Mamelodi Sundowns), hakuna cha kushangaza kuendelea kupata A. Wasipopata A (kushinda makombe ya Africa), ni mshangazo na hatua kali huchukuliwa kama kusoma zaidi na madarasa ya ziada, kuchapwa (kutimuliwa kocha, kutimuliwa wachezaji, kukatwa mishahara, etc). Ni hatua ambayo Simba na Yanga wakiifikia, haitakuwa mshangao tena. Nafikiri umenielewa ninachomaanisha.
Naomba kuwasilisha/My 2 cents.
 
Una hoja ya msingi lakini...

Any way, kwenye kushindania gari na pikipiki , ukiishia hatua ya kushinda pikipiki nayo ni hatua ya mafanikio japo hajafikia mafanikio kamili. Si sawa na ambae hajapata kabisa.

Robo fainali wanapata commission kutoka CAF.
Sina shida na hilo, ndo maana kuna neno mshindi 1, 2, 3 wengine ni washiriki kama kuna bonus ya kifuta machoni wanapewa .

Kuna ligi zile za ambazo timu imekosa kunyakua kombe, basi inapambana kutafuta nafasi za ushiriki wa mechi za kimataifa.

Hawawezi kuita MAFANIKIO.
 
Una hoja ya msingi lakini...

Any way, kwenye kushindania gari na pikipiki , ukiishia hatua ya kushinda pikipiki nayo ni hatua ya mafanikio japo hajafikia mafanikio kamili. Si sawa na ambae hajapata kabisa.

Robo fainali wanapata commission kutoka CAF.
Sio Commision tu, ni Bilioni 1.5, ligi yenyewe hawapati hizi hela.
 
Sawa yaweza kuwa hawajafikia mafanikio ila kuna rekodi fulani wameweka, kwenye mpira huwa wanaheshimu rekodi kadhaa zinazowekwa hata kama hazijapelekea kwenye mafanikio, ila zinakumbukwa

Ni kama Morocco ambavyo ilishindwa kuwa nchi ya kwanza ya Africa kuchukua kombe la dunia, lakini ikaweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza ya Africa kufika mpaka nusu fainali za kombe la dunia, hiyo ni rekodi

Au Cameroon ilivyoweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza ya Africa kuifunga Brazil kwenye michuano ya kombe la dunia pamoja na kwamba haikufika hata 16 bora ya michuano hiyo na kuishia hatua ya makundi tu
 
Kumbe unaujua mpira?
 
Mimi nikiwa ni mdau wa soka, Nashangazwa na sifa ,majigambo na majivuno wanayojipatia mashabiki , wapenzi , viongozi na waandishi wa habari za michezo kuwa HATUA YA ROBO FAINALI YA MASHINDANO YA AFRIKA yaliyofikiwa na vilabu hivi eti tunaita MAFANIKIO.

Huo ni UONGO, UZEMBE NA UDWANZI, mafanikio yoyote katika mashindano ni kutwaa MATAJI. Kama timu yako haijawahi kutwaa taji katika mashindano inayoshiriki USIITE MAFANIKIO.

Hio ni KUSHIRIKI tu. Lakini sababu ya UONGO, UZEMBE NA UDWANZI ndo maana eti TUNATAMBA NA KUITA mafanikio kitendo cha kufika ROBO.

Sasa unafika ROBO halafu unajisifia! Jiulize hivi GEITA GOLD kwenye kombe la FA ilipofungwa na YANGA mwaka jana pale LUPASO walifurahia. Eti kwa sababu wametolewa ROBO fainali? Hakuna walisikitika kwa sababu MAFANIKIO NI KUBEBA KOMBE.

TUACHENI, UONGO, UZEMBE NA UDWANZI pesa ya mama ni kichocheo cha kuhakikisha tunafikia mafanikio ambayo ni KUBEBA MAKOMBE.
Ubebe makombe kwa kikosi gani we mama?
 
Ukitumia fikra pevu utajua mafanikio ni Nini na utajua kuwa mafanikio sio kupata ushindi wa juu zaidi tu Bali kufikia hatuna ambayo hujawahi kuyafikia katika mazoea yako
 
Mafanikio katika soka ni KUNYAKUA MATAJI kwa mashindano UNAYOSHIRIKI.

Mambo mengine ni KUJIFARIJI.
 
Sawa yaweza kuwa hawajafikia mafanikio ila kuna rekodi fulani wameweka, kwenye mpira huwa wanaheshimu rekodi kadhaa zinazowekwa hata kama hazijapelekea kwenye mafanikio, ila zinakumbukwa

Ni kama Morocco ambavyo ilishindwa kuwa nchi ya kwanza ya Africa kuchukua kombe la dunia, lakini ikaweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza ya Africa kufika mpaka nusu fainali za kombe la dunia, hiyo ni rekodi

Au Cameroon ilivyoweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza ya Africa kuifunga Brazil kwenye michuano ya kombe la dunia pamoja na kwamba haikufika hata 16 bora ya michuano hiyo na kuishia hatua ya makundi tu
Una hoja safi kweli asee.
 
Back
Top Bottom